Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 638
- 1,771
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, ameonya vikali dhidi ya wale wanaotaka kununua nafasi za ubunge, akisisitiza kuwa kitendo hicho ni ukiukaji wa maadili ya chama na hakitavumiliwa. Badala yake, amewashauri kutumia fedha hizo kuanzisha biashara kama maduka.
Wasira alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi katika mkutano uliofanyika mjini Shinyanga.
Alieleza kuwa CCM imebadilisha mfumo wa upatikanaji wa wagombea wa ubunge kwa kura za maoni, ambapo idadi ya wajumbe wa kupiga kura imeongezeka kutoka 400 hadi 4,800. Lengo la mabadiliko hayo ni kuhakikisha mgombea anayepatikana ni chaguo halisi la wananchi.
Chanzo: Nipashe

Aliongeza kuwa hata kwa kiwango hicho cha fedha, mgombea hatoweza kutoa rushwa ya kutosha kwa kila mjumbe, akisema:"Zamani mlikuwa mkiwahonga shilingi laki moja moja kwa wajumbe 400. Sasa hivi wapo 4,800; kwa kiwango hicho hicho cha hongo, ni sawa na shilingi milioni 400. Si bora fedha hizo ufungue duka? Unanunua ubunge wa nini wakati mshahara wa mbunge ni shilingi milioni nne tu?" alisema Wasira.
"Huwezi kutoa milioni 400, utawapa tu shilingi elfu kumi kila mmoja, lakini sisi tutakushughulikia kimaadili. Tunataka mtu achaguliwe kwa hiari ya wapiga kura, si kwa kununua ubunge. Lazima turudishe nidhamu ya chama."
Chanzo: Nipashe