SHINYANGA: Aporwa kisu asijiue, ajichinja kwa chupa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,471
2,000
Mkazi wa Mtaa wa Mabambase katika Manispaa ya Shinyanga, Saada Elias(24) amefariki dunia kwa kujikata koromeo kwa chupa ya soda.

Mwanamke huyo alijiua kwa chupa muda mfupi baada ya kunyang'anywa kisu wakati akijaribu kujichinja kwa madai ya kuandamamwa na ugumu wa maisha.

Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa tisa usiku, wakati Mwanamke huyo akiwa chumbani kwake alikokuwa amelala na mdogo wake wa miaka 12 na mtoto wake wa miaka minne.

Inaelezwa kuwa mwanamke huyo alichukua uamuzi wa kujichinja kwa kisu lakini mdogo wake huyo alishituka kutoka usingizini na kumpokonya silaha hiyo ndipo alipochukua chupa ya soda na kujikata koromeo papo hapo.

Akisimulia tukio hilo, Peter Maduhu ambaye ni mpangaji mwenzake alisema baada ya mdogo wake kuomba msaada kuwa dada yake amejichinja ndipo alipoamka na kutoa msaada lakini walipoingia ndani walimkuta tayari ameshajikata koromeo kwa kutumia kipande cha chupa ya soda.

Alisema kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa akilalamiaka kuwa anaumwa kwa muda mrefu ugonjwa ambao hakua akiutaja.

Aidha alisema marrehemu alikuwa akidai kuwa hakuna ndugu wala mtu wa kumsaidia licha ya kuandamawa na ugumu wa maisha.

''Marehemu alikuwa akifanya biashara ya Mama ntilie'' alisema Maduhu ''lakini siku ambayo alikuwa akitaka kujiua mdogo wake alikuwa akisema Dada yao yupo kazini''

''Kumbe amejifungia ndani na ilipofika majira hayo ya saa tisa usiku ndipo tukasikia kelele za mtu akiomba msaada na tulipofika chumbani kwake alikuwa amejikata koromeo.

Baba mzazi wa marehemu Elias Ruleja ambaye ni mkazi wa mkoani Kagera alisema mtoto wake huyo alitoroka nyumbani mwaka jana kuja kuishi Shinyanga bila ya yeye kufahamu hadi alipopokea habari za kifo chake. Alisema amahuzunishwa sana na kifo hicho huyo akiwa mtoto peke aliyekuwa amebaki baada ya kaka yake kufariki miaka mingi iliyopita.

Nipashe
 

Man Thom

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
717
1,000
Kuna wakati huna mtu wa kumshirikisha. Na kama yupo anakuwa haelewi ni nini hasa unajisikia ndani ya moyo wako.
In one way ni sawa unayoyaongea, ila tafiti zinaonesha kwamba, watu wengi wanaojitoa uhai ni wale aidha wametengwa na familia, au hawathaminiwi na jamii inayowazunguka..hawana yeyote wa kuweza kuegemea, kifupi wamekosa muelekeo wa maisha..as a result wana-commit suicide! So to me sharing is caring demi'
 

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,312
2,000
Kujua ni matokea ya ugonjwa wa akili uliokosa matibabu kwa wakati.

Mfano...depression, bipolar, schizophrenia n.k
 

MBIIRWA

JF-Expert Member
May 24, 2013
2,471
2,000
Magu ameua mtu huko Shinyanga,
Jambo la kushukuru hilo pepo halikumwelekza kuanza kuua mtoto na mdogo wake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom