Siasa ya mikopo wa vyuo vikuu inavyowatesa wanafunzi wa law school of tanzania

Aug 18, 2012
17
2
Tangu kuanzishwa kwa LAW SCHOOL OF TANZANIA mwaka 2008 kulikuwepo na utaratibu wa kutoa mkopo kwa wanafunzi wote wanaodahiliwa kusoma LAW SCHOOL OF TANZANIA, pesa hiyo imekua ikitoka Wizara ya Katiba na Sheria. Lakini ilipofika mwaka jana sheria ya bodi ya Mkopo ilibadilishwa na kuingizwa kipengele kinachoruhusu bodi kutoa mkopo kwa wanafunzi wa LAW SCHOOL OF TANZANIA. Kwa sababu bodi wanajua siasa ya mkopo huo wakaweka vigezo vya kisiasa kwa ajili ya wanafunnzi wa LAW SCHOOL KUPATA MKOPO.
Vigezo vilivyowekwa na bodi havina mashiko na si haki kwa watoto wa masikini wanaosoma kwa ajili ya kupata vigezo vya kitaaluma waweze kujiajili na kuajiliwa. Vigezo hivyo ni kama ifuatavyo:-

1: Mtu awe alikua mnufaika wa Mkopo
Kama wengi tunavyofahamu sheria ni moja ya taaluma ambayo sio kipaumbele kwenye ugawaji wa mkopo wanafunzi wanapokua chuo kikuu. Hivyo kigezo hiki hakiwezi kufikiwa na wanafunzi wengi wanaokuja kusoma law school, kwa sababu wote ni wale waliokua kwenye taaluma isiyo kipaumbele. Bodi kuweka kigezo hiki ni kuwakatisha tamaa wanafunzi waliokua wanataka kujiunga na hiki chuo, na pia ni kuonyesha kuwa wanaweka vigezo ili watu wakose mkopo na sio kuweka vigezo ili watu wapate mkopo na kuwezesha watu wanaotoka familia masikini.

2: Mtu awe ameanza kulejesha mkopo
Kwa taaluma ya sheria ili mtu aweze kupata ajira au kujiajiri mwenyewe kigezo kikubwa ni lazimma awe amepita law school, na pia mtu hawezi kurejesha mkopo kama hajaajiliwa na kupata pesa ya kurejesha bodi hivyo hiki kigezo hakikuzingatia msingi wa taaluma na vigezo vya kitaaluma vya kuweza kuajiriwa.

3: Mtu asiwe amemaliza miaka minne ilopita,
Kwa uwezo wa Law school haiwezi kuchukua watu wanaohitimu Bachelor of Laws kwa mara moja na kwa vipindi vya kufuatana mpaka wakamalizika, ndio maana kukawa na intakes, kitendo cha board kuweka hiki kigezo cha kuhitimu hakikuangalia kwa mwaka LAW SCHOOL inachukua watu wangapi na wahitimu wa sheria ngazi ya degree ni wangapi na wanaweza kudahiliwa na law school kwa awamu ngapi muda huo wakijumuisha na wanaohitimu mwaka unaofuata sio kukurupuka kisiasa.


Hivyo kitendo cha Board ya mkopo kuweka vigezo ambavyo ni vigumu kufikishwa na watu wanaohitaji kuomba mkopo inaonyesha bodi wenyewe hawajui lengo lao, na pia inaonyesha bodi haipo kusaidia watanzania Masikini bali ipo kukidhi matakwa ya Wanasiasa na watu fulani walioko kwenye mfumo wa serikali ambao walikua wananufaika na pesa iliyokua inatolewa na WIZARA YA KATIBA NA SHERIA.
Kwa sababu kumekuwa na matamko mbalimbali ya viongozi wakubwa wa Serikali kuwa watu wote walioomba mkopo wamepata mkopo, huku wanafunzi wa LAW SCHOOL hawajui hatma yao inaonyesha hii imekua siasa na Viongozi kutafuta sifa huku hakuna ukweli kwa kile wanachotamka ni Rai yangu kwa Raisi na Viongozi wengine hasa katika Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Elimu, Bodi ya Mkopo na Law School kulishughulikia suala hili mapema hili kuhakikisha wanafunzi wanaishi vizuri ili kujifunza na sio wanaishi shule ili wafeli.
 
Sioni cha kulalamika, Law School sio elimu ya msingi, sidhani kama Serikali inapaswa kuigharamia Hata kidogo... Mngejitegemea tu na hiyo fedha ikafanya mambo mengine. Watoto wa masikini unaowasema wako VETA na vyuo vingine vya ufundi, hawako kwenye masomo ya nyongeza kama Law School au CPA
 
Nadhini mtoa hoja ameeleza vizuri sana. Sio kweli kuwa walosoma law wanatoka familia zinazojiweza. Ni muhimu tukumbuke kuwa ili utambulike kuwa wewe ni mwansheria ni lazima upite law school. Kwa hiyo hiyo ni elimu ya.msingi sana na bila hivyo hakuna mahali mtu ataajiriwa au kujiajiri kama mwanasheria bila kupitia law school. CPA ni tofauti kidogo na hii kwakuwa kuna uwezekana wa mtu kupiga kazi sehemu nyingi bila hiyo CPA ila hakuna uwezekano wa kufanya kazi bila kupita law school.
Mkuu hii serikali haipo makini na.swala zima la elimu. Masharti yalowekwa kwakweli hayatekelezeki.
 
Back
Top Bottom