johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 91,116
- 158,380
Ni kawaida panapokuwa na matukio ya kitaifa ya kisiasa viongozi wetu wa dini hukusanyika pamoja na wanasiasa na kufanya dua.
Sasa watanzania wote tunajua kuwa Maji ni uhai na kwamba katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu mvua haijanyesha. Mpaka sasa nilitegemea wale mitume na manabii wa nchi hii walau wangetukusanya pale uwanja wa taifa kwa ajili ya maombi kama wafanyavyo nyakati za mwaka mpya.
Nimpongeze Mufti Abubakar Zuber kwa kuitangaza jumapili hii kuwa ni siku ya kuombea mvua za heri, nami naahidi kuwa pamoja nao katika maombi hayo kiroho.
Mitume na manabii nanyi hamuoni umuhimu wa kutenda kama Mufti na kama mmebanwa na ratiba zenu tujulisheni ili tuangalie namna nzuri ya kushirikiana na Mufti siku ya jumapili.
Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka!