Siasa za CCM na elimu

mwl. mziray

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
597
397
Hivi karibuni tulisikia baadhi ya wanachama wa CCM waliotangaza nia ya kuwania nafasi ya kuipeperusha bendera ya chama hicho ktk uchaguzi mkuu wakitilia mkazo zaidi katika suala la "elimu"

Nilipata wakati mgumu na kujiuliza maswali mengi kama ni elimu ipi wanayoizungumzia haswa hali iliyonifanya kuzikumbuka shule zinazojulikana kama "shule za jumuiya ya wazazi"

Kwa hakika shule za jumuiya ya wazazi zimedumu kwa muda mrefu na zilijengwa kwa nguvu za wananchi katika kipindi cha mfumo wa chama kimoja na baada ya mfumo wa vyama vingi bado ziliendelea kushikiliwa na CCM japo si kweli kwamba wananchi wote waliochangia kuzijenga bado wapo CCM tu.

Kwenye miaka ya 2000s kulikuwa na uvumi mkubwa sana kuhusu shule hizo kutaka kuuzwa kwa serikali japo sikufahamu juhudi hizo ziligonga vipi mwamba.

Kilichofanya niandike uzi huu ni jinsi CCM kupitia jumuiya kubwa ndani yake ijulikanayo kama "jumuiya ya wazazi" ilivyoshindwa kuziongoza shule hizo na kupelekea kuwa na hali mbaya sana katika ngazi ya utawala, taaluma na miundombinu mbalimbali.

Mpaka sasa shule nyingi zina hali mbaya sana na nyingize zinaelekea kufa kutokana na madeni sugu yaliyosababishwa na uzembe uliopindukia katika ngazi ya utawala, uchotwaji fedha usio halali na mambo mbalimbali.

Kwasasa baadhi ya shule zinashindwa kulipa mishahara ya watumishi kwa wakati muafaka hali inayodhoofisha utendaji kazi katika taasisi hizo.

Pia Walimu wanaoajiriwa katika shule hizi sio Waalimu kutokana na taaluma zao na hufanya kazi kama vibarua kutokana na kutokuwa na mikataba ya kazi. shule nyingi zimeshuhudiwa zikiajiri vijana waliohitimu kidato cha sita maarufu kama "form six leaver" wakiwa na upungufu wa "teaching methodology" hivyo kuzidi kuzamisha jahazi la taaluma.

Ufaulu katika baadhi ya shule hizo pia ni hafifu sana kulinganisha na shule binafsi au shule za serikali halikuwa gharama ya ada katika shule hizi ni kuanzia milioni moja "1,000,000/=" kwa wanafunzi wa bweni pia huduma zitolewazo ni hafifu kupindukia.

Utaratibu wa kuajiri pia haupo wazi kwani baadhi ya watumishi ni ndugu wa viongozi katika ngazi ya utawala hivyo kutoangalia ubora bali kujuana. Hali hii imechangia kuporomosha ufaulu katika shule hizo.

Upo uozo mwingi kana kwamba nashindwa kuelezea yote katika uzi huu.

SWALI LANGU NI JE, KAMA CCM IMESHINDWA KUWA KIOO KATIKA SHULE HIZI ZA JUMUIYA YA WAZAZI WALIZOZISHIKILIA KWA MIAKA KADHAA NA KUZIGEUZA KUWA VITEGAUCHUMI VYAO HALI ZINAKUFA, TUTAAMINIJE NIA YAO JUU YA KUIENDELEZA ELIMU?

JE, IMANI YA WANANCHI JUU YA JUMUIYA YA WAZAZI INATOKA WAPI HALIKUWA IMELALA FO FO FO FOOOOO?

HAO UVCCM WANAJIFUNZANINI KUTOKA KTK JUMUIYA YA WAZAZI?

Ifikie mahali tuache siasa tufanye kazi.

Naomba kuwasilisha.
 
mziray polesana rais wako yupo ulaya anakula shushu ebu fikiria maisha bora yako wapi?ARIMPYA KASI MPYA NGUVU MPYA IKO WAPI?
 
mziray polesana rais wako yupo ulaya anakula shushu ebu fikiria maisha bora yako wapi?ARIMPYA KASI MPYA NGUVU MPYA IKO WAPI?

Maisha bora yapo kwa watawala maana sisi tukisota masaa matatu kwenye foleni za dar wao wanapita na ving'ora.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom