''Siasa si Hasa''

''Siasa si Hasa''

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
3,216
Reaction score
994
Nimekumbuka msemo huu wa siasa si hasa. Maana yake tuliambiwa katika siasa unapomsikia mwanasiasa akisema jambo siyo lazima awe na maana hiyo...ndiyo maana ya si hasa. Wengi wetu wakatafsiri kuwa kama siyo hasa basi siasa ni uongo. Hata hao sipingani nao, ni kweli siasa ina uongo mwingi. Aliyeko madarakani atajitahidi kuwapa maneno matamu hata kama ni uongo ili kuwaaminisha anawapatia kilicho bora. Kwa upande mwingine mpinzani wake atatafuta neno la kumpinga aliyepo madarakani hata kama ni kwa kumsingizia uongo ili mmwamini yeye.

Niseme kwanini nimekumbuka siasa si hasa: Watanzania tukumbuke Mwalimu Nyerere alitutawala chini ya mfumo wa chama kimoja na tukamwambia aache udikteta atupatie nafasi ya vyama vingi, yeye akang'atuka na tukaaanza vyama vingi. Mwinyi akatupatia 'ruksa' katika siasa na biashara tukamuona hana maana na kweli hakuwa na maana. Uchumi ukadorora. Mwalimu kwa kuliona hilo akatuamsha na kutuambia tumchague Mkapa. Mbabe huyu Mkapa akatuongoza kwa ubabe na aliyesema akaambiwa maneno makali ya kukaripia tukaogopa. Hata hivyo, si Nyerere wala Mkapa angependa tuongozwe na Kikwete. Walijitahidi sana kutuambia kwa ishara na maneno yao lakini sisi tulimtaka Kikwete na Mkapa akatuachia huyu jamaa. Matokeo yake tukamuita 'dhaifu' anaacha nchi iende bila kuongozwa. Mtawala gani dhaifu huyu?....Maneno haya hata upinzani ukayasema maana ulipewa ruhusa hata ya kumtia vidole machoni naye hakusema kitu. Watanzania sasa tukaamua kusema tena kumbe Nyerere japo wengine walimuita dikteta kumbe sisi tunahitaji dikteta wa kweli si wa kusemwa. Hata upinzani wakasema sana tupate sasa dikteta aitawale (achilia mbali kuongoza) nchi hii ya Tanzania.

Hapa sasa kuna shida. Kumbe kuna dikteta mzuri na dikteta mbaya. Kwa wanachama wa chama tawala (kule kwetu tunawaita chama twawala) wakadai dikteta anayefaa ni Magufuli, anafaa sana. Tumeona kazi zake katika ujenzi, akisema bomoa ni kubomoa tu.
Lakini hawa upinzani (walijiita ukawa) wao wakadai dikteta anayefaa ni Lowassa, naye tuliona kazi zake, alimudu hata kutimua watumishi wa serikalini bila kufuata utaratibu.

Sasa hawa maditeta sisi tukawakubali na tukawapa kura milioni nane kwa milioni sita. Kiukweli walichuana sana. Haswa tuliwakubali hawa madikteta.

Hatimaye ameshinda mmoja sasa tumepata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaitwa Rais John Pombe Joseph Magufuli. Huyu sasa ni rais tena anaongoza na kutawala. Hata siku 100 hazijaisha tukamsifia sana anatumbua majipu balaa tena anafungua mahakama ya mafisadi. Tulimsubiri sasa tumempata. Hata Sefue akamshangilia...''tumbua babaaaa'' naye akatumbuliwa. Hata uwanjani akatuuliza...alitaka kujirizisha kama tunaikubali kazi yake ya kutumbua...Nitumbue nisitumbue?.. tukajibu Tumbua. Ama kweli ametumbua hadi sasa anatumbua kumbe majipu yasiyoiva tena yanauma hata hatumshangilii tena.

Ghafla, upinzani umepata neno. Siyo Dikteta tuliyemtaka huyu, kumbe ndiyo walitaka dikteta mzuri siyo mbaya kama huyu. Tufanyeje sasa?

Wakagomea spika mdogo lakini mbabe wakaambiwa nendeni. Wakatoka wamefunga midomo. Wakagawanyiaka. Wakaacha ukawa wakaanza ukuta. Huyu tuliyemtaka hataki mizaha na usaha. Anatumbua tu. Wakajaribu, wakafungwa. Wakakataa kula wengine wakaanguka, huyu jamaa hasikii. Wakaitwa kwa ' herode na pilato' wakaonywa. Wakaamua isiwe taabu tumeahirisha. Wanasema wamsome kwanza huyu jamaa haeleweki.

Sasa mimi sijaelewa: Tumempata rais JPM tunampenda. Kwa staili yake ya kuongoza, we acha tu..hasa kutumbua majipu. Lakini mwaka haujaisha tumemkosoa.

