Siasa za Tanzania zinapogeuzwa kama mchawi.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Moja ya sifa kuu ya mchawi ni kuhakikisha juhudi za binadamu mwingine kimaendeleo hazifanikiwi.

Siasa za Tanzania kwa sasa zinakoelekea ni kama mapambano kati ya wachawi wachache na wanajuhudi wengi wa maendeleo. Kinachoanza kuonekana ni kama kundi la watu wachache liko nyuma ya pazia la kisiasa likisubiri kuloga ili kuhakikisha juhudi za wananchi wengi wapenda maendeleo zisifanikiwe.

Kuna baadhi ya watu kwa sasa wanapata faraja na furaha sana pindi serikali ya awamu ya tano inapojikwaa katika juhudi zake za kuwaongoza wapenda maendeleo nchini ili wafike salama katika jamii yenye uchumi wa kati mwaka 2015.

Kila serikali inapojikwaa utawaona wanajitikeza na kuanza kusema, ''Tulisema'' lakini huwezi kuwaona wanajitokeza pale serikali inapofanikiwa katika kazi zake.

Kuomba na kusubiri serikali ijikwae ili matamanio yao yatimie ni sawa na mchawi anayeloga au kuomba mabaya yawafike binadamu wengine.

Wananchi wengi walimchagua Rais Magufuli siyo kwa sababu waliamini ni maraika, la hasha. Wananchi wengi walimchagua Rais Magufuli wakifahamu vizuri kuwa ana mapungufu na pia anatoka katika chama ambacho kimewaangusha sana wananchi wengi wakati wa vita vya kupata maendeleo ya haraka. Ieleweke Magufuli alikuwa bora zaidi ukilinganisha na wagombea wengine wa Urais Tanzania wa Uchaguzi Mkuu 2015.

Aliyewahi kuwa USA Defense Secretary, Donald Rumsfeld aliwahi kusema, “You go to war with the army you have, not the army you might want or wish you had at a later time.”

We are at war against poverty, ignorance, diseases and grand corruption (ufisadi) with the army we have (Rais Magufuli & cabinet), not the army others might want or wish to have. The only weapon is our own determination, efforts and unity.

We've got to empower ourselves through unity and efforts to determine the fate of our beloved country.

Amiri Jeshi amepatikana na kwa sasa nchi iko vitani. Kuendelea kuwa kama Mchawi huku ukibeza wakati mazingira katika vita yanakugusa moja kwa moja ni sawa na mjinga au mpumbavu aliyeko vitani lakini anataka aangamie ili matamanio yake ya kushindwa vita yatimie.

Maendeleo ya haraka hayawezi kupatikana wakati kuna baadhi ya watu bado wako kwenye negative campaign mode and defeatism.

Serikali ni wewe, mimi na yule na pia mafanikio ya serikali ni akisi letu kitaifa.
 
ukiona hivyo ujue wengi hawakumchagua,hata hivyo hii serikali bado ni ya kimaigizo.kwa sasa toka mwezi 10 mwaka jana hamna maendeleo yyte ambayo yamefanyika.hamna hela yoyote toka serikalini kwenda halmashauri/Mji/manispaa yoyote Tanzania sasa hayo maendeleo yatatoka wapi?
 
Juhudi za kuleta maendeleo ya nchi hii haziwezi kuletwa na ccm,yaani chama hicho hicho cha watu wale wale,Sera zile zile,akili zile zile kishindwe kuleta maendeleo in 50 years kiweze kwa miaka kumi?kama unaona serikali ya kweli serikali ya awamu ya tano inania ya kuleta maendeleo washauri waanza kuweka mifumo ya kuwezesha maendeleo hayo kutokea tukianzia na katiba bora ya nchi uone kama utaweza
 
Unaposeama "Serikali ni wewe, mimi na yule", wakati huohuo unasema "the army (rais & baraza lake la mawaziri) ndio wako vitani' unamaanisha nini?

