Shule kukosa madawati ni uzembe wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule kukosa madawati ni uzembe wa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Malipesa, Mar 7, 2012.

 1. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba wa JF mniwie radhi kama hii itakuwa imesawahi kutolewa hapa, ila ni kwa umuhimu wake ndo nimeamua kopst.

  Sekata ya elimu ni sekta nyeti kabisa katika nchi yoyote.

  Ni kitu cha ajabu kabisa kuona shule zetu hapa nchini zinakosa madawati na kupeleka baadhi ya wanafunzi wake kukaa chini.

  Hili la shule zetu ukosa madawati haingii akili kwa mtu yeyote anayeifahamu tz vizuri, nasema hivi kwa sababu tz ni mojawapo ya nchi zenye misitu mingi katika maeneo mengi ya nchi. Viongozi wetu wanashindwa kuchukua hatu madhubuti kuhakikisha rasilimalizetu ziantumika kwa manufaa ya watz badala yake kwa hili utakuta tani za magogo zinavunwa na kusafirishwa nje tena wakati mwingine kwa magendo ya wazi kwani wakubwa wa nchi wanaliona hili na kulinyamazia kwa manufaa yao binafsi.

  Ukiacha rasilimali ya misitu ambayo magogo yangepatikana na kupeleka kuwa na mbao nyingi za kutengeneza madawati mengi kabisa hadi ya ziada, lakini pia tuna rasilimali nyingine nyingi ambazo sehemu ya mapato yake yangeelekezwa kwenye elimu ambapo kimsingi kwa nchi km tz wala wananchi wasingetakiwa kugharamia elimu kwa kiasi kikubwa kama ilivyo kwa sasa.

  Kumbe kwa utajiri ambao tz inao kama ufisadi usingekuwa kwa kiasi kikubwa km ilivyo sasa hata elimu ingeweza kutolewa bure.

  Kwa maoni yangu, nahitimisha kwa kusema shule kukosa madawati ni uzembe wa serikali (serikali zilizopita na zilizo madarakani)

  Karibuni kwa michango zaidi na maoni.
   
Loading...