Tetesi: Shirikisho la vyuo elimu ya juu Kilimanjaro utata mtupu, wagushi nyaraka kugombea

Kikuburu

Member
Jul 8, 2016
43
30
Heri ya x mass wote.

Habari za mtifuano ndani ya shirikisho la vyuo vya elimu ya juu mkoani kilimanjaro (CCM) za vuja,
Kama mnakumbuka katibu mkuu wa shirikisho(ccm) DANIEL ZENDA akiongozana na hamasa taifa,Kaimu mwenyekiti taifa alifanya ziara ya kikazi mkoani hapo na blog moja iliripot ziara hiyo.Ambapo walifungua tawi lingine Tawi la SAUT ARUSHA.

Katika ziara hiyo walitangaza nafasi 2 mwenyekiti wa seneti ya mkoa Kilimanjaro kwa kuwa mwenyekiti wa sasa NHUUMBA amemaliza katika chuo cha udaktari KCMCU na kuonekana yuko mbali wakati anafanya mazoezi kwa vitendo hivyo ufanisi wa kazi hautakuwepo na mchumi wa mkoa ambaye amehitimu.

Nafasi ilipotangazwa, katibu wa mkoa bwana Samson Joseph ndipo wagombea walitakiwa kuchukua form kwa makatibu wa matawi.

PICHA IKAANZA
Mnamo tarehe 14/11/2016 ambayo ni siku moja kabla ya tarehe ya mwisho ya kuchukua form za kugombea vijana wawili ROBERT SATURINE&SAMWELI KAMANDWA
walimpigia simu Bi Mwajuma Fadhili katibu wa tawi la mwenge majira ya jioni karibia saa moja na kisha wakafika alipo na kumuambia wanahitaji form. Mtoa taarifa anasema katibu huyo aliwahoji kwanini wanakuja kuchukua form usiku na deadline ni kesho yake na mda wa kazi umekwisha? Wakadai walishindwa kupata mawasiliano naye hadi walipopata namba kwa mwanachama mmoja.

Swali lingine aliwahoji kwa nini wanakuja kujitambulisha kwenye tawi kwa mara ya kwanza usiku na kuomba form ya kugombea nafasi ya mkoa? wakajibu kuwa mwenyekiti wa tawi anawafahamu. Katibu huyo akawaomba wamuonyeshe kadi zao za chama cha mapinduzi na pia hawakumuonyesha.

Katibu wa tawi hilo akaishia kuwapatia form ambazo hazina mhuri na sahihi yake ili kesho yake akutane nao kwa kujiridhisha zaidi.

Inasemekana walijaza form hizo na wadhamini wao wote walitoka nje ya tawi, mmoja tu anatoka hapo ila na yeye hajulikani kwenye tawi.

Alipofuatilia taarifa zao kwa mmoja wa wasajili wa chuo alibaini hawajasajiliwa katika chuo hicho,
na mmoja wao aligundulika kuwa namba ya usajili aliyotoa ni ya mtu mwingine sio yake. Kisha akaamua kumtaarifu mwenyekiti kwa ufuatiliaji zaidi.

Mwenyekiti wa mkoa aliamua kufika chuoni hapo na kubaini yafuatayo:
ROBERT alijaza form tarehe 15/11 ndiyo deadline lakini alisajiliwa tarehe 21/11 na namba ya usajili aliyoitoa hadi siku ya mwisho wa kuchukua form chuo kilikuwa hakijafikia namba hiyo. Hivyo baada ya kutoa ile namba akavizia ili asajiliwe kwa namba ile ile baada ya week 1. japo hadi siku hiyo alikuwa hajajisajili kwenye idara yoyote wala kwa mhasibu taarifa zake haziko vizuri.

Mwenzake SAMWEL alibainika hajasajiliwa kabisa japo wote waliambatanisha joining instruction form zao na namba za usajili(haijulikani walizipataje)

Hivyo mwenyekiti alipata taarifa ya maandishi kutoka mwecau juu ya ubabaishaji wa vijana hao.

Chakushangaza baada ya majina yao kutojadiliwa kwakuwa hawana sifa sio wanachuo walipeleka malalamiko yao moja kwa moja taifa (kwa katibu ZENDA) bila kuwataarifu ama kupitia kwa makatibu wa tawi na mkoa.

Uchaguzi huo hadi leo haujafanyika kwakuwa taifa hawajatuma majina ya waliopitishwa na wanadai wapo wengine waliotuma malalamiko yao japo hawawataji moja kwa moja.

SINTOFAHAMU: Siku ya ziara yao mkoani kilimanjaro kuna taarifa za chini chini kwamba katibu taifa aliwasiliana na mmoja wa wagombea hao yeye ndiye ampokee na akamtafutia mahali saafi pa kulala badala ya kupekelewa na viongozi wa mkoa kwa kuwa ni ziara ya kikazi.Katibu wa mkoa aliwapa onyo kuwa kama ni ziara ya kikazi basi walale walipoandaliwa na uongozi kama ni ziara binafsi waende huko ndipo wakalala kwa shingo upande.

Maswali:

.Je huyu katibu taifa na hawa wanodaiwa kugushi wana uhusiano gani?

.Kwa nini ziara ya kikazi alichonga kukutana na mtia nia huyo mahala pao?

.Je malalamiko yao kwanini hayakupitia kwenye tawi lolote wala mkoani?

.Huyo mgombea robert anang'ang'ania nini mkoani hapo kwa kuwa yeye ndiye alikuwa mwenyekiti
kwa mda mrefu na kushindwa uchaguzi mwaka huu april?
.Mwenyekiti wa tawi hakuonyesha kugushwa na jambo hili.

.Serikali yetu na ya chuo imewachukulia hatua gani watu hawa endapo kweli waligushi?

INASEMEKANA KATIKATI YA SAKATA HILO KATIBU WA TAWI MWENGE ALIJIHUDHULU
japo taarifa rasmi haikutolewa mkoani na kwa wanachama imebaki tetesi! sijui tatizo ni nini?

CCM ni ile ile huyo katibu ahamie upinzani tujenge nchi.
Mfumo huu ndio unatuletea viongozi mafisadi kumbe mnalindana tangia chini kabisa.
 
Back
Top Bottom