Shinikizo la damu

vicent tibaijuka

JF-Expert Member
Mar 22, 2012
268
57
shinikizo la damu

Baadhi ya kesi 30 000 ya mashambulizi ya kiharusi na na magonjwa ya moyo hutokea kila mwaka hapa Tanzania, na matatizo haya yamekuwa yakiongezeka mwaka kila mwaka. Mpaka sasa hivi wakati watu wa nchi nyingine wakiwa wanaokolewa kutokana na matibabu dhabiti, ufanisi wa vitendea kazi na madawa ya kisasa, Tanzania bado tuko nyuma, na hivyo kufanya tuendelee kupoteza ndugu na jamaa zetu siku baada ya siku.
Lakini ukweli ni kwamba wengi wa watu hawa wasingekuwa wanapatwa na matatizo haya kama wanglikuwa wanajua chanzo au tatizo kubwa la magonjwa hayo, yaani shinikizo la damu. Kwa lugha ya kigeni blood pressure (BP).

Shinikizo la damu ni ugonjwa mkubwa. Leo hii inakadiriwa kuwa
mamilioni ya watanzania wanaongezeko la shinikizo la damu lakini wao hawahui kwani ugonjwa huu huja taratibu na dalili zake mali nyingi huwa hazi wazi.
Watanzania wengi hawajui kuhusu shinikizo la damu, hii ni kwa sababu hata serikali haina mkazio kwa hilo zaidi tu wamekazania magonjwa ya kuambukiza, wakati watanzania wengi hasa wa mijini wanaisha maisha kama ya nchi za ulaya magharibi, yaani kuangalia TV muda mrefu, kula vyakula vya mafuta kwa wingi, kunywa pombe kwa wingi, kutofanya mazoezi, kutembea kwa magari muda mrefu, kuona kuwa unene ni sifa, nk. Lakini pia ikumbukwe kuwa Bp inaweza pia kurithika. Kwa kweli ongezeko la shinikizo la damu ni hatari kwani huongeza hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa.
Utafiti umefanyika kwa muda mrefu, lakini bado kuna mengi ya kufanya ili kuweza kuelimisha jamii na kuokoa maisha ya wa tu.
Kwa ufupi hapa nitaelezea kuhusu jinsi moyo unanyofanya kazi na jinsi shinikizo la damu linavyo tokea na dalili zake.
MOYO. Ni kiungo kilichoko kifuani chenye ukubwa kama ngumi yako na kazi yake ni kusukuma damu sehemu mbalimbali za mwili. Moyo una vyumba vinne, viwili vya juu huitwa atrium na na vya chini huitwa ventricle. Kawaida katika kila sekunde moja moyo husinyaa ili kusukuma damu mwilini kutoka katika venticle ya kushoto kupitia mshipa wake mkuu huitwao aorta. Na kutoka katika ventricle ya kulia damu huenda katika mapafu ili ipate hewa ya oksijeni. Na baada ya hapo hutanuka ili damu kutoka kwenye mapafu na sehumu nyingine ya mwili kuingia tena. Wakati wa kusinyaa huitwa systoli na shinikizo lake ni systolic pressure, na wakati wa kutanuka huitwa diastoli, na shinikizo lake huitwa diastoli pressure. Ni kutokana na shinikizo hilo twaz jua kama mtu ana shinikizo la damu kubwa. Mabadiliko ya msukumo wa damu katika moyo hubadilika kutokana na mfumo wa nerva zilizoko katika moyo, zinaitwa sympathetic nerve na vimengenyo vingine vinavyo chochea kazi ya moyo. Mfano pombe, sigara, chai na kahawa, stress, mawazo mengi, nk. husababisha kazi ya hizi nerva kuongezeka na kuufanya moyo ufanye kazi kwa kasi huku mishipa ya mwili iksinyaa na kusababisha shinikizo la damu kuwa kubwa.
Shinikzo la damu hubadilika mara kwa mara kutokana na shughuli afanyazo mtu. Mara nyingi huwa juu wakati mtu afanyapo kazi na hupungua wakati amepumzika au amelala.
Unene husababisha shinikizo la damu kwani mafuta (cholesterol) hujaa katika misha ya damu na hivyokusababisha njia ya kuwa ndogo na hivyo kusababisha msongamno wa damu kuwa mkubwa. Kitendo hiki ni cha hatari kwani husababisha baadhi ya sehemu za mwili zisipate oxygen ya kutosha na hivyo kusababisha madhara mengine. Mfano, kama haifiki vizuri miguuni mtu hupata maumivu wakati wa kutemba hata ka si mbali. Kama haifiki kwenye figo basi figo huharibika na kusababisha BP tena kuwa zaidi, na hata kwa mwanaume mafuta yanapokuwa kwenye aora sehemu za nyonga anaweza hishiwa nguvu za kiume. ikiwa kichwani mishipa ya kichwa huweza pasuka na kwani ni miembamba mno na kufanya damu kuvilia kichwani na mtu kupata kiharusi au kufa., kama mishipa ya moyo pia itajaa mafuta huyu mtu atakuwa anapata maumivu kifuani wakati wa shughuli au hata kama kapumzika kwa oxygen haitafika katika misuri ya moyo na hiyo huweza sababisha moyo kusimama na kutofanya kazi. Kama yamejaa kwenye mshipa mkubwa wa moyo, mtu huyu atakuwa napata kizunguzungu au hata kuanguka kwani damu haifiki kichwani ya kutosha (hasa wazee), pia kwa uzeeni mtu mwenye ugonjwa wa kusahau hali ya weza kuwa mbaya zaidi.
Kawaida shinikizo la damu ni vema likawa chini ya 130/80mm Hg. Kwa wenye kisukari ni vizuri ikawa chini ya 120/80mm Hg.
Shinikizo la damu limegawanyika katia sehemu mbili, ya kwanza ni ile kwamba yenyewe iko juu bila sababu au kula chumvi nyingi, pombe, na ya pili ni kutokana na magonjwa mengine kama figo, saratani, baadhi ya vidonge vya majira, dawa za kuzuia maumivu, kortison, mabadilko ya hormoni. nk.

