Shirikisho la elimu washirikiana na UWT taifa kuadhimisha siku ya mama duniani

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
879
969
Viongozi mbalimbali wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Vyuo Vya Elimu ya Juu CCM wakiongozwa na M/kiti wa Shirikisho Taifa Bi Zainab Abdallah na viongozi wengine kutoka Dodoma na Iringa leo wameshirikiana tena na UWT mapema asubuhi katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika kumuenzi na kumpongeza Mama Samia Suluhu Hassan, Mwanamke na mwana mama wa kwanza katika historia ya nchi yetu kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya usafi, kutembelea wodi za kina mama na kukabidhi vifaa mbalimbali.

Wakati huo huo, Shirikisho Vyuo Vya Elimu ya juu Mkoa wa Dodoma kupitia vyuo vya Udom, Mipango na Hombolo kwa mara nyingine asubuhi ya leo wamechangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama na watoto ambao wamekuwa wakipoteza maisha kwa kukosa damu.

M/kiti wa Shirikisho Taifa anatarajia pia kushiriki katika mkutano wa hadhara wa kumpongeza Mwanamke wa nguvu, Mwanamke wa mfano, Mwanamke wa Mwaka, Mwanamke Shujaa, kipenzi cha kina mama, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan viwanja vya Nyerere Square Mchana huu.

Uongozi wa Shirikisho Taifa unampongeza sana Mama Samia Suluhu Hassan, ikiwa leo ni siku ya mama duniani. Tunamtakia kila la heri ktk utekelezaji wa majukumu yake katika ujenzi wa taifa. Tunachukua fursa hii pia kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa kuwapa akina mama nafasi mbalimbali za kuwatumikia watanzania na kutuletea Makamu wa Rais wa Kwanza Mwana Mama. Tunamshukuru pia kwa kuboresha sekta ya elimu na afya kumkomboa mwana mama wa Tanzania. Tunamtakia Mh Rais kila la heri ktk kutekeleza majukumu ya ujenzi wa Taifa. Tutaendelea kumuunga mkono kwa kufanya kazi ili taifa letu liweze kusonga mbele.

Tunawatakia wakina mama wote nchini heri, baraka na mafanikio. Shime akina mama!!! Nani kama Mama??

Mungu Ibaraki Tanzania.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Imetolewa na:
Zainab Abdallah
M/kiti wa Shirikisho Taifa (Mnec),
Vyuo Vya Elimu ya Juu.
 
Back
Top Bottom