Shuhuda nyingi za 'wanaompokea bwana' makanisani huwa za uongo

jasmine jamil

Member
Nov 1, 2016
5
39
Nilikutana na rafiki yangu mmoja week iliyopita Jumapili akawa ameniomba sana sana niende kanisani kwake, mimi ni muislam alinishawishi sana Jumapili kweli nikaenda wana kipindi chao cha shuhuda, akaenda mbele akasema alikuwa ananiombea sana rafiki yake niokoke na kweli eti nimekubali kuokoka na nipo kanisani akaninyooshea kidole watu wakashangilia sana sikupewa hata muda wa kusalimia.

Nikakaa tu wakahubiri pale muda wa kutoka nikaambiwa nibaki na mchungaji nilivobaki nikamwambia hiyo bwana mchungaji mimi sijawahi kuwa mkristo wala sijaokoka hata sielewi ni kwanini huyu mama rafiki yangu anadanganya, akaniambia samahani wakaingia chumba cha nyuma huko wakawa wanamgombeza wanamwambia wewe ipo siku utaharibu kila kitu, tena rudisha hela yote hustahili kupewa kitu.

Kuna watu huwa wanabadili dini na kuwa wakristo wakishafika huko huwa wanaambiwa watoe shuhuda zao wengi hudai wakati wakiwa waislam waliteseka na majini na mapepo na walifanya sana madawa bila kupona ila walipookoka eti wakapona kana kwamba kwenye uislam kuna uchawi na mapepo huo ni upuuzi mkubwa sio kweli kwenye uislam kuna mapepo au majini kwani wakristo wangapi wanateseka na nguvu za giza, uchawi na mapepo?

Mbaya zaidi hao wanaobadili dini walikuwa tu waislam majina hata kuswali unakuta walikuwa hawaswali hawajui dini wakipata tu mitihani ya maisha wanakimbilia kwa waganga, matokeo yake wanapata madhara wanasingizia uislam, kwani uslam ndo unasema mtu afuge majini au avae hirizi hujui dini, hujui kuswali, hujui kufunga unadai umeokoka acheni dini ya Mwenyenzi Mungu

Jasmine Jamil proudly muslim!
 
Miongoni mwa maeneo ambayo sijakuamini ni kusema ulisikia akiambiwa arudishe hela.

Kulingana na ulivyoandika, Unashauri watu waanze kuwalaumu waganga na siyo Uislam?
Unawazungumziaje ambao hawakwenda kwa waganga ila wakabadili dini moja kwa moja?
 
Watu wana marafiki na ndugu wa imani tofauti..lakini inapofika mida wa kuabudu kila mmoja anaelekea anapoamini. Iweje wewe mnafiki umsindikize rafiki kanisani? Inaelekea hata msikitini hujawahi kuingia...sasa si ni bora ubatizwe na jina lako ni Josephine..
 
Kuingiza mtu kwenye dini yako kwa hadaa..

Asee hawa walokole wana matatizo gani lakini?,
mbona wakatolic hawako desperate kiihivyo.hata wasabato atakuhubiri sana lakini hawezi tumia ujanja janja ili eti mtu ufuate dini yake.
Hii ni aibu sana
 
Wewe mwenyewe muislam jina tu, ungekuwa muislam kweli usingekubali kuingia kanisani hata kwa panga.
Pia hujui hata majini na uislam ni kama maombi na walokole
Kwani uislamu na ukristo ni uadui hadi ushindwe kuingia sehemu anayoabudu rafiki/ndugu yako?
 
Nilikutana na rafiki yangu mmoja week iliyopita Jumapili akawa ameniomba sana sana niende kanisani kwake, mimi ni muislam alinishawishi sana Jumapili kweli nikaenda wana kipindi chao cha shuhuda, akaenda mbele akasema alikuwa ananiombea sana rafiki yake niokoke na kweli eti nimekubali kuokoka na nipo kanisani akaninyooshea kidole watu wakashangilia sana sikupewa hata muda wa kusalimia.

Nikakaa tu wakahubiri pale muda wa kutoka nikaambiwa nibaki na mchungaji nilivobaki nikamwambia hiyo bwana mchungaji mimi sijawahi kuwa mkristo wala sijaokoka hata sielewi ni kwanini huyu mama rafiki yangu anadanganya, akaniambia samahani wakaingia chumba cha nyuma huko wakawa wanamgombeza wanamwambia wewe ipo siku utaharibu kila kitu, tena rudisha hela yote hustahili kupewa kitu.

Kuna watu huwa wanabadili dini na kuwa wakristo wakishafika huko huwa wanaambiwa watoe shuhuda zao wengi hudai wakati wakiwa waislam waliteseka na majini na mapepo na walifanya sana madawa bila kupona ila walipookoka eti wakapona kana kwamba kwenye uislam kuna uchawi na mapepo huo ni upuuzi mkubwa sio kweli kwenye uislam kuna mapepo au majini kwani wakristo wangapi wanateseka na nguvu za giza, uchawi na mapepo?

Mbaya zaidi hao wanaobadili dini walikuwa tu waislam majina hata kuswali unakuta walikuwa hawaswali hawajui dini wakipata tu mitihani ya maisha wanakimbilia kwa waganga, matokeo yake wanapata madhara wanasingizia uislam, kwani uslam ndo unasema mtu afuge majini au avae hirizi hujui dini, hujui kuswali, hujui kufunga unadai umeokoka acheni dini ya Mwenyenzi Mungu

Jasmine Jamil proudly muslim!
Ni sawa kabisa Jasmin huyo mama alifanya makosa kwa kuwa alisema uongo.Jasmin kumbuka lakini kwamba mmeambiwa muwaulize watu wa kitabu kama kuna jambo lolote ambalo ninyi kama Waislamu hamlielewi. Cha kushangaza Ni kwamba hamtaki kutuuliza,na mnatuita "makafir."Kumbuka pia kwamba Yesu au Isa Bin Mariam ndiye ambaye kwenye siku ya kiama atawahukumu wanadamu,wewe na mimi. Hii ni kutokana na Quran.Akili ya kawaida kabisa inaniambia kwamba ni busara kujua atakaye nihukumu atanihukumu kwa lipi Jasmin! Kama basi hujaamua kuokoka kwa sasa, mjue basi huyu Isa Bin Marian kwa kuwa ndiye atakaye kuhukumu.
 
Back
Top Bottom