kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
KWA muda mrefu sasa Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikichukua hatua za kupunguza gharama za maisha ya Watanzania, kubana matumizi ya serikali na kuhakikisha miradi ya kuondoa kero za wananchi, inatekelezwa kikamilifu.
Hakuna Mtanzania ambaye hajaona juhudi za serikali hii tangu ilipoingia madarakani, wakati Rais John Magufuli alipotangaza hatua za haraka za kudhibiti matumizi katika safari za nje, kubana mianya ya upotevu wa mapato na kuelekeza fedha katika miradi ya kuondoa kero za wananchi.
Kila mmoja wetu ni shahidi kuwa serikali hii ilipoingia tu madarakani, baada ya muda mfupi mapato ya serikali yaliongezeka na gharama za serikali zikapungua, hatua inayoonesha kuwa imewezesha kupata ziada ya kupeleka katika miradi ya kuondoa kero za wananchi.
Hata hivyo, pamoja na mafanikio ya hatua zilizochukuliwa katika muda mfupi tu wa serikali hii, kumeibuka siasa tofauti na za kidemokrasia, badala ya kushiriki kuongeza kasi katika maendeleo, zinatumika kupunguza kasi ya maendeleo.
Leo hii, siku chache tangu kuanza kwa mwaka wa kwanza wa fedha wa Serikali ya Awamu ya Tano, tumeshuhudia bajeti ya kwanza ikitenga asilimia 40 katika miradi ya maendeleo, hii haijapata kutokea, lakini baadhi ya wanasiasa wakisusa kutoa maoni yao kuhusu namna ya kuiboresha.
Pamoja na siasa hizo, wananchi wameendelea kushuhudia, sekta wezeshi katika kuchochea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla ya nishati, ikitengewa fedha nyingi kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo na kusambaza umeme kwa Watanzania wengi zaidi.
Kwa haya machache kati ya mengi ambayo wananchi wameyaona, ikiwemo kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma, kudhibiti ubadhirifu na mengine kama miradi mikubwa ya kipaumbele kwa kutaja machache, serikali hii ina kila sababu ya kuungwa mkono, si tu na wanachama wa chama tawala, bali na Watanzania wote ikiwemo vyama vya upinzani.
Ni kwa mantiki hiyo, sisi tunaungana na wote wanaounga mkono hatua njema za serikali katika kuletea maendeleo Watanzania, huku tukishiriki katika kuhakikisha wanaokwaza maendeleo popote, ndani au nje ya serikali, hawafanikiwi.
Kwa msimamo huo, tunashauri siasa za aina hii zisiungwe mkono kwa kuwa hazina tija katika kuongeza uzalishaji katika ngazi ya kaya wala katika ngazi ya taifa. Inawezekana wanaofanya siasa hizo, kwao mkono utakwenda kinywani, lakini mchango wao katika kusaidia mkono mnene wa walio wengi kwenda kinywani kama wao ni mdogo au haupo kabisa.
Hiyo si demokrasia hata kidogo. Siasa hizo ni ghasia hata kama zitapewa jina la kudai demokrasia, kwa kuwa hazisaidii katika kuboresha maisha ya wananchi, bali zinarudisha nyuma hatua nzuri zilizoanza kuonekana katika maisha ya Watanzania.
Umefika wakati Watanzania tukatae siasa hizo, kwa kuwa hata huko katika nchi zenye uzoefu mkubwa na zilizokomaa kidemokrasia, baada ya uchaguzi, kila mtu ni kazi kwa kuwa bila kazi, hakuna chakula, kulala, kuvaa wala maisha mazuri