Siasa Matokeo ya Vifo vya Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa Matokeo ya Vifo vya Watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnyamahodzo, Jan 23, 2012.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni wakati mwingine kwa waandishi wa habari za utafiti na watafiti kuchunguza na kupata data za vifo vya watanzania kutokana na uzembe na maamuzi mabovu ya wanasiasa. Sizungumzii waandishi wa habari za kiudaku au fupi fupi, hawa hawataweza kusaidia kivile.

  Mtakumbuka kuwa ni waandishi wa habari wakisaidiana na wanasiasa ndiyo waliowapeleka watu Loliondo,lakini hawakufuatilia baada ya hapo ni watanzania wangapi wamekufa. Makundi yote yalikaa kimya.

  Nasema tena afadhali kwa waandishi wanaweza kuregret kwa hili lakini si wanasiasa waliopo madarakani hata kwa lile shinikizo lao walilolifanya kwa wataalamu ya kuwa wasiseme ukweli juu ya athari ya tiba ya "kikombe cha babu"

  Ulipoanza mgomo wa Interns Muhimbili na Dodoma, waandishi makini waliikosa kuitumia fursa hiyo kuujulisha umma kwa data kamili namna watanzania wadogo kwa wakubwa walivyokufa kutokana na mgomo huo; achilia mbali idadi kubwa ya walioendelea kuugulia maumivu kutokana na maradhi waliyonayo.

  Kesho madaktari wanaanza mgomo. Tunaomba waandishi makini hasa wale wa habarh za uchunguzi, wavamie mahospitalini, kwenye vituo vya afya na zahanati halafu watoke na data ngumu kuujulisha umma. Serikali katika hili haiwezi kusema ukweli, si mnakumbuka mgomo ule wa 2005 uliowahusisha Kigwangala et al wakiwa interns pale Muhimbili na combating technique ya Serikali kupeleka madaktari toka Lugalo na mikoani? Baadaye serikali ilificha idadi kamili ya vifo.

  Nawasilisha!!
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu, tunaomba waandishi mkeshe mahospitalini.
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nimekuelewa mkuu, japo neno kukesha ulilotumia wako watu wataosema unamaanisha washinde huko usiko kucha. No that is the meaning. I agree by saying that investigating Journalist should throw their eyes keenly to hospitals, health centres and disperies so that they may collect all datas related to "mass killing" due the doctors strike caused by unaccountable politicians.
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mpaka mgomo wa awali unakwisha sijaona chombo cha habari kilichomudu kutoa angalau idadi ya watu waliokufa katika Hospitali moja kwa kipindi kile cha mgomo.

  Waandishi, lishughulikieni hili. Wapo wafanyakazi wengi wa sekta ya Afya waliotayari kuwapatia data.

  Kujua idadai kutasaidia kuwaambia viongozi wetu "gharama ya maamuzi yao mabovu ni idadi hiyo ya vifo vya watanzania"
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Anayechochea mgomo huu ni chizi! Hamtspata faida yeyote ya kisiasa kama mnavyodhani!
   
 6. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mtaalam yeyote asiyetathmini madhara ya jambo kama matokeo, hayumkini kuitwa mbumbumbu. Fikiri, hata mcheza mpira hutathmini madhara ya kumtoa mchezaji katika mechi waliyofungwa au kupata ushindi, sembuse kada nyingine?
   
 7. s

  sugi JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  waandishi wetu cjui wanahongwa hawa?yaan wanatoa habari za ajabuajabu tu,habari zinazohusu maslahi ya umma wanabana
   
Loading...