George Kahangwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2007
- 547
- 148
Ndugu wanaJF na watanzania wote!
Wengi wetu tunapenda kufuatilia habari za kisiasa katika nchi yetu kwa sababu mbalimbali; kuu kati ya hizo ni kwa kuwa siasa zinagusa maisha yetu ya kila siku na zina athari katika mustakabari wa kiuchumi wa Taifa.
Kama vile tunavyotamani kuona nchi yetu ikipata maendeleo makubwa, ndivyo tunavyopenda kuona siasa zetu nazo zikipiga hatua kwenda mbele.
Binafsi nasikitika kuona kwamba, tunachokipata badala yake ni kuzidi kuporomoka kwa viwango vya siasa hizo, kama inavyodhihirishwa na mambo ambayo wanasiasa wetu wanayaongelea siku hizi.
Matharani, hivi karibuni zimezuka siasa za; fulani atakufa hivi karibuni, chama fulani kitakufa si muda mrefu maana kimelaaniwa; na wanyama fulani wa mwanasiasa fulani wataangamia wote.
Ndugu zangu watanzania, kweli tumekosa mambo ya maana ya kuzungumzia katika siasa zetu hata tukashuka katika kiwango cha chini namna hii?
Mbona tunayo matatizo mengi ya kiutamaduni, kijamii, kiuchumi na hata kisiasa yaliyo ya muhimu kujadiliwa?
Wanasiasa tafadhali, jirekebisheni. Huko mlikofika sasa ni pa chini muno! Siasa za kutabiliana na au kuombeana vifo ni siasa za washirikina.