Siasa chafu na mwelekeo wa Taifa letu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa chafu na mwelekeo wa Taifa letu.

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Shayu, Mar 30, 2012.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Ningependa kufanya tafakuri ya Mwelekeo wa Taifa letu na ni nini itakuwa hatma yetu kama tutaendelea na aina ya maisha na siasa tunazo ziendeleza kwa sasa ambazo naona zimeligawa Taifa letu na kulifanya kukosa mwelekeo na dira, kwasababu ya wanasiasa kukosa maono na kusahau misingi itakayojenga Taifa hili na kufuata mwelekeo ambao hauna tija wa ubinafsi. Mantiki ya uongozi imeondoka kabisa ambayo ni kuongoza watu katika njia stahili, kujenga uchumi imara wa nchi na kuwaleta watu wake pamoja ili kulitumikia Taifa lao wenyewe.

  katika Taifa lolote kiongozi ndio kioo katika jamii, taswira ya jamii inategemea sana aina ya viongozi walionao.Ujenzi wa taifa lolote lile unategemea sana busara na hekima za viongozi wao, akili za viongozi ni muhimu sana katika ujenzi wa Taifa imara.


  Kwahiyo usalama na kuendelea kuwepo kwa Taifa hili kunategemea sana hekima za viongozi wetu na wananchi wanaowaongoza. Ni muhimu sana kuwa makini jinsi tunavyoliendesha Taifa hili, mawazo yetu ndio yanayojenga taifa hili , hivyo ni muhimu sana kwetu kuangalia jinsi tunavyofikiri kuhusu Taifa hili na kubadili mwelekeo wa mawazo yetu na jinsi tunavyoendesha siasa zetu kwa faida yetu na vizazi vijavyo.

  Ni lazima tufahamu ya kuwa tuna majukumu ya ujenzi wa Taifa hili kila mtu ana wajibu huo, hatuwezi kulichukia Taifa hili na wakati huo huo tukawa na jukumu la kulijenga. Hatua ya kwanza ya kulijenga Taifa hili ni kulipenda na kufahamu kwamba hapa ndipo nyumbani kwetu na hii ndio ardhi yetu, tuna wajibu wa kuitumikia.


  Siasa ni chombo pekee ambacho kama kingetumika vizuri kingeunganisha Taifa hili na kutuleta katika malengo mamoja ya ujenzi wa Taifa hili, ingetumika ku order jamii zetu, kuweka jamii zetu katika mpangilio mzuri, tunafahamu kwamba bila order hakuna maendeleo yeyote yatakayopatikana, na hakuwezi kuwa na order kama hakuna discipline kutoka katika uongozi wa serikali mpaka familia, hili ni jambo muhimu sana katika ujenzi wa Taifa letu kama tunataka kuendelea bila hilo kamwe hatutaweza.

  Ningependa tuangalie upya jinsi tunavyoendesha siasa zetu na tujiulize kama kweli zina maslahi kwetu kama Taifa? tujiulize kama mwelekeo tunaoenda nao tutafika? Lazima tuangalie upya mahusiano ya vyama vyetu, ili tujenge siasa zitakazokuwa na maslahi kwa Taifa letu, madhumuni ya kuwa na vyama vya siasa ni kujenga Taifa sio kulibomoa na kujenga uadui. Kama siasa imekuwa chanzo cha kugawa watu na vurugu sioni umuhimu wa kuwepo kwake.
  Siasa imeshindwa kutatua matatizo ya wananchi wetu kama ilivyotakiwa na kulingana na maliasili tulizonazo.


  Siasa ina umuhimu mkubwa katika kujenga fikra za watu kama tutaitumia vizuri kwakuwa mabadiliko ya watu huanza katika fikra, jinsi watu wanavyofikiri, huo ndio ukombozi wa kweli, tuna mtazamo mbaya kuhusu uongozi.
  Kuna mapungufu makubwa katika uongozi kwenye Taifa letu, kufikiri ukipata nafasi ya uongozi umepata kutajirika au ni sehemu ya sifa na majivuno ni ujinga.


  Taifa linahitaji mwelekeo, watu wanahitaji kujengwa kiakili na katika maendeleo ya kawaida ya binadamu, lengo la siasa ni kuimarisha maisha ya binadamu sio kuyafanya duni.


  Tunahitaji viongozi watakaofanya kazi kwaajili ya kutumikia wananchi kuleta madadiliko katika Taifa letu, kwanza kumbadilisha mtu mwenyewe na mtazamo wake, lakini pia kumletea maendeleo ya vitu.
  Ni lazima tubadilishe fikra za watu wetu kwanza alafu maendeleo ya vitu, na vitu hivyo vitagawanywa katika sehemu kuu mbili, vitu muhimu kwa maendeleo ya binadamu na vile ambavyo si lazima sana binadamu kuwa navyo.

  Binadamu anahitaji maji salama, makazi, mavazi na chakula ili afya yake iimarike, lakini kuna maendeleo mengine ambayo binadamu anahitaji kuwa nayo ya vitu ambayo lazima yajengwe katika misingi ya maadili ili binadamu asijali vitu zaidi ya utu.


