Siasa na rasilimali zetu.

Siasa na rasilimali zetu.

cedrickngowi

Senior Member
Joined
Jun 9, 2012
Posts
148
Reaction score
23
Habari wakuu!
Najaribu kutafakari sana jinsi rasilimali zote za nchi hii zinavyobinafsishwa kwa wageni.Madini,misitu,mapori ya kuwindia,Mahoteli nk.Najiuliza swali moja la msingi na ambalo nashangaa kama wanasiasa wetu wanafikiria juu ya hili au?
Ni kwanini tunashindwa KU-NATIONALISE rasilimali zetu?Nadhani hii ingekuwa njia nzuri zaidi na ya uhakika ya kujipatia maendeleo kwa manufaa ya watanzania wote kuliko UBINAFSISHAJI tunaofanya kwa WAGENI.Itambulike kuwa Tanzania haiwezi kujengwa na watu kutoka nje,lazima ijengwe na SISI wenyewe.Tunapotumia wawekezaji WAZAWA maana yake ni kwamba hata faida inayopatikana wange RE-INVEST hapahapa badala ya kupeleka nje kama wanavyofanya wageni tunaowabembeleza kuja.Nasikitika sana kusikia rais wetu anatumia muda mwingi kuzunguka nje ya nchi KUBEMBELEZA watu waje kuwekeza then wanakuja tunaambukia kujengewa viwanda vya Cement,chuma,Supermaket na mahotel.Ni kweli hakuna watanzania wenye uwezo wa kufanya haya?Nadhani tunahitaji kuanza upya na kujiuliza ni maeneo gani hasa tungehitaji wawekezaji toka nje (and i mean real INVESTERS) na si kila area kama tunavyofanya sasa.NINACHOKIONA HAPA TUNAUZA NCHI,na tuandae majibu kwa vizazi vijavyo.
 
Umesema sawasawa kabisa, Nyerere alisema kama mtu anakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukalikubali anakudharau. Serikali yetu inashauriwa na hao wanao jiita World Bank (WB), Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) kupitia kwa watawala wetu, Mkapa- Uwazi na Ukweli, JK Maisha bora kwa kila Mtanzania wakauza viwanda vyetu chini ya Comrade Dr.Kigoda na leo ndo analeta tena mkakati wa kufufua viwanda, swali je ataweza?

Kama Watanzania wataendelea kuwapitisha hawa wavua Magamba ujue wataisha kama mshumaa tu.

Mungu aiepushe nchi hii kwa kutumia uweo wake maana hawa sasa wamedhamiria kuifanya nchi hii kuwa ya kifalme, yupo jamaa anazunguka makanisani akigawa mifedha nao wanazipokea tu, sijui kama akipata tutaponaje. Mungu ingilia kati tutaisha wengine hatuna hatia yoyote.
 
Back
Top Bottom