Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)

hakuna shida

Member
Dec 16, 2015
25
5
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga tunaomba radhi wateja wote wanaohudumiwa na laini ya Kahama kutokana na kukosekana kwa huduma ya umeme siku ya
leo Jumanne tarehe 22 Machi, 2016 kuanzia saa 10:07 jioni hii. Katizo hili ni baada ya nguzo kuanguka eneo la Isaka.
Maeneo yaliyoathirika na katizo hili ni maeneo yote ya Ugweto, Usanda, Tinde, Kagongwa mpaka Kahama Mjini.
Mafundi wetu wanaendelea na juhudi za kurekebisha na kuweza kurejesha huduma kwa watumiaji wote wa laini hii.
Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano Makao Makuu.
 
Back
Top Bottom