Halafu kwa akili zako nyingi kama unavyojinasibu humu kwanini unasahau kuwa hili ni taifa la kidemokrasia, open society & open government whatever that means!, kwanini hupendi/hutaki kusikia third part opinion?
 
Nadhani hujasoma vizuri andiko langu au kama umesoma basi utakuwa hujaelewa vizuri.

Kuhusu maendeleo na pesa kupelekwa kwenye halmashauri/Mji/Manispaa, Serikali hii haijatoa bajeti yake kwa sababu bado huu ni mwaka wa bajeti ya 2015/16.
 
Juhudi za kuleta maendeleo ya nchi hii haziwezi kuletwa na ccm,yaani chama hicho hicho cha watu wale wale,Sera zile zile,akili zile zile kishindwe kuleta maendeleo in 50 years kiweze kwa miaka kumi?kama unaona serikali ya kweli serikali ya awamu ya tano inania ya kuleta maendeleo washauri waanza kuweka mifumo ya kuwezesha maendeleo hayo kutokea tukianzia na katiba bora ya nchi uone kama utaweza
Nani alikuambia juhudi za kuleta maendeleo zinaletwa na chama?

Juhudi za kuleta maendeleo zinaletwa na wananchi wenyewe!

Kazi ya serikali ni kuwaongoza wananchi katika kupata maendeleo.
 
Unaposeama "Serikali ni wewe, mimi na yule", wakati huohuo unasema "the army (rais & baraza lake la mawaziri) ndio wako vitani' unamaanisha nini?
Siyo lazima uwe mstari wa mbele vitani ndio uhesabike uko vitani.

Hata Taifa lilipoingia vitani ili kupambana na Idd Amin, hata watanzania ambao hawakuwa mstali wa mbele vitani, kwa maana nyingine hawakuvaa magwanda ya jeshi, huwezi kusema hawakupigana vita.

Hata kutoa mchango wa unga ili wapambanaji walioko mstari wa mbele wapate chakula inahesabika ni mchango vitani.

Halafu kwa akili zako nyingi kama unavyojinasibu humu kwanini unasahau kuwa hili ni taifa la kidemokrasia, open society & open government whatever that means!, kwanini hupendi/hutaki kusikia third part opinion?
Nani amekuambia sipendi/sitaki kusikia third part opinion?

Toka lini wachawi wakawa na constructive opinion zaidi ya kuloga au kuombea mabaya yawafike wengine.
 
Mkuu bora hata ya mchawi,kuna watu wamefikia kusema bora wazungu warudi waje kututawala tena.
Watu wanashindwa kutofautisha kukosoa na kuponda.
 
Siyo lazima uwe mstari wa mbele vitani ndio uhesabike uko vitani.

Hata Taifa lilipoingia vitani ili kupambana na Idd Amin, hata watanzania ambao hawakuwa mstali wa mbele vitani, kwa maana nyingine hawakuvaa magwanda ya jeshi, huwezi kusema hawakupigana vita.

Hata kutoa mchango wa unga ili wapambanaji walioko mstari wa mbele wapate chakula inahesabika ni mchango vitani.

Nani amekuambia sipendi/sitaki kusikia third part opinion?

Toka lini wachawi wakawa na constructive opinion zaidi ya kuloga au kuombea mabaya yawafike wengine.
Endelea kutafuta wachawi sasa!

Ukiamka na kukuta mchawi wewe mwenyewe, ndipo utajua kwanini vipele vimezunguka macho yako!!
 
Serikali hii ya Ccm bado ni yamaigizo, hawana ubavu wa kupambana na ufisadi na rushwa. Wao ndio waasisi wa ufisadi na rushwa tokea tulivo pata uhuru halafu eti wao wenyewe ndio wapambanaji wa walicho kiasisi.
 
MsemajiUkweli,

..mkimsifia sana Magufuli atabweteka na kuharibu kazi.