  Lazima tujenge Taifa letu katika misingi ya utu na kujaliana kwakuwa sisi ni Taifa moja.
  Jambo la msingi ni ku order upya Taifa letu, kuangalia upya mfumo wa siasa zetu na misingi ya Taifa letu na familia zetu, kwa kuipa nguvu ustawi wa jamii kwa elimu na maadili , na kuangalia upya elimu yetu ili iwe na tija katika ujenzi wa Taifa letu.


  Taifa kama taifa kamwe halimsomeshi mtu kwa faida yake binafsi bali awe na mchango katika ujenzi wa jamii yake na Taifa lake na ndio maana mataifa yameanzisha shule, ili watu wake waelimike waishi vizuri na wajenge mataifa yao ama sivyo kusingekuwa na manufaa yeyote kwa Taifa kuwa na shule.

  Taifa ni mkusanyiko wa watu wenye malengo mamoja ya kufanya maisha ya binadamu kuwa bora zaidi na jamii haitoweza kufikia malengo hayo pasipo elimu. Kwahiyo watu walioelimika lazima wakusanye nguvu zao na akili zao katika ujenzi wa Taifa hili sio kuliibia.


  Tatizo ninaloliona elimu yetu imekuwa ya kibinafsi mno, mtu anasoma kwa manufaa binafsi ili awe tajiri au aajiliwe lakini sio anasoma ili apate elimu ili isaidie katika ujenzi wa Taifa lake, pasipo umoja wa fikra kamwe Taifa hili hatutalitoa hapa lilipo, lazima tuwe wamoja tulisaidie Taifa hili kwa faida ya wote na vizazi vyetu vijavyo, Hili ndio jukumu lililotufanya hai na lililotuweka katika ardhi hii ya Tanzania ujenzi wa Taifa letu. Vurugu fujo na vituko havitasaidia Taifa letu kukua wala matusi ya baadhi ya watu humu jamii forum wanaotukana na kudhalilisha wengine, tuitumie vizuri jamii forum kwa kuleta mawazo mazuri yatakayojenga Taifa letu.


  Lazima tuwafundishe watoto wetu umuhimu wa Taifa hili kwao ndani ya familia zetu, lazima tuwakuze katika misingi ya kitanzania na katika roho ya uzalendo wa Taifa letu. Naiangalia hali ilivyo katika Taifa letu kwa sasa kama baba aliyefariki na kuwaacha watoto wakigombania urithi ndivyo tulivyo kwa sasa.


  Hakuna order katika serikali, katika vyama na katika jamii, Taifa hili linahitaji mwelekeo na linahitaji mwelekeo sasa kabla hali yake haijawa mbaya, tunahitaji kujenga umoja wa Taifa letu na kuimarisha uchumi wetu. Taifa hili hakuna lilichokosa kulifanya Taifa kubwa.


  Kama tutatengeneza order kwa viongozi kujiheshimu na kutii utawala wa sheria na kila mwananchi kutimiza wajibu wake na kuwa mzalendo na Kama tukiamua tutaweza. Ni jitihada zetu na maarifa yetu yatakayo tufikisha tunapotaka kwenda. Najua kila mmoja wetu anataka kuona Taifa hili likiwa bora, anataka kuona Taifa hili likiwa na heshima.


  Ni lazima tubadili mawazo yetu sasa, ili Taifa letu lipige hatua. Hatutaweza kuwa na maendeleo yeyote bila kujenga mahusiano yetu kwanza kama watu tunaoishi katika Taifa moja, kama hatutajenga upya vyama vyetu vya kisiasa katika misingi ya maadili na kuacha fikra kwamba ukiwa kiongozi umepewa nafasi ya kujitengenezea utajiri na sifa au ukubwa na kutawala wengine bali ni njia ya kuwakusanya watu pamoja katika jukumu la kujenga Taifa letu na kujiletea maendeleo tutafika. Tujenge misingi ya vyama vingi sio katika uadui bali katika ushindani wa sera na undugu, tusifanye siasa chanzo cha mapato ndio mwanzo wa uadui vurugu na fujo iko hapo, tunaweza kugombania madaraka katika misingi ya sheria na kuheshimiana kwa kushindana katika sera na kuwaletea wananchi maendeleo, Taifa hili linahitaji kutoka hapa lilipo.


  Maendeleo yetu yatakuja kwa nguvu ya pamoja pasipo kundi moja kujiona bora zaidi ya kundi jingine.
  Tukiendelea kama tunavyoendelea kufanya siasa ni mtaji wa ujasiliamali tutakuwa tunakata mti tuliokalia kamwe hatutafika, uchu na uroho wa madaraka na mali utatufanya tupigane vita, ni dhahiri tunaona mwelekeo wa siasa zetu kwa sasa na machungu yanayotokana na siasa hizo za uchu wa madaraka, siasa zisizokuwa na staha na heshima, hatuwezi kuendelea namna hiyo, hatuwezi kujenga Taifa letu kwa staili hiyo na wala tusitegemee maendeleo, mjinga atategemea maendeleo katika hali hiyo.