Anaonea mafisadi?....mbona tulisema awashughulikie?
Anaonea watumishi hata mishahara haipandi?....mbona mlikuwa hewa?

Basi acha turudi kwenye siasa....aahhhh hapo sasa yeye hataki. Subirini jipu likikamuliwa hadi kiini kitoke ndiyo mtapona. 'Siasa acheni hizo siyo hasa' mtaanza 2019 serikali za mitaa, tulieni.
Hatuna pa kutokea. Biashara zimedoda....tulizoea kukwepa kodi sasa tumekabwa hadi EFD..... kulipa tumeumia eti hatumtaki kwa lipi sasa?. Tulipe kodi ajenge hospitali, alipe mishahara watumishi na hata watoto wasome bure.

Kumbe siasa si hasa. Tukiambiwa kuacha siasa tumegoma. Hata watumishi kumbe nao wanapenda siasa. Msikilize huyu; ...sijamuelewa kabisa, mishahara hapandishi na dili ofisini hatupigi....hawa ukuta nao waoga si waandamane?...Nanai aandamane? Wewe huwezi kuandamana? Kila siku mara uandike facebook na mitandao yote ukiulizwa wewe nani unadai ''anonymous''...sema jina tukujue? Kimya.

Huyu naye mfanyabiashara, alidai CCM ni ileile. Pesa akaikopesha na yeye akajitosa kugombea mara udiwani hadi ubunge...kisa CCM ikirudi mwaka huu tutapiga pesa hata ya gesi inakaribia kutoka. Hamadi!!.... Jamaa huyu kakaba kila kona. Alipoingia bungeni eti anawatishia wakurugenzi wampe milioni 30 ama awasemee watumbuliwe...maweeee!!???...pesa hawatoi. Na gari kukopeshwa mwisho milioni 90...Mungu wangu, pesa yote aliyohonga wapiga kura haitarudi. ''Imekula kwake''..hataki tena ubunge. Tumemwambia subiri ukamuliwe hadi 2020 na wewe ndiyo mbunge wetu na usipotuletea hongo 2020 hatukupi.

Sasa bora siasa....japo si hasa. Dikteta kweli tulimtaka ila angekuja dikteta mzuri. Na huyu naye!? mbona sasa haeleweki?...

Anayo miaka yake 4. Tumpe muda. Wengine watalimia meno...
Bado nina imani naye....nchi hii ilikuwa imeoza acha irudi katika mstali. Hata kama hatutafikia malengo lakini tutapiga hatua. Mkapa alitupeleka hatua mbili mbela bahati mbaya Kikwete akaturudisha hatua tatu nyuma. Sasa hyu anataka tupige hatua sita mbele....lazima turuke siyo kutembea wenzetu wanatuacha. Kuruka kunahitaji uwezo, tusichoke twende naye.

Nilitaka kusahau huyu kiongozi wa 'kiroho' yeye ni mwema tu hata akimshangilia dikteta wa kwanza baadaye akahamia kwa dikteta wa pili ni sawa tu. Mbona yeye ni wa 'kiroho ' hamruhusiwi kumsema. Naye alitegesha apate mlo wake kwa dikteta wa kwanza ama wa pili. Bahati mbaya wote sasa hawamjali...aliyepata na aliyekosa...naye wa kiroho kakosa mwelekeo. Akitumbua anasifia......ukuta ukijengwa anasifia...hata hajitambui. Na wale wafuasi sasa hawajitokezi kusema amebarikiwa kajenga ghorofa na gari mbili sasa anampa wa kiroho naye gari....hawaji wamekabwa! Sadaka hazitoshi. Hata mafuta ya kuweka katika helikopta (chopa) hana si itajengwa buibui?

Nimalizie na huyu msanii....yeye alipigania sana dikteta wa pili. Bora yule wa kwanza dikteta wake alipata. Wote wanaonja joto ya jiwe....nyani kula mahindi mabichi....hahaaaaaa. Kumbe maji tuliambiwa yanafanya mtu awe mweupe siyo ni pesa. Pesa imeota mbawa. Msanii kachanganyikiwa....ilikuwa milioni 10 kumpandisha jukwaa. Sasa ukimuita hata kwa laki 5 anakubali.

Msinipige mawe,,,,,,,labda tusubiri aingie Donald Trump tuyaone maajabu mengine zaidi kudhihirisha 'siasa si hasa'
 
Mwandishi sijamgusa.....nimewaachia ninyi. Si mnawajua? Wengine wao wamekula shavu...wengine hasira zao katika kalamu...ukikosea (wao wanaita kukosoa)...umekula za uso. nini? gazeti limefungiwa!!!///
 
Naapa uzi huu ndio utaongoza kwa matusi kuliko nyuzi zote jf...Time will tell
 
Back
Top Bottom