Dalili.

Watu wengi hawajui kwamba wao wana shinikizo la damu. Dalili kawaida si kali, lakini mara nyingi ni uchovu wa mara kwa mara, kizunguzungu, kutapika, kuwa na hasira za haraka, kichwa kuuma, macho kuanza kushindw kuona mbali, kupumua kwa tabu nk.
Njia pekee ya kujua ka unashinikizo la damu la juu ni kupima wewe mwenyewe au kwenda hospitalini ili wakuangalie. Hasa baada ya kufikisha miaka 45 ni vizuri kuwa unapima mara kwa mara. Ila kuna baadhi ya watu wana dalili ziitwazo koti nyeupe, kwani wafikapo hospitalini baada tu ya kumuona daktari pressure hupanda.Hii ina maana kwamba shinikizo la damu kuongezeka kwa sababu ya woga. Watu hawa hubidi kupima pressure wakiwa katika hali ya utulivu au nyumbani,
Vipimo vya muhimu kfanya wakati ukiwa na shinikizo la damu ni ECG, sukari ya damu, mafuta katika damu (cholesterol LDL,HDL), madini, baadhi ya homoni TSH,T4,
Magonjwa ya kisukari ni hatari sana kwani huweza sababisha mabadiliko mengi katika mwili hasa mishipa ya damu na neva hivyo kusababisha hali kuwa mbaya zaidi kwa mtu mwenye shinikizo la damu.
Lengo kuu la matibabu ya shinikizo la damu ni
kuzuia matatizo ya ugonjwa kama vile ugonjwa wa moyo, kiharusi na mengine ya moyo na mishipa ugonjwa huo. Katika yote hayo ni vizuri tubadili miongozo ya misingi yetu ya maish.msingi wa kwanza kabisa ni mabadiliko ya chakula na mazoezi ya viungo, kupunguza ulaji chumvi. Kunnywa kiasi kidogo cha pombe au kuacha kabisa, kuondoa stress, kuacha sigara nk.
Matibabu ni ya ghali sitayaandika hapa kwani itkubidi umuone daktari kwa ushauri zaidi. Dawa ni nyingi na matumizi ni tofauti na pia inategemeana na vipimo vyako vimeonekanaje. Na hata baada ya kutumia dawa lazima utekeleze masharti ya daktari.
 
Back
Top Bottom