Si kila mwenye wazo mbadala sio mzalendo

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,872
Nimeamini hakika kuwa siasa ni imani na ili uwe muumini wa dini fulani au mwanachama wa chama fulani lazima kwanza muhubiri wa imani hiyo ashughulike kwanza kuharibu sehemu ya akili yako inayoshughulika na reasoning. Akifanikiwa kuua reasoning yako basi utafanya chochote anachokitaka.

Kumekuwepo na hoja ambazo kwasasa zinachukua mrengo wa kisiasa toka mheshimiwa Rais alipopokea taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu. Mjadala umekuwa mkali sana baada ya mbunge wa Singida Mashariki kusema aliyoyasema. Katika speech zake zote mbili ambazo nimezisikia mheshimiwa TL nilimuelewa anamaanisha yafuatayo

SPEECH YA KWANZA (MIGA CONVECTION)
Katika speech hii TL anakubali kabisa kuwa tunaibiwa na kwamba wanatupiga kwelikweli, lakini anasema pamoja na kutuibia bado tunapaswa kudeal nao kwa umakini mkubwa, ukizingatia kwamba wanatuibia kupitia sheria zetu mbovu tulizozitunga miaka 18 zilizopita. Lissu anadai mkataba unawaruhusu hawa watu kupeleka mchanga huko wanakopeleka, sasa kuwazuia tu kienyeji kisiasa inaweza kutuumiza pale tutakapopelekwa mahakamani. Amekuwa na wasiwasi na mfumo uliotumika na sisi huwa tunasema wasiwasi ni akili. Lakini pia tujue tunapambana na watu wa aina gani, kwakweli katika vita hivi tunapambana na watu wazito wenye hila na kila aina ya uwezo na ujuzi. Hata kama uko kwenye haki still wanaweza kukufanya walivyofanya ZIMBAMBWE na kwingineko. Kwahiyo TL anapendekeza namna bora ya kudeal na hawa watu
a) Tujitoe MIGA and other bilateral treaties ili tusiweze kushtakiwa nje hata kama tutafanya haya. Hapa TL anaona ni bora tungejitoa huko kwanza ndiyo tuzuie mchanga ambao kwa sheria ya sasa ni mali yao.
(b) Tupitie mikataba yote ili kuona udhaifu na kuyarekebisha

SPEECH YA BUNGENI (ECONOMIC DIPLOMACY)
Hapa TL alikuwa anaelezea madhara yanayoweza kutokana na hatua zetu hasa kwa wawekezaji wakubwa. Wawekezaji hawawezi kuja kwenye nchi ambayo conflict kati yao na serikali humalizwa kibabe na kisiasa. Ndiyo maana wanapenda uwepo wa arbitrator . Kwahiyo wawekezaji wengine wanaweza kuogopa kuja kulingana na tunavyodeal na hawa ACCACIA. Wengine wnadhani mgogoro huu hausikiki huko kwa wenzetu nje, ukweli ni kwamba mgogoro huu umefanya wawekezaji wengi watake kuijua Tanzania na sera zake za uwekezaji. Wawekezaji hao wako interested na hii scandal vibaya mno kwasababu mapambano yetu na ACCACIA yanawapa platform ya kufanya maamuzi ya ama waje kuwekeza au lah. TL anaposema gharama tutakayolipa itakuwa kubwa hamaanishi eti tutashindwa kesi halafu tulipe hela, GHARAMA hujumuisha mambo mengi pamoja na kulipa kama tutashindwa kesi, kukosa wawekezaji, wawekezaji kutoa pesa zao Tanzania , kuharibu uhusiano na nchi wanakotoka nk.

DHANA YA DIPLOMASIA YA UCHUMI

Tatizo ni kwamba watu wengi hawajui maana ya diplomasia ya kiuchumi na ndiyo maana wengi wanamuona TL kama mwehu asiyekuwa mzalendo. Katika dunia ya sasa bila diplomasia ya uchumi hakuna mtu atakuja kuwekeza kwako. Ndiyo maana ili kulinda investments zao hao wenye pesa wanataka kesi ziwe zinapelekwa kwenye arbitration courts ambako wanategemea kupata haki na siyo serekali ndiyo iwe muhukumu.

HITIMISHO
1. Kwa mtazamo wangu mheshimiwa Rais wetu yuko sawa kabisa, ameonesha nia njema. Hatuwezi kumuhukumu kwamba kwanini afanye sasa wakati alikuwa moja wa waliopitisha hiyo sheria. Tujue alikuwa chini ya wenye nguvu kwahiyo hata kama alifanya kosa wakati huo tusiendelee kumhukumu bali tumpe moyo na kumsaidia
2. Si kila mwenye mawazo mbadala siyo mzalendo, uzalendo si kuunga mkono kila kinachosemwa na kiongozi, wazazi au viongozi wa dini. Ukiwa ni mwandamu mwenye akili timamu kuhoji, kuangalia faida na hasara ya jambo fulani ni jambo jema. Leo TL kuonekana ni mwehu ama kaohongwa si kweli kwasababu hata wakati akipigana dhidi ya hizo sheria pia aliitwa mchochezi , mtu asiyependa maendeleo na kupewa na vyesi. Leo yanatokea hatutaki kukubali kwamba kuna watu walitufikisha hapa tunapambana na TL tena.
3. Jana TL kamaliza kwamba anaongea na wanaojua , siongei na wagonga meza, NDIYO MAANA JANA AKIONGEA WAZIRI MAIGA , AG na wengine walio makini pale bungeni walikuwa wanamuangalia kwa makini sana, labda utafute ile clip uone vzr. kwa watu wanaojua TL ana hoja ila kwa waliozidiwa na mahaba ya vyama na uzalendo wa kijinga wanamuona kama hana akili.

NIMALIZIE KWA KUSEMA HAYA, KATIKA BIBLIA NA KORANI WAPO MANABII NA MITUME WALIOTEULIWA NA MUNGU MWENYEWE TENA KWA KUAMBIWA. LAKINI KWASASA WAPO WATU AMBAO WANAUWEZO WA KUONA MAMBO YA MBELE WAKATI WENGINE HAWAYAONI NA WAKATI WENGINE WATAKAPOANZA KUYAONA WAO WANAONA MENGINE MBELE ZAIDI.
 
Back
Top Bottom