Shinyanga: Zaidi ya shilingi Bilioni 3 zatumika kujenga jengo la hospitali ya wilaya Kahama

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
1643627520240.png

Zaidi ya shilingi Billion 3 ambazo ni fedha za mapato ya ndani ya halimasahuri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga zimetumika kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika hospital ya wilaya Kahama.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo kwa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga mganga mkuu wa hospitali ya Manispaa ya kahama Dk Lucas David amesema ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 90 na utasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa ambapo kwa sasa hospitali hiyo inapokea wagonjwa wa nje 1000 kutoka katika wilaya za mikoa ya Tabora na Geita.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Anderson Msumba amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo utakamilika machi mwaka huu.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa kamati hiyo Mabala Mlolwa ameipongeza halmashauri ya manispaa ya Kahama kwa kuongoza katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa asilimia 67 katika nusu ya mwaka wa fedha 2021/22.

“Tumepokea kwa furaha taarifa ya Waziri wa tawala za mikoa ana serikali za mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa ya kuzitangaza halmashauri zilizofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato hiyo ni ishara ya utendaji kazi bora kwa watumishi wa umma ambao ndio watekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM” alisema Mlolwa.

Credit; Star TV
 
Back
Top Bottom