Mkuu habari kama hizi inafaa ziwafikie watanzania wengi. Kama uchumi unaporomoka kila kukicha watu wanwaweza kujua waht kind of administration team we have.
Najua kuna watu wanasema thamani ya shilingi si kigezo pekee cha kuonesha hali ya uchumi, lakini ni lazima tutambue pia kuwa ni kigezo muhimu. we are ruining our country, this has to stop. A shiling must appreciate and eventually become stable.
..acha zako wewe kama huelewi kaa kimya, kushuka kwa thamani ya shillings sio kushuka kwa uchumi, hope iendelee kuporomoka ili uchumi wetu uendelee kuwa imara.
Naombeni ofafanuzi angalau kiduchu hapo kwenye red...acha zako wewe kama huelewi kaa kimya, kushuka kwa thamani ya shillings sio kushuka kwa uchumi, hope iendelee kuporomoka ili uchumi wetu uendelee kuwa imara.
Koba said:..acha zako wewe kama huelewi kaa kimya, kushuka kwa thamani ya shillings sio kushuka kwa uchumi, hope iendelee kuporomoka ili uchumi wetu uendelee kuwa imara.
..acha zako wewe kama huelewi kaa kimya, kushuka kwa thamani ya shillings sio kushuka kwa uchumi, hope iendelee kuporomoka ili uchumi wetu uendelee kuwa imara.
hii shiling imeshuka kwa hiyo ni kuporomoka kwa uchumi kama shilingi ingekuwa imeshushwa na BOT kusaidia export then ungesema unavyotaka, by the way TZ ni net importers we are not china or japan ambao wana-export sana
sio kila kushuka kwa sarafu ni kuzuri inategemeana na uchumi wa nchi yako una base na nini......
acha lugha ya matusi kama vitabu vyako viko mbali jaribu hata ku google utapata uelewa zaidi
hii shiling imeshuka kwa hiyo ni kuporomoka kwa uchumi kama shilingi ingekuwa imeshushwa na BOT kusaidia export then ungesema unavyotaka, by the way TZ ni net importers we are not china or japan ambao wana-export sana
sio kila kushuka kwa sarafu ni kuzuri inategemeana na uchumi wa nchi yako una base na nini......
acha lugha ya matusi kama vitabu vyako viko mbali jaribu hata ku google utapata uelewa zaidi
Unajua haya ndio madhara ya kutumia terminologies kihasara hasara. Labda nikuulize swali ndugu Koba, je wewe unatumia kigezo au kiashiria gani kutambua hali ya uchumi? Pato la taifa? Uzalishaji wa taifa? Mgawanyo wa pato la taifa?
Kwa kuongezea na pengine kuboresha yale ya ndugu Geza Ulole, ni kweli kwamba pato la taifa limekuwa likikuwa mwaka hadi mwaka ila ukuaji wa pato hili ukililinganisha na kasi pevu ya ukuaji wa idadi ya watu na pia mfumuko wa bei, unaonekana si maridhawa kama vile wanasiasa wetu wanavyopenda kuwaambia wananchi na wale wasio na ufahamu mzuri wa misamiati ya Uchumi.
Uporomokaji huu wa nguvu ya manunuzi ya shilingi nimeshauandika hapa jamvini si chini ya mara moja.
Mkubwa Koba kuna kitu kinaitwa "fallacy of composition" na hii ni bora ukaizingatia katika mada hii. Kwa kifupi kudhania ya kwamba kama hali ya mtu mmoja ni nzuri inamaanisha hali za watu wote ni nzuri si sahihi hata kidogo.
Kwa bahati mbaya natambua ya kwamba kuna baadhi ambao kipato chao hakijakuwa vya kutosha ili kuweza kumudu maongezeko ya bei na hivyo kudumisha thamani ya manunuzi ya shilingi wanayoichuma na hawa ndio ambao wana kila haki ya kusema ya kwamba kwao wao mambo si mazuri.
