Siasa za ubinafsi zinanyong'onyeza nafasi ya Tanzania ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

F.S

Member
Sep 5, 2014
34
26
Jumuiya ya afrika mashariki ni tunda la kila nchi mwanachama, hivyo ni jukumu la kila nchi mwanachama kuwa na mipango na mikakati mathubuti katika kuitetea nafasi yao katika kuijenga nchi yao.

katika afrika mashariki tumeona nchi za wenzetu kama Kenya na Rwanda kuchagua wabunge wa EAC kimkakati katika kuimarisha utaifa wao na uchumi.Wenzetu wanaona miaka 100 mbele, hawataki kupoteza hata sekunde, ilimraidi wamepata fursa kwenye jumuiya ya Afrika mashariki bhasi nao hawafanyi makosa katika teuzi zao. Wanateua watu ambao ni hazina kwa taifa lao na jukumu kubwa mi kufungua milango imara ya kiuchumi.

Inaumiza sana pale tanzania tunapoweka siasa mbele na kuuzika utaifa. inaumiza sana kuona uccm na uchadema umetawala chaguzi hizi ambazo ni fursa pekee kama taifa kupeleka watu imara na wenye uelewa mkubwa wa mataifa jirani na fursa zilizopo ndani ya jumuiya, watu wenye weledi mkubwa na uwezo wa kuitetea nchi yao kwa nguvu zote.

Ifike mahali kama taifa tuuweke utaifa wetu mbele. kiukweli Laurance Masha alistahili na alitosha kuwa sehemu ya jopo la watakaoibeba Tanzania kwenye medani hii ya EAC, lakini kwa kuwa siasa zimekuwa mbele na utaifa tumeuacha nyuma bhasi tumemuondoa kwenye nafasi hiyo adhimu.

sio kwamba waliochaguliwa hawafai au hawana uwezo, La hasha, katika wote waliojinadi leo Masha alionyesha uwezo wa hali ya juu. wakina mama mnaweza Sana, lakini Masha viatu vilimtosha zaidi.

Siasa tukiziendeleza zitalitafuna taifa sana. Ni muhimu ifike sehemu tuheshimu utaifa wetu na tupambane kupasua anga za kiuchumi duniani kama wenzetu kenya na Rwanda. Teuzi hizi zisiwe kichaka na siasa au kujuana bali zitolewe na mchakato mzima ufanywe kimpango mkakati wenye lengo la kuijenga Tanzania imara zaidi kiuchumi.

Hongereni sana Pamela Maasai na Josephine Lemoyan kwa ushindi wa kishindo. Mkaitendee haki Tanzania.

Wasalaam
-Chief F.S.M
e2853036ebf1bef23e9b3afab6ad8504.jpg
 
Kuna haja ya wabunge kupewa elimu ni kwa jinsi gani ushiriki wa Tz katika Bunge la EA unaweza kulifanya taifa kupiga hatua. Wengi hupiga kura bila kufahamu kiundani kazi za mwakalishi na role ya bunge la africa mashariki katika maendeleo ya Tz pia mahusiano na nchi washiriki.
 
Kuna haja ya wabunge kupewa elimu ni kwa jinsi gani ushiriki wa Tz katika Bunge la EA unaweza kulifanya taifa kupiga hatua. Wengi hupiga kura bila kufahamu kiundani kazi za mwakalishi na role ya bunge la africa mashariki katika maendeleo ya Tz pia mahusiano na nchi washiriki.

WANAJUA NDUGU, SHIDA SIO TRAINING WALA, SHIDA NI KUWA WAZALENDO, MIMI WALA SIKUTAKA KUFUATILIYA. NILIJUA TU HAYA YANGETOKEA. HAWA JAMAA WALIPASWA PITA TOKA KIPINDI KILE CHA KWANZA. DUNIA YA LEO ITATUCHEKA, SASA NA SISI TUSIWACHAGUE, MAANA WAO PILA WALICHAGULIWA NA SISI.
 
Back
Top Bottom