Wakuu habari zilizopatikana ni kwamba Shimbo hakulazwa SA. Ila alipopata habari inasemekana ni kweli pressure ilimpanda, hakupelekwa SA wala Hospitali yao ile ya Lugalo, alipelekwa ile ya usalama wa taifa ili askari wasijue. Habari zaidi zinasema pesa alizokutwa nazo zinatokana na yafuatayo:
1. Serikali ya Comoro ilitoa euro milioni 180 kama shukrani kwa JWTZ yeye amekula zote bila huruma.
2. Serikali inampangia kila mwanajeshi hela ya chakula kwa mwaka. Askari wanasema wanapokwenda vitani nje ya nchi huwa hawalipwi hela hizi, zote anachukua huyu jamaa. Anafanyia nini, haijulikani.
3. Tenda zote jeshini ni za huyu jamaa, ukiacha matrekta inasemekana amewahi kupaka rangi majengo yapatayo manne huko morogoro ambayo yangegharimu hata mil 10, yeye alitumia mil 600. Mchezo huo inasemekana pia alifanya hivyo Arusha kwa mil 800.
4. Askari wanaokwenda vitani nje ya nchi kama wale Comoro, Darfur, Liberia na Lebanon inasemekana wanatakiwa kulipwa posho ya dola 1800, lakini badala yake wanalipwa dola 600 tu.
5. Askari wanaokwenda kufanya kazi ya uangalizi nje ya nchi wanatakiwa walipwe dola 10,000 lakini yeye shimbo anawakata mpaka dola 5000
6. Wanasiasa mafisadi inasemekana wanamtumia pia huyu jamaa kuhifadhi mihela yao kwa kuwa jeshi haliguswi.
6. Huyu jamaa inasemekana haguswi hata na mkuu wa majeshi jenerali Mwamunyange kwa sababu amewekwa na rais
7. Kiujumla askari inasemekana hawampendi hatta kidogo.