Mfano hai Semilong na Bongolander ni US dollar ambayo kwa miaka michache iliyopita tangu Kichaka akiwa madarakani imekuwa ikishuka thamani karibu kila mwaka na hata mwaka huu kutokana na US kuwa na uchumi ulioanguka vibaya sana kuliko katika wakati wowote ule tangu ipate uhuru ukiondoa the big depression.
Hali hii ilisababisha nchi nyingi duniani ikiwemo China kutishia kuacha kuitumia US dollar katika manunuzi na mauzo yao katika soko la dunia.
Mkuu toka juhudi za uzazi wa mpango zikwame na kuwekwa kapuni, sasa hivi kuna population explosion na serikali haijali kabisa. Ndio maana tunaona economic growth hai-match uchumi, tragedly hakuna anayejali.
Umeongea point nzuri sana kuhusu role ya mafisadi kwenye kupuuza kuporomoka kwa thamani ya shiling. Tunaoumia ni sisi tusio na pesa nyingi, kwa fisadi nauli ya daladala hata ikpanda mara mbili hapungukiwi kitu. hata bei ya petrol na dizel ikipanda hana neno kwa kuwa ana bilions, ni sisi hohehahe ndio tunahangaika.
Uwezo wa kudhibiti, inflation ni moja kati ya mambo yanayotofautisha serikali ya Ben na JK
Mfano hai Semilong na Bongolander ni US dollar ambayo kwa miaka michache iliyopita tangu Kichaka akiwa madarakani imekuwa ikishuka thamani karibu kila mwaka na hata mwaka huu kutokana na US kuwa na uchumi ulioanguka vibaya sana kuliko katika wakati wowote ule tangu ipate uhuru ukiondoa the big depression.
Hali hii ilisababisha nchi nyingi duniani ikiwemo China kutishia kuacha kuitumia US dollar katika manunuzi na mauzo yao katika soko la dunia.
Mugabe was in same line of thinking like yours, he devalued Zim Dollar to the extent that he created milions of poor milionaires, and eventually Zimbabwe opted to use a basket of foreign currencies(Rand, USD and GBP) . So where is upuuzi and who is mpuuzi here, me or Mugabe?
....yaliyotokea kwa Mugabe (Hyperinflation) ni kwa sababu aliwafukuza wale white farmers ambao ndio walikuwa wanajaza treasury yake, na sio kweli Mugabe aliamua to devalue their money to grow the Economy,anyway still sioni sababu ya nchi kama TZ kuwa na strong currency kutokana na hali mbaya ya uchumi,kwa economy yetu we need to export more na weak currency encourage that,Chinese wanagombana kila siku na washington kwa sababu wanaiweka currency yao sooo weak ili wapate advantage in doing business,lakini mambo ya weak/strong currency ni 2 way street kwa hiyo weak/strong is not necessary good or bad
.Wakati kipimo cha uchumi (GDP) kwa kiasi kikubwa kinakubalika miongoni mwa wachumi, wachumi hadi sasa wamekuwa wakikuna vichwa vyao juu ya faida na madhara ya kuteremka kwa thamani ya ela katika GDP kwenye nchi masikini. Wachumi wanatueleza kwamba ili uchumi (GDP) ukuwe imports zinatakiwa zipunguzwe, na shilingi yetu inaposhuka thamani (aidha kwa devaluation au depreciation) moja kwa moja inapunguza imports na kwa nadharia ya uchumi hii inachochea kukuwa kwa GDP
Baadhi ya wachumi-maendeleo (development economists) wanapinga "Koba theory" wakisema kwamba (i) thamani ya shilingi ikishuka sambamba na exports GDP itapungua (ii) thamani ya shilingi ikishuka kwa muda mrefu na kiasi kikubwa (excessive devaluation) ina sabababisha contractionary effects kwasababu nchi masikini zinategemea imports kwa kiasi kikubwa, kwahiyo imports za bidhaa kama mafuta, zana za kilimo, afya na miundombinu zinapopanda bei kutokana na teremko la thamani ya shilingi zinasimamisha na kudumaza shughuli za uchumi.
