ikigoma iwachu
Member
- Aug 23, 2013
- 71
- 10
SIku za karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Viongozi, Wanachama maarufu, na watu wa kutegemewa kwenye vyama vya upinzani na hata CCM kuhama kwa visingizio kuwa wanaridhishwa na juhudi za JPM. Huku wale wa CCM wakidai demokrasia ina minywa! Binafsi nashangaaa! Kinachonifanya nishangae ni kudhani hao VIONGOZI wamejiweka kwenye hizo nafasi hivyo wanaweza kuwafanya waliowachagua kuwa ni wajinga kiasi cha kuvunja matumaini yao bila kuwashirikisha!
Pia hivi kweli demokrasia yetu imefikia kiasi cha kuamini utendaji wa Mtu? Wakati mfumo mzima bado upo vilevile? Yaani unawezaje kuziamini juhudi za JPM za kupambana na hali tuliyonayo wakati unajua kuwa ikitokea muda wake ukaisha hakuna uhakika wa mazuri yake kuendelezwa?
Mimi nilidhani huu ndo ulikuwa muda mwafaka kudai misingi imara ya nchi na siyo kujichanganya kwa kudai unaridhishwa na utendaji wa VIONGOZI wa serikali!
Hamuoni kama mnatusaliti sisi tuliowapa dhamana? Na unadhani mnastahili adhabu gani? Huwa nasema itafikia kipindi uchaguzi utakuwa mnaenda wagombea tu na hao askari maana akili zetu mnazichezea! Yaani tuwaamini halafu baada ya wiki unatuambia umeona umepotea sasa unarudi kwenye NURU! Huo ni usaliti na unafiki? Na watu kama nyie nchi za wenzetu mnastahili kupunguziwa muda wa kuishi katika sayari hii!