Kwa muda sasa tumeshuhudia wapinzani wakijenga hoja nzuri na fikirishi bungeni. Lakini wenzao wa chama tawala wamekuwa mahiri kwa mipasho, vijembe na kejeli huku wakipitisha mambo kwa mgongo wa wingi wao.
Wabunge wa ccm wanaendeshwa na mihemko ya kisiasa badala ya kutoa hoja zinazojenga taifa kwa maana ya kuikosoa serikali inapokosea ama kuishauri serikali.
Wabunge wa upinzani wamekuwa wakikumba na madhila ya kupewa adhabu ya kutohudhuria bunge kwa kipndi fulani ama kutolewa nje kwa nguvu na polisi. Chanzo cha yote haya ni hoja nzito zenye mantiki ambazo ccm na serikali yake huziona ni mwiba kisiasa.
Kwa nyakati tofauti wabunge wa upinzani wamekuwa wakitoka nje ya bunge kuonyesha kutokubaliana na mambo yanayoendelea ndani ya bunge. Jambo hili limetokea mara nyingi sana. Na mara zote likitokea ccm huendeleza yao. Tabia hii ya ccm kupuuza hoja na shinikizi la wapinzani sasa inaota usugu.
Wakati umefika sasa wa wabunge wa upinzani kubadilisha mbinu ya kudai haki bungeni. Kama busara imeshindikana basi wabunge wa upinzani muanze kuingia bungeni na filimbi za kupigia kelele pale mnapo onewa ama kupuuzwa (Kenya walitumia njia hii kupinga hotuba ya rais Uhuru).
Njia nyingine ambayo imetumika katika mataifa ya Somalia, Ukraine, Urusi, Brazil, n.k na kuzaa matunda kwa kiwango kikubwa ni kutembeza mkono/kichapo bungeni. Weka briefcase pembeni vueni na tai zenu tembeza ngumi za haja.
Siasa inabadilika nanyi mbadilike, vinginevyo nyote mtafungiwa kuhudhuria vikao vya bunge. Ama mtafika mahala mjengewe uwoga wa kuihoji na kuikosoa serikali.