Wachumi-maendeleo wanashindwa kujibu maswali kadhaa kisayansi yanayofanya "Koba theory" ikose impizani. Kwanza wanashindwa kuweka kiwango kinachokubalika cha teremko la thamani ya ela ya nchi (i.e. they fail to define excessive devaluation). Pili, wanashindwa kutueleza sababu za kiuchumi juu ya kuwapo kwa nchi masikini zenye uchumi unaokuwa na kuimarika wakati ela ya nchi husika iko chini ya thamani ya US$ au pound ya mwingereza. Tatu, wanashindwa kutueleza namna ambavyo nchi masikini kama Tz inavyoweza kukuza viwanda vyake ambavyo vitaathirika na kupungua kwa bei za imports, na jinsi nchi inavyoweza kukwepa kuwa dump la bidhaa za nje (mfano wachina wanavyotumaliza sasa hivi). Nne, kwa kipindi hiki cha uchumi wa soko huru nchi nyingi hazifanyi devaluation badala yake zinaacha soko huru kurekebisha mwenendo wa ela zao (depreciation), hivyo basi kesi ya excessive devaluation haina mshitakiwa, mshitaki wala hakimu. As such, "Koba theory" prevails.
.
Heshima mbele mkuu ila naomba nikuweke sawa katika hayo machache niliyoyaweka katika nyeusi. Kwanza sio rahisi hivyo kwamba kwa uchumi kukua ni sharti bidhaa kutoka nje zipungue. Tafadhali rejea nadharia zinazoelezea salio la malipo ya nchi (Balance of Payments) na zile akaunti mbili za malipo, PCA na Capital, na pia kijazio ama kirekebishio cha salio hili, Official Intervention/Balancing Variable. Si kweli kwamba ili uchumi ukue ni sharti uagizaji wa bidhaa kutoka nje upungue. Mifano hai ipo mingi tu kuanzia vinara kama Marekani na Uingereza na mpaka vilaza kama Tanzania na Uganda. Na vile vile pia kama unakumbuka kipindi cha "quantitative easing" kule Japan mwishoni wa miaka ya 90 na mpaka katikati ya miaka la 2000, wao walikuwa wanauza sana nje kushinda wanavyoagiza lakini ukuaji wa pato lao la taifa bado ulikuwa legelege.
Naweza nikatoa somo refu katika hili lakini ushauri wangu ni kwamba rejea tu vitabu vyako vya Uchumi na unaweza ukaanza na kile cha ngazi ya kati cha Ben Bernanke na wenzake cha "Macroeconomics, 6th Ed."
Thamani ya shilingi haina tofauti na bei ya shilingi. Kushuka au kupanda kwake hakuna uhusiano wa moja kwa moja na hali ya uchumi. Kuna viambatanisho vingine ambavyo vinafafanua athari za kushuka au kupanda kwa shilingi. Kuna baadhi ya vitu umeanisha hapo juu vinavyoleta maana lakini ukitoka katika nadharia za vitabuni na ukaingia katika hali halisi vitu hivi si "black and white" kama vile ulivyoainisha. Kuna vitu kama vikwazo vya uwezo (capacity constraints), tija/ufanisi katika uzalishaji (productivity), na uwezo wa uchumi kumeza (absorptive capabilities) vinavyoingia hapo kati na kuleta matokeo ya mwisho uliyoyataja.
Ulichoandika hapo juu si kweli hata kidogo na kama unafikiri hivyo fanya upembuzi uyakinifu katika maandiko mengi ya Uchumi. Unajua tofauti kubwa ya sayansi za jamii kama Uchumi na sayansi kamili au hesabati ni kwamba katika sayansi za jamii hakuna jibu la sahihi la moja kwa moja. Leo hii kwa kutumia taarifa X za kipindi fulani mtu A anaweza kupata jibu B lakini mtu huyu huyu au mwingine kwa kutumia taarifa X za kipindi tofauti za kile cha mwanzo anaweza kupata jibu C.
Koba hajatoa nadharia yoyote ambayo ni ngeni. Na kwa kujