Najua na ninafahamu wapo watakaokataa,
Wapo watakaoponda na kubeza hoja hii kwa kuwa huionea aibu ingawa ina ukweli na pengine wao ni wafuasi wazuri pia.
Ni ukweli usiopingika kuwa wenye mafanikio wengi (Si wote) Ukichekecha upenuni siri ya mafanikio yao baadhi ni Uozo na Kichefuchefu kitupu na pengine aibu.
Wameyapata mafanikio hayo kwa njia zisizo za kiungwana na wanayalinda hivyohivyo pia,
Na vilevile maisha yao yanaonekana kwenda sawa kila siku yaani wapo vizuri.
Fikiria:
Una Mke/Mume ambae umeridhika nae, mmeshajenga familia nzuri tu,mmedumu kwa muda wakutosha na maisha yanakwenda wote mkiwa na furaha.
-Lakini kumbe yeye (mwenza wako) Kuwa nawe/kukupata na kufanikiwa kuishi nawe, Upo mkono wa kishirikina
(Kakufanyia Madawa ili kukupata na anakuweka/kakutuliza kwa madawa hayohayo)
-Haya Yapo na ni Maisha watu wanaishi.
AU
Ili, Mambo ya mwenza wako yaende sawa,
Shurti afanye ushirikina na wewe ukijua kabisa na kwa kuwa umo tayari katika ndoa na unajua kuwa hiyo ndio njia ya kupata mkate wa watoto unashirikishwa unakubali katika kufanya hayo makitu.
-Ni maisha pia.
Unaishi na Mumeo/Mkeo mmedumu si kidogo, Maisha yanaenda unafahamu kazi anayoifanya kumuingizia kipato siku zote.
Lakini, Kumbe kazi hiyo ni Kichaka cha shughuli nyingine Chafu na isiyosemeka katika hadhara pengine Mwizi ama Jambazi.
-Nayo ni maisha na watu wanaishi.
Ili upate mkate wako wa kila siku na 'ka-extra' inakubidi umdanganye Boss au Kumhadaa Mteja, Kufanyia wengine Fitna, Majungu, Uchonganishi,Uongo na wakati mwingine Ugombanishi-Na hatimae mkate wako unapatikana.
-Ni maisha na watu wanaishi.
Waswahili wanasema Si bure!