Shule ya msingi Muhimbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule ya msingi Muhimbili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rosweeter, Jan 27, 2012.

 1. Rosweeter

  Rosweeter JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 1,136
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikiguswa sana na hali ya mazingira ya Shule ya msingi Muhimbili. Imekuwa ni kawaida kwa maji machafu kufurika na kumiminika katika mazingira ya shule hiyo. Hali inakuwa tata zaidi inyeshapo mvua. Nina miaka saba katika maeneo haya na siku zote hali imekuwa ikijirudia mara kwa mara.

  Mazingira haya ni hatarishi sana hasa kwa watoto wadogo wanaosoma shule hapo. Ninaamini afya za watoto hawa zinalindwa kwa kudra za mwenyezii Mungu tu kwani wako katika mazingira hatarishi sana hasa yatokeapo magonjwa ya milipuko. Ninachoshangaa ni jinsi ambavyo wahusika wamelifumbia macho suala hili na kuonekana kuridhika kwa kukaa bila kuboresha miundo mbinu katika shule hiyo na mazingira yanayoizunguka. Uongozi wa shule na kamati ya shule hawalioni jambo hili? Wazazi mnaosomesha wenye watoto katika shule hii mmeridhika na hali hii? Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, ni wajibu wenu kuhakikisha miundo mbinu inaboreshwa.

  Wito wangu naomba Halmashauri husika ilifanyie kazi suala hili siyo kusubiri mpaka maafa yatokee ndiyo ionekane kuna tatizo kama ambavyo tumeshazoea.

  Nawasilisha.
   
 2. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Yapo upande gani maji hayo? Mwanangu anasoma hapo...
  Ni huku upande wa makaburinii au...?
   
 3. Rosweeter

  Rosweeter JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 1,136
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Yakianza kutitirika siyo ya kutafuta mpaka getini na barabara kubwa ya United Nations, kiasi kwamba hata kuvuka barabara huwa ni shida.
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,872
  Trophy Points: 280
  Labda sereakli yenu iko kwenye MCHAKATO wa kulishughulikia vuteni subira kidogo.
   
 5. Rosweeter

  Rosweeter JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 1,136
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Hii michakato isiyokwisha hii imetuchosha
   
 6. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  mi siishi Dar.. Kwa kipindi hiki hali si shwari kutokana na uhaba wa mvua au..?
   
 7. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mmmh!!! subiri serikali iunde kamati ya kuchunguza miundombinu ya maji taka shuleni hapo and then watalipana posho kibao trust me!!!
   
 8. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  hizi shule zilizopo mijini ni ambazo wajanja wanasubiri watanganyika wanaofahamu ni mali ya umma wafe wote ili wajimilikishe viwanja. Mojawapo ni shule ya msingi bunge. Watanzania mtakaobaki na kuuliza mtaambiwa hivi vilikuwa viwanja vye tuliviacha tu,sasa tumeamua kuvitumia,mtaoneshwa na hati kabisa. Miaka kumi ijayo pale takutana na minara ya nyumba mingi,bila serikali ya magamba kutoka madarakani we are dead!
   
Loading...