Siasa za CCM na Uongo Kila Kukicha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za CCM na Uongo Kila Kukicha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hossam, Mar 15, 2012.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Ndugu wana Jamvi,

  Nimekuwa kimya kwa muda mrefu humu kwa sababu ya mwendo kasi wa maisha ulioongezeka ghafla.

  Napenda kutoa mtazamo wangu juu ya suala la Mkapa kuingilia mambo yasiyomhusu.

  Rais mstaafu Mkapa anaheshimika kwa jambo moja tu la kuwatia adabu viongozi wa serikali katika kipindi chake cha miaka 10 ila analaumiwa kwa kuuza viwanda na mashirika ya umma ambapo amesababisha vijana kibao kuwa wazururaji bila sababu ya maana.

  Mkapa kwa heshima yake hiyo sasa anaonekana kituko baada ya kujidumbukiza kwenye mjadala wa kifamilia usiomhusu. Ndio maana tunasema siasa sio kuropoka na kulisha watu wali na maharage ndugu zangu. Mkapa anapoingilia mpangilio wa familia au ukoo wa Nyerere mbele ya umma unadhihirisha jinsi gani CCM imeishiwa hoja na kubaki kutapatapa kwa maneno yasiyo na maana. Hivi Mkapa anataka kusema yeye ni much know kiasi cha kujua ukoo wote wa Nyerere? Ama yeye Mkapa ndio mtu rasmi ambaye Nyerere alimueleza na kumtambulisha ukoo wake wote enzi za uhai wake? Ni nani basi ambaye hakufanya kazi na Mwalimu? Je hao wote waliofanya nae kazi walihitaji kuujua ukoo wa Nyerere wote ili kulinda ubaba wake wa Taifa? Je Mkapa hakuwa na kazi zaidi ya kutafuta na kuujua ukoo wa Nyerere? Sasa kama yeye anadai Vicent sio ukoo wa Nyerere basi aseme Vicent ni mtoto wa nani!! Au yeye Mkapa aseme Vicent kaanza kumtambua lini. Ufahamu wa Mkapa na busara zake zilishakwisha tangu alipostaafu urais Tanzania, ona jinsi alivyosema 'baadhi ya wapinzani hawana adabu' hii kweli ni kauli ya rais mstaafu? Na ikitokea siku wapinzani wakaidaka dola Mkapa atabatilisha kauli yake?

  Mbona demokrasia Tanzania inasuasua? Hivi Kikwete hakuambiwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010 'hana adabu' na jamaa aliyesema hivyo kuishia kupewa kesi ya kumdhalilisha rais? Basi niseme tu kwamba viongozi wako juu ya sheria maana hata wakiongea uharo na madudu na matusi hakuna wa kuwakemea. Ndio. Ni huyuhuyu alisema pia wapinzani ni kokoto, ni huyuhuyu alisema wapinzani ni wapuuzi. Basi mpuuzi ni yeye alijiuzia Kiwira hali akiwa Ikulu, alipe pango kwa kuwa alifanya business akiwa Ikulu, mpuuzi mwenyewe!!!

  Haya hata huko Arumeru ni vituko tu, tunatambua kwamba Lowassa anashutumiwa kwamba ni fisadi papa, yeye japo anasema hajui ufisadi wake uko wapi, lakini Tanzania inaelewa hivyo, sasa Fisadi huyu kaunganisha nguvu ya Mkapa na wabunge kama akina Sendeka wanafki wakubwa wanaopiga vita ufisadi wasioujua. Kama Mkapa kaungana na familia ya akina Lowassa kwa maana ya Siyoi na Pamela huku Pamela akiwa mtoto wa Kikwete wa harusi sasa kuna nini hapa?

  Hawa CCM wapuuzi sana aisee, wanapenda sana kutufanya sisi mazuzu huku wakijua hatuwezi kuwafanya kitu. Yaani upuuzi wa CCM umefikiwa kiwango cha ajabu na unafanana na Profesa mmoja mjinga kabisa wa chuo kikuu aliyewatungia mtihani wanafunzi wake na kisha akawaambia 'njooni sasa tufanye mtihani huu na atakayenizidi nitamzawadia' hivi uliona wapi mwalimu akafanya mtihani alioutunga mwenyewe? Fisadi limezaa fisadi, toto la fisadi nalo ni fisadi pia, na rafiki wa fisadi ni fisadi mara mbili, huo ndio ukweli. OOh tunavuana Magamba tunavuana Magamba, sasa mmewavua wangapi?, upuuzi tu.

  Hata watu wakipiga vipi makele CCM wameamua kuwa maviziwi walafi na wasiosikia la mtu, Kubenea alisema Siyoi aligawa rushwa waziwazi na hajachukuliwa hatua yeyote? Tuamini kwamba Mkapa alimtuma Siyoi kwa maelekezo ya Lowassa na Kikwete? Hapa kuna jambo ndugu zangu. Kila siku Lowassa anasema yeye na Kikwete hawakukutana barabarani, someni kwa maarifa kauli hii mtagundua kwamba Lowassa ni rais wa 2015 iwe isiwe. Kama asipoingia Magogoni basi Kikwete hatakuwa na changuo lolote zaidi ya kuihama Tanzania itakayoingia kwenye civil unrest isiyo na mwisho. Sihitaji mjadala katika hili kwa kuwa hakuna mwenye point za maana za kunishawishi vinginevyo. Ni juzi tu mgomo wa madaktari tulikuwa tunawalaani serikali kwa kusababisha mgomo huo lakini baada ya Kikwete kuwahutubia wenye upeo finyu tunaanza kuwalaani madaktari kwamba hawakutumia busara, yaani katika sakata la mgomo huo serikali haina hatia, sasa magazeti na redio zimejadili weeeee lakini ukweli ama uongo aliousema Kikwete hakuna aliyetia neno, hata wale akina haki za binaadamu wamefyanta mkia kama mbwa koko akiona chatu. Mipango za CCM na serikali yake ni migumu sana aisee. Madaktari hoi, na sijui sasa watakuja na lipi tena.... Usilolijua litakusumbua.

  Ufamilia sasa unapamba moto, mara huyu mtoto wa fulani mara yule baba yake fulani, ilimradi familia sasa ndio inaongoza nchu huku na sisi akina Pangu Pakavu tunakenua meno tu bila kufikiri, tunaliwa lakini tunakenua tu, Watanzania ni viumbe wa ajabu kabisa. Naamini Watanzania wa sasa ni wajinga kuliko wale enzi za Mwalimu mwaka 1961. Hawa wa Nyerere walikuwa wana akili kuliko sisi Bongo Fleva.

  Nimalizie kwa kumjulisha Mkapa kwamba mambo ya familia ya Nyerere awaachie akina Nyerere wenyewe ambao yeye Mkapa na wenzie waliamua kuwatenga kijiweni baada ya Mwalimu kufariki. Ipo siku na sisi tutatangaza kwamba hao watoto wa Mkapa anaodai ni wake sio wake na tutamtaka akapime DNA ili aaibike vizuri, katika hilo tutamtaka apande jukwaani kutangaza kwamba kalea watoto wasio kuwa wake.

  Ni mimi
  Pangu Pakavu
  Nawasalimia.
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  huu ni unafiki mbaya sana yaani kuulizia uhusiano ndani ya familia nyerere kwenye mkutano wa hadhara wakati watoto wa nyerere anawajua na mkewe bado yupo angeweza kumuuliza tu.
   
Loading...