figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,689
- 55,662
Prof. Issa Shivji. picha na Bongo Celebrity
Watanzania wametakiwa kuwa makini na suala la umiliki wa ardhi, wakati huu ambapo kumekuwepo na kiu kubwa juu ya rasilimali hiyo kutoka kwa wawekezaji.
Hayo yamesemwa na Profesa mashuhuri wa sheria nchini, Issa Shivji, katika kongamano la kumbukizi ya mwanamapinduzi wa Guyana, Walter Rodney aliyewahi kuandika kitabu cha “How Europe underdeveloped Africa” iliyofanyika leo Juni 10, jijini Dar es Salaam
Prof. Shivji amesema kuwa endapo suala hili halitoangaliwa kwa umakini, nchi inaweza kujikuta katika matatizo ya ardhi kama Zimbabwe na kusababisha migogoro mikubwa.
Shivji ameongeza kuwa ipo haja ya kuwepo kwa mijadala juu ya ardhi ili kuliweka sawa suala hilo na kuepusha hisia za uporaji.
Prof. Shivji amesema kuwa nchi bado ipo katika matabaka ya walionacho na wasionacho hali ambayo haileti mustakabali mwema kwa vizazi vijavyo.
Chanzo: AZAM TV