Shule ya sheria Tanzania ni kituko

Waliofeli watakuwa na majibu mazuri ngoja tusubili mkuu ili tuunganishe dot.
 
Wnakosesha mapato taifa kwa kuminya ajira za vijana hii fani si ndo unaweza kuajiliwa au kujiajili!!
 
Wabongo tunapenda slope sana... Yani akili yako haijatulia unataka upewe muhuri??

Kuna mwingine juzi amesoma kozi ya arts alafu anataka akasajiliwe erb tena awe professional engineer!!

Nani katuloga?? Aloo kama huwezi kufaulu nenda kafanye kazi ingine... Nyie ndio mawakili mnaokuja kukimbizwa na akina lissu na kibatala mahakaman, vichwan hamna kitu kabisa!!
 
Hivi ni vitengo vya kujipatia pesa group fulani habari ziwafikie ile bodi flani karibu na maktaba
 
Soma ww acha kulialia mbona watu wanatoboa tu
 
Mleta mjadala nadhani ni mvivu wa kusoma. Nashauri ajiulize je wanaofaulu wakoje? Ukitaka kufanya vizuri kwenye elimu huna budi kuacha anasa na kulalamika. Kata shule ipasavyo kama hutapasua nyavu.
 
Mkuu utazunguka sana ila jibu ni moja, umefeli kwasababu hukusoma au hukuweka juhudi! msianze kuzunguka na kuruka ruka hapa haitawasaidia
 
Kwa maana hiyo kusiwepo n kufeli kabisa wakiingia 600 wote wafaulishwe tu!! Kweli taifa la wajinga hili
 
Mkuu nikueleweashe kidogo. Shule ya sheria ya UDSM km inavyojulikana inaongozwa na watalaamu kutok a pale UDSM hivyo hata systems za ufundishaji na ufanyaji mitihani ni wa UDSM. Vijana waliosomea sheria vyuo vingine vya kibiashara ambavyo wanaangalia pesa na sio uwezo wa mtu darasani wakifika pale shule ya sheria huwa lazima wafeli kwani wamezoea kusoma kwa mazoea na kufaulu mitihani. Pale UDSM bila kusoma na kuelewa huwezi kufaulu mitihani hata ukiwa ni nani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…