Shutuma za CCM dhidi ya CDM ni za Kweli?

Kama kweli chadema wana uwezo mkubwa namna hiyo wa kuwalead wanafunzi wasomi wa vyuo vikuu amost vyote nchini, maprofesa kama wa UDOM, wanafunzi kwenye daladala, walimu, wafanyakazi wa rshirika la reli, wazee wastaafu wa afrika mash na makundi mengine, basi kinastahili kukabidhiwa dola kwa uwezo wao mkubwa wa ushawishi na kukubalika kwao.
 
Naomba wanajf tujadili tuhuma hizi.

CCM chakishutumu Chadema migomo vyuo vikuu

Na Mwandishi wetu

13th February 2011

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimekituhumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kuwa kimekuwa kikichangia migomo ya wanafunzi wa Elimu ya juu, na kuchochea vurugu zinazoendelea vyuoni.
Tuhuma hizo zilitolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda alipokuwa akizungumza na Madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa, wa wilaya ya Kinondoni wa chama hicho juzi jijini.
Ng'enda alisema Chadema wamekuwa wanaleta migogoro na misukumo katika vyuo vikuu ili chama tawala CCM kiondolewe madarakani kwa migogoro hiyo.
"Vurugu hizi zina ushawishi mkubwa wa siasa hasa Chadema na hasa tukio la Arusha, walianzisha vurugu na wenyewe kukaa pembeni, hadi leo hakuna kinachoendelea baada ya wale watu kufa na kuzikwa, kikubwa waliambiwa wapumzike kwa amani," alisema.
Alisema CCM hakiwezi kung'olewa madarakani, na chama chochote bali kitajing'oa chenyewe, kwa kutokuwa na ushirikiano ndani ya chama.
Alisema kuwa chama kitahakikisha kinawapa vipaumbele wananchi kwa kuwatatulia shida zao zilizoko katika jamii, ili kukipa chama fursa ya kurudisha heshima yake katika kuogoza nchi.
Pia alimpongeza mgeni rasmi wa kikao hicho, Didas Masaburi Meya ya jiji la Dar es salam, kwa nia yake ya kujua ufanisi wa huduma za jamii katika manispaa zote tatu, katika ziara aliyokuwa anamalizia katika kikao hicho.
Dk. Masaburi katika ziara yake aliahidi mipira kwa kila kata, lengo likiwa ni kuweka vijana katika umoja wa chama, na kuwaingiza katika mpango wa ajira, katika kila kata wanazoishi, kama ulinzi shirikishi na usafi wa mazingira.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

KUMBE HATA KIPINDI KILE MZEE MWINYI ALITUKANWA MATUSI YA NGUONI UDSM KIKAFUNGWA NIMEKUMBUKA WALIHAMASISHWA NA CHADEMAAA!!!!!!!

Kweli mfa Maji haachi kutapatapa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Yaani badala ku-focus kuondoa matatizo ya watu yanayowafanya wagome wao wanakimbilia kuwatupia watu wengine lawama kama kwamba wanavogomea ni vya uongo. Huku ndio kunaitwa kufirisika kifikra, tatueni matatizo ya watu muone kama watagoma :twitch:!!
 
aksante sana mkulu. endelea kutujengea CHADEMA yetu. unakaribishwa pia.

ni vema sana kuwa mwanachama wa chama kinachoamsha walolala!
 
Jamani hata ukifuatilia mjengoni, Bwana Mapesa naye aliongea upupu huo, yaani! Hoja kweli ni hadimu!!
 
Mimi nakubaliana na anayesema chadema wanahusika na migomo na chokochoko zote zinazoendelea sasa hivi, how?
1. Chadema kimeondoa mental slavery-watu sasa wanaanza kujitambua na kujieleza -unafiki, nidham za uoga mwiko kwa chadema.
2. Chadema inalaani vikali propaganda na siasa za uongo za ccm, huwezi kuwahadaa wananchi kwamba uchumi unakua kwenye makaratasi wakati -huduma zote mbovu -hakuna maji, hakuna umeme, elimu hovyo, afya hovyo, barabara hovyo, wizi wa mali ya umma juu, wanachuo wanakosa mabweni, watanzania wengi wanalala chini na kwenye nyumba chafu na hovyo-chadema haipo teyari kuona wafanyakazi wakitaabika, chadema haiko teyari kuona wakulima wakikosa huduma za pembejeo, masoko, na miundombinu bora, chadema haiko teyari kuona reli ya kati ileile ya tangu ukoloni, chadema haiko teyari kuona elimu duni ya sekondari za kata, chadema haipo teyari kuona sheria inapindishwa, chadema haiko teyari kuona wafanyakazi wa bodi wakitanua kwa ufisadi wa pesa za walipa kodi huku walengwa wanachuo wakihangainga. Chadema imesema mara nyingi kwamba nchi haiwezi kutawalika kama kero na matatizo mengi ya watanzania hayawezi kupatiwa majibu na badala yake kuendelea na propaganda za uongo na unafiki. Leo hii kila kitu kimepanda bei ni wajibu wa serikali kutafuta majibu sahihi na kutatua matatizo badala ya kulia lia. Ninawaomba chadema wasirudi nyuma wazidi kusimamia haki na kusema ukweli kama alivyosema mdee, mnyika, silinde, tundu, wenje na timu nzima ya chadema bungeni kwamba kwenye sifuri itamkwe sifuri, na penye moja itamkwe moja siyo kumi, kwa kufanya hivyo wataifanya serikali kuwajibika na kuwaletea maendeleo wananchi -nawashauri ccm wasiendelee kuiona chadema mchawi kwakuwa kwa kufanya hivyo wanaipaisha siku hadi siku huku chadema ikiwasikiliza wananchi na kuiweka njia nyeupe kwenda ikulu.
 
