enery
JF-Expert Member
- Aug 21, 2015
- 368
- 439
Nipende kuanza kwa kuwajulia hali ndugu zangu watanzania na wazalendo wa nchi yetu pendwa yenye mito na mabonde mengi ya nafaka. Kubwa nalopenda kuandika leo ni juu ya Shirika letu la nyumba la Taifa (NHC). Kwa muda sasa shirika limekuwa katika mpango wa kujenga nyumba za bei nafuu, lakini sioni tija ya mradi huu wala mwisho wake utakuwaje kwa kipato cha watanzania wa sasa. Niliona Kigoma juzi kati katika taarifa ya habari, Naibu waziri wa Aridhi, akijaribu washawishi watumishi wa umma kununua nyumba zile, kweli ni bei nafuu, nimeona dodoma nyumba ya bei ya chini ni milioni 57 je nani ataweza kumuda kwa hali ya uchumi wa sasa.
Kumukuwa na ongezeko kubwa la kodi za nyumba toka kwa wamiliki wa nyumba kutokana na kutokuwepo kwa chombo shindani kinachoweza wafanya washushe bei zao badala ya kuendeelea kupandisha.
Ningeona tija kwa shirika la nyumba mfano kwa mkoa wa dodoma badala ya kujenga huo mradi wao wa nyumbu, wangeenda maeneo ya Uhindini na kwingine ndani ya manispaa ya dodoma na kununua zile nyumba za mika ya 1958 pale uhindi wakajenga maghorofa ya kutosha kwa ajjili ya kupangisha na ksiha kukusanya kodi kwa miezi mitatu mitatu, hii ingeafanya kodi pia mtaani kushuka toka kodi za mwaka mara miezi sita mpaka miezi mitatu pia.
Uhindini kwa sasa ina miundo mbinu mizuri ya barabara, maji taka, umeme na maji safi pia, ila nyumba ni za kizamani sana.
Sielewi hii miradi inajenga ya nyumba za bei nafuu mmetuangalia watanzania wate kwa ujumla kipato chetu kipoje ama mnajenga mje nunua watu wenye uwezo tu kisha mtupangishe tena?
Ni swali nalojiuliza kila panapokucha bila kupata majibu ya uhakika.
TBA walijitahidi sana kujenga yale majengo ya site 1, Site 2 na Site 3 pale area D. laiti kama kungekuwa na majengo mengi ya dizaini ile kila mahali Tanzania Dar es salaam, Dodoma, Morogoro, Iringa, mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya nk, pesa ambayo shirika lingekusanya ingekuwa maradufu ya kile wafanyacho sasa. Ingekuwa imesaidia vijana wengi kuishi mahali pazuri, Dar es salaam mradi wa kawe sijui utakuwaje kwa maisha ya watanzania wa sasa na kipato chao.
Angalie faida wapatao wamiliki wa nyumba za kawaida tu kwa sasa, je kama shirika lingekuwa na miradi kama iyo mngekuwa wapi?
Napenda kuwasilisha
Niwatakie siku njema na kazi njema katika ujenzi wa taifa