  Faida ya kipindi kifupi tunayoipata kwa siasa chafu na zenye lengo la manufaa ya kibinafsi zitaleta hasara kubwa katika Taifa letu, italigawa taifa letu vipande vipande na maendeleo yetu kama binadamu itakuwa historia.
  Hatuwezi kusema Tanzania haiwezi kuwa kama nchi nyingine zenye vita wakati matendo yetu yanatupelekea huko, ujengaji wa Taifa unahitaji umakini mno na kujitolea kwa viongozi na watu wake.


  Ujenzi wa Taifa lolote lile, muundo wake na mpangilio wake unategemea sana akili na maarifa za viongozi wa Taifa hilo, unapoona ujenzi wa mataifa mengine yamejengwa na busara na hekima za watu wa Taifa hilo, tunafurahia kwenda katika mataifa hayo lakini tujiulize tunafanya nini kujenga nyumba yetu wenyewe? Tunafanya nini ku transform ardhi yetu iwe sehemu nzuri ya kupumzika kwa roho zetu na miili yetu? Kama tutafanya kazi kwa pamoja tutafanikiwa, furaha ya pamoja huletwa na jitihada za pamoja ni lazima tujumuike katika kujenga Taifa letu.  Sisi sote ni watoto wa Taifa hili mababu zetu walipata tabu kwa pamoja ya ukoloni ni lazima tusimame pamoja kujenga Taifa hili , tofali baada ya tofali, ni lazima tujenge misingi imara isiyoyumba ya taifa hili, tunaweza tukiamua.
  Ni lazima tuwe na tumaini hili, ni lazima tuishi katika tumaini hili mpaka maono haya yatimie. Tumaini letu liko wapi watanzania? kunapokuwepo na matumaini kuna uhai na leo hii katika taifa letu hakuna matumaini kila mtu analalamika lakini wakati ni huu sasa wa kusimama na kuamsha tumaini hili, kwamba tunauwezo wa kujenga Taifa letu na pakawa mahali pazuri ba kumpumzikia
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Somo zuri la uraia,tatizo linakuja upande mmoja unapoamua kutumia matatizo ya raia kama mtaji wa siasa!mfano kurejesha shamba kwa wananchi,kutoa tenda ya ujenzi wa daraja mbutu,kugawa pesa,chakula wakati unapofikia uchaguzi tuu!jee kipindi kingine si wanakua wanaiba rasilimali zetu?inakua kampuni ya east africa meat ichote karibu 2bn za kujenga machinjio dar halafu ifilisike na hakuna aliyenyongwa hadharani pale jangwani au mnazi mmoja?
   
 3. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Hayo yote tutashinda kama vyama vya siasa havitatumia huo kama mtaji wa kuingia ikulu, kwakuwa na vyenyewe vina matatizo ya kimaadili ndani yake, hakuna discipline kwakuwa hata misingi ya kuanzishwa kwake ni kuchukua dola na sio kufanya transformation ya jamii, ndio maana mara nyingi hawaongelei sera wala kujaribu kuelimisha watu ili walipende Taifa lao na kubadilisha fikra zao juu ya Taifa lao, sasa watu wanalichukia Taifa hili hawalijali hata miji yetu hatuijali tunatupa takataka ovyo ili tulibadilishe Taifa hili lazima tubadilishe fikra za watu wetu, tujenge umoja na uzalendo, ufisadi una misingi yake ni lazima tutafute chanzo cha tatizo ili tupate dawa sahihi ya tatizo hilo ama sivyo tunaweza kupambana na ufisadi na usiishe, mimi nafikiri tuangalie upya Tatizo hili vyama vya kisiasa wanalitumia kama mtaji wa kuingia ikulu pasipo kujenga vyama vyao kwanza katika maadili, giza huondolewa na mwanga giza haliwezi kuondolewa na giza. Ni lazima tuangalie upya mfumo wa elimu yetu na makuzi ya watoto wetu tujenge maadili yao. Maoni yangu Taifa letu liko katika confusion kutokana na siasa zetu na sidhani kama chadema pia wanauwezo wa kuondoa tatizo hili pasipo kwanza kujiangali wenyewe maadili yao na maadili ya jamii kwa ujumla, tuna tatizo katika jamii, huu ufisadi hauko katika serikali tu kwahiyo ni lazima tujiangalie kama mtu mmojammoja na kama Taifa, hasa sisi tunaosema tumeelimika lazima tuwe chombo cha kuleta mabadiliko. mabadiliko sio kuondoa serikali moja na kuiweka nyingine, mapinduzi ni kuondoa mfumo mzima ambao haufai na kuweka mfumo mwingine utakaoleta tija na maendeleo katika jamii.
   
 4. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mtoa mada na wachangiaji wote wanazungumzia jambo moja kuu: Tanzania haina dira itakayoliongoza taifa. Katiba iliyopo inajicontradict mno. Kama kweli mwananchi atapewa fursa ya mapendekezo, la utangulizi ni dira ya taifa na msisitizo wa namna ya kuifikia. Kwa kipindi hiki cha mpito tuendelee kufichua yaliyojificha ili kila mtu aelewe kiongozi wake anastahili heshima na sio wa kuogopewa.
   
Loading...