Shughuli mbalimbali za Rais mstaafu dkt. Jakaya Kikwete Washington DC

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ameshirikia katika Kongamano la Kimataifa la Afya lijulikanalo kama World Health Congress lililofanyika jijini Washington D.C. tarehe 12 Machi, 2016. Katika Kongamano hilo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa ni mmoja wa Wanajopo katika mjadala unaohusu Mbinu Bora za Kukabiliana na Majanga ya Afya.

Katika mjadala huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alielezea uzoefu ambao Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kutafuta Namna Bora ya Kukabiliana na Majanga ilioupata katika nchi zilizoathiriwa na janga la Ugonjwa wa Ebola. Alieleza kuwa dunia iko katika hatari kubwa ya kuathiriwa na majanga ya afya kutokana na kuweko na mfumo dhaifu wa sekta ya afya katika nchi zinazoendelea. Alisisitiza umuhimu wa nchi zilizoendelea kusaidia nchi znazoendelea kuimarisha mifumo ya afya ikiwemo kujenga uwezo wa wataalam wa afya na namna ya kukabiliana na milipuko.

Aidha, ameelezea umuhimu wa kupitia upya muundo na mifumo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kuliwezesha kukabiliana na majanga kwa wakati ambako kwa sasa uwezo wake huo ni mdogo, na unategemea zaidi msaada na utayari wa nchi wanachama. Dkt. Kikwete amesisitiza pia umuhimu wa dunia kuwekeza katika utafiti na ugunduzi wa kinga dhidi ya magonjwa haswa yale yanayokabili nchi masikini. Kwa ajili hiyo, Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kukabiliana na Majanga imeshauri kuanzishwe mfuko maalum wa fedha za kwa ajili ya kuchochea utafiti na utengenezaji wa chanjo za magonjwa hayo.

Katika hatua nyingine, Rais Mstaafu jana tarehe 13 Aprili ameshiriki Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kushauri Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu kwa Wote Duniani inayoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mheshimiwa Gordon Brown. Tume hiyo inayotegemewa kuwasilisha Ripoti yake mwezi Septemba, 2016 ina lengo la kutafuta namna bora ya kuondoa tofauti iliyopo katika viwango vya elimu duniani ifikapo mwaka 2040. Azma ya Kamisheni hiyo ni kufikia usawa katika elimu ambapo ifikapo mwaka 2040, mtoto atakayesoma shule kutoka nchi yoyote alipo duniani apate elimu yenye ubora unaolingana na wenzake kote duniani. Azma hiyo inatokana na uhalisia kuwa kwa kasi iliyopo sasa, itazichukua nchi zinazoendelea miaka 65 kufikia viwango vya elimu vya sasa vya nchi zinazoendelea.

Kwa kuanzia, Kamisheni inakusudia kupendekeza mapinduzi ya kifikra yatakayowezesha watoto wote wanaosoma katika nchi zinazoendelea wafikie viwango vya ubora wa elimu wa nchi za uchumi wa kati ifikapo mwaka 2030 na wale wa nchi za uchumi wa kati wafikie viwango vya ubora wa elimu wa nchi zilizoendelea ifikapo 2030. Rais Mstaafu Kikwete aliteuliwa kuwa Kamishina wa Kamisheni hiyo kutokana na uzoefu na mchango wake katika kupanua fursa za elimu katika kipindi chake cha miaka 10 ya uongozi wake. Mkutano ujao na wa mwisho wa Kamisheni hiyo utafanyika Oslo, Norway mwezi Julai, 2016.
 
Safari hii hakuomba mumpige picha ili mzisambaze humu mtandaoni jinsi anavyokula bata kama mlivyokuwa mkifanya alipokuwa madarakani?
 
jk anaonekana anajua vitu vingiiii lakini ameshindwa kutusaidia wa tanzania anashiriki mikutano mikubwa inayohusu afya anasimama anaongea vizuri tu point tupu lakini bongo wagonjwa wanalala hadi uvunguni mwa kitanda ndio maana magufuli akapiga marufuku safari hazina faida yoyote hyo gharama kwenda mkutano wa afya nunulia madawa.
 
Back
Top Bottom