Siasa za upinzani Tanzania utata

hindikwetu

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
251
86
Ukiangalia,jinsi mataifa mengine hasa ya Ulaya,kijiti cha siasa ni mara nyingi hupokezana,zipo sababu kadhaa kwanini wanapokezana,kwanza vyama vina kuwa na misimamo ya kisera,na si misimamo ya kimalumbano na kusubiria tu chama tawala kikosee mahala ndo,igeuke kuwa sera,ajenda na mjadala wa chama,hapo ndipo tunapopishana na siasa za huku kwetu.
Kwa mfumo huu kupokezana kijiti yaweza kuwa ni ndoto ambayo itakuwa mbali sana,maana mikasa ya kisiasa inapopungua na harakati za upinzani hupungua ni kama hawana kazi za kila za kila siku za kichama kwa mtaji huu ujenzi wa vyama vyao pia ni ngumu.NIngependa kuona mikakati hasa ya upinzani,zaidi ya kuona uhai wa vyama hivyo pale mshale wamatukio tu ya kisiasa unapo panda.Swali hapa nini kifanyike tuwe na upinzani ambao pamoja na mambo mengine lakini pia ujenzi wa vyama na ukuzaji sera zao
 
Back
Top Bottom