fj_dom
Member
- Jan 29, 2017
- 22
- 13
Nchi hii kwa hakika kila tunaposonga ndipo mambo yanavyozidi kushangaza mpaka wakati mwingine najiuliza hivi kweli tuna nia njema na elimu yetu au ni maneno tu kila mara.
Matokeo ya kidato cha nne yametoka na naamini wengi wetu tunaopenda kufuatilia mambo tumeshayajua. Sasa cha kushangaza ni pale shule zinapofanya vibaya wanasiasa wanapojitokeza na kuchukua maamuzi ambayo dhahiri yana mlengo wa kisiasa ili waonekana mbele ya mamlaka za uteuzi na si ambao wanafanya mambo kwa utashi uliotukuka.
Katika shule kumi zilizofanya vibaya, sita(6) kati ya hizo zimetoka Dar es Salaam. Cha kushangaza nimeona wakuu wa shule hizo wameshatumbuliwa kama gazeti moja la leo lilivyonukuu. Sasa hivi unamtumbua mwalimu mkuu kwa misingi ipi hasa.
Shule hizo zote ni za serikali na za kata. Hivi kweli shule ya kata unaweza kuifananisha na Feza, Marian, St. Francis au Kaizerege kwa kutaja chace, nimetaja hizo shule maana ndizo zilizofanya vizuri kitaifa mwaka huu na pia kwa miaka kadhaa sasa zinaendelea kufanya vizuri.
Shule hizo kwanza kabisa, idadi ya wanafunzi wanaokuwa darasani ni ndogo, pili wana maabara zinazoeleweka, tatu wanafunzi hawapati adha ya usafiri hivyo kupata mda mzuri wa kumpumzisha akili, nne wana walimu wenye ari ya kufundisha kwa kupatiwa mishahara isiyoleta msongo wa mawazo, tano wana walimu wa kutosha kwa kila somo hivyo kuwapa mda wa kutosha walimu kuandaa vipindi vyao vizuri na hivyo kusaidia kuwaimpart elimu inayostahili kwa wanafunzi husika.
Sasa hawa ndugu zetu wa kutumbua, hivi unaendaje kumtumbua mwalimu mkuu wa shule za kata ambaye wanafunzi tu katika kila darasa wako kuanzia 70 na kuendelea, walimu hamna, usafiri huwa ni kero kwa wanafunzi hivyo kufika nyumbani wakiwa wamechoka au wengine kama ni wa kike inabidi warubuniwa na wapenda dogo dogo ili japo adha hiyo iwatoke na kusababisha kupoteza mwelekeo katika masomo yao.
Ifike mahali tuache siasa tu katika mambo ya msingi. Kama nia ipo ya kweli kuboresha elimu zetu, kwanza kabisa, mishahara ya walimu iboreshwe na pia stahiki zao za nyuma walipwe ili japo kuwapa ari hao walimu katika fani yao. Na pia usafiri katika shule za kutwa ziboreshwe, badala ya matumizi kama ya kununua magari ya washawasha mengi kipindi karibia na uchaguzi ni bora zinunuliwe school buses na huo mradi uendeshwe na halmashauri husika.
Vile vile, vitabu vya taaluma visambazwe vya kutosha badala ya kusema elimu bure alafu inakuwa majanga maana vitabu hamna sasa wanafunzi watasomaje au kujiendelezaje katika somo husika. Hii tumbua tumbua ili kutisha watu sidhani kama ni njia sahihi. Njia sahihi ni kuandaa bajeti yenye uhalisia pamoja na kuisamamia utekelezaji wake kwa 100%.
Natumai itafika mda nchi hii, tukaacha siasa katika mambo ya msingi.