Sijajua haswa what is the problem, ukiwa C cha Mafisadi hoja huisha, inabaki pumba tuu, tena pumba ya mpunga!
 
Nadhani ni kukwepa majukumu yao, wanafunzi wanadai haki zao nyie mwasema chademando waanzilishi? Kama wameanzisha basi wamekuwa wakicreate awareness kwa wanavyuo ni hii si kosa!
 
Hebu Wapeni haki zao tuone kama watagoma tena!!!!!!! Boresheni miundo mbinu nk tuone kama kutakuwa na nyoko nyoko ya mwanafunzi yeyete, ukisiki ujue ni CDM hao
 
Mohamed shosi ni mvuta bange mkubwa mi namfahamu sana toka utotoni. Na huwa anaropoka sana akilivuta hilo bange
je lisemwalo lipo kama halipo laja? Tuambie shosi
 
Siku za mwanzo walikuwa wanasema wanafunzi wa elimu ya juu wanatumiwa na VYAMA VYA UPINZANI siku hizi wamemodify msemo na kuwa WANATUMIWA NA CHADEMA, kwa nini na kwa nini leo?

CCM wako flexible wanabadilika kulingana na mazingira yanavyobadilika!
Tunawajua, tutazidi kuwajua na siku inakuja tutawajibisha.
 
Lisemwalo lipo kama halipo laja...............
sifikiri kama unawasaidia wana jamii katika kupata weredi chanya katika mada hii kwa kutoa misemo ya wahenga kama hilo.... show ur stand man so that we may get different view from different contributors including u......i dont think huyo mwenyekiti alifanya utafiti wa kutosha kwani reality ya maisha ndo contributor ya migomo..........ni kweli afahamu kuwa sh 5000 haikidhi maitaji ya mwanafunzi katika kipindi hiki...... ni kweli afahamu kuw mkate unauzwa 800/=, maji ya kilimanjaro 1000/=, lunch 2500/=,, what about diner? copies?transport?kiwi?dawa ya meno?...if real migomo ina kivuri cha CDM,,,big up kwani wamesaidia m2 kujitambua thaat msomi wa chuo kikuu 5000/= haikutoshi
 
NIKWELI CHADEMA INASABABISHA MIGOMO YOOTE NCHINI WAKUBWA!
ELIMU ILIYOTOA CHADEMA KUHUSU HAKI ZA WANACHI ZINASABABISHA MIGOMO!
DHARAU KWA SERIKALI YA JK CHADEMA INASABABISHA, CCM WAMECHAKACHUA MATOKEO MKATOA SIRI HADHARANI!
DOWANS, EPA NA UFISADI MWNGINENEO WA CCM CHADEMA WAMEUFICHUA!
CHADEMA HAMUWEZI MKAKWEPA KWA HILI TAFADHALI! n
 
mimi nakubaliana na anayesema chadema wanahusika na migomo na chokochoko zote zinazoendelea sasa hivi, how?
1. Chadema kimeondoa mental slavery-watu sasa wanaanza kujitambua na kujieleza -unafiki, nidham za uoga mwiko kwa chadema.
2. Chadema inalaani vikali propaganda na siasa za uongo za ccm, huwezi kuwahadaa wananchi kwamba uchumi unakua kwenye makaratasi wakati -huduma zote mbovu -hakuna maji, hakuna umeme, elimu hovyo, afya hovyo, barabara hovyo, wizi wa mali ya umma juu, wanachuo wanakosa mabweni, watanzania wengi wanalala chini na kwenye nyumba chafu na hovyo-chadema haipo teyari kuona wafanyakazi wakitaabika, chadema haiko teyari kuona wakulima wakikosa huduma za pembejeo, masoko, na miundombinu bora, chadema haiko teyari kuona reli ya kati ileile ya tangu ukoloni, chadema haiko teyari kuona elimu duni ya sekondari za kata, chadema haipo teyari kuona sheria inapindishwa, chadema haiko teyari kuona wafanyakazi wa bodi wakitanua kwa ufisadi wa pesa za walipa kodi huku walengwa wanachuo wakihangainga. Chadema imesema mara nyingi kwamba nchi haiwezi kutawalika kama kero na matatizo mengi ya watanzania hayawezi kupatiwa majibu na badala yake kuendelea na propaganda za uongo na unafiki. Leo hii kila kitu kimepanda bei ni wajibu wa serikali kutafuta majibu sahihi na kutatua matatizo badala ya kulia lia. Ninawaomba chadema wasirudi nyuma wazidi kusimamia haki na kusema ukweli kama alivyosema mdee, mnyika, silinde, tundu, wenje na timu nzima ya chadema bungeni kwamba kwenye sifuri itamkwe sifuri, na penye moja itamkwe moja siyo kumi, kwa kufanya hivyo wataifanya serikali kuwajibika na kuwaletea maendeleo wananchi -nawashauri ccm wasiendelee kuiona chadema mchawi kwakuwa kwa kufanya hivyo wanaipaisha siku hadi siku huku chadema ikiwasikiliza wananchi na kuiweka njia nyeupe kwenda ikulu.
aaah denyo umefikilia the same na mimi kwa hiyo cdm ndo wakulaumiwa na mafisadi, hutuna haja yakuona kama ccm wanakose ila wanapatia saana!
 
Back
Top Bottom