..mimi naona ni bora wakosoaji wawepo, tena wengi, ili kuhakikisha Magufuli anakuwa alert wakati wote.

..vyombo vya habari lazima viwe huru zaidi. bunge lazima lipewe meno na uhuru wa kuisimamia serikali. mahakama nazo ziwe huru na zenye maadili.

cc Bukanga
 
Mkuu bora hata ya mchawi,kuna watu wamefikia kusema bora wazungu warudi waje kututawala tena.
Watu wanashindwa kutofautisha kukosoa na kuponda.
Mimi sina tatizo na watu wanafanya constructive criticism. Hata mimi ni mmoja wao ili kuweka serikali katika njia nzuri.

Tatizo langu ni kwa wale wameuvaa uchawi huku wakividhia serikali ijikwae katika utendaji ili wa-prove eti walichokuwa wanakisema kimekuwa vindicated or justified.
 
Endelea kutafuta wachawi sasa!

Ukiamka na kukuta mchawi wewe mwenyewe, ndipo utajua kwanini vipele vimezunguka macho yako!!
Kwa nini niwatafute wakati wapo na wanaonekana vizuri ukitumia 3D thinking!
 
MsemajiUkweli,

..mkimsifia sana Magufuli atabweteka na kuharibu kazi.

..mimi naona ni bora wakosoaji wawepo, tena wengi, ili kuhakikisha Magufuli anakuwa alert wakati wote.

..vyombo vya habari lazima viwe huru zaidi. bunge lazima lipewe meno na uhuru wa kuisimamia serikali. mahakama nazo ziwe huru na zenye maadili.

cc Bukanga
JokaKuu, Kupinga hoja kwa dhumuni la kujenga ni kitu kizuri, ila kuna baadhi ya watu nia yao si kujenga, furaha yao ni kuona Magu ameshindwa kitu fulani, na wao wanajiita wazalendo, wanaitakia mema Tz.

Vilevile kuna tabia ya ajabu na mbaya imejengeka sanasana katika kundi la vijana wa kitanzania, tabia ya mtu anayepinga ovyo ovyo ndio anajiona ana akili na mjanja, jinsi muda unavyoenda itafika kipindi mtu hata akipinga kwa hoja atadharauliwa na kuonekana anapinga pinga tu kwa sababu ya precedence inayojengwa saivi ya kupinga pinga tu ovyo.

Kuendelea kuupa promo yoyote huu upingaji wa ovyo ovyo na kichawa( as per msemakweli ) ni kuua, saivi si ajabu kuona vijana wanaojinasibu wa UKAWA wakitetea hata wizi, ubadhirifu na uwajibikija ili mradi tu wawe wamepinga, mwisho wa siku watakuja kuwa #LGBT activists kama sio wachawi.
 
ukiona hivyo ujue wengi hawakumchagua,hata hivyo hii serikali bado ni ya kimaigizo.kwa sasa toka mwezi 10 mwaka jana hamna maendeleo yyte ambayo yamefanyika.hamna hela yoyote toka serikalini kwenda halmashauri/Mji/manispaa yoyote Tanzania sasa hayo maendeleo yatatoka wapi?
Sidhani kama ni kweli unachokisema. Hao wengi mimi naona ni watu wa jf waliong'ang'aniwa na mitizamo ya kisiasa iliyo katika misingi ya adui muombee njaa ndo hata wanakosoa hata mambo yasiyokuwa na tija kama vile; Mecky Sadiki kaambiwa nini! Rais kameza vidonge! Lakini ukifuatalia haya tafiti ndogo zinazofanywa na vyombo vya habari utaona Wananchi wapo upande gani. Siyo siri wananchi waliowengi sasa hivi wanamatumaini si kama zamani japo hakuna makubwa sana yaliyofanywa ukiachia mbali kuirudisha heshima ya Mtanzania katika maeneo mbalimbali ya huduma za umma.
 
Back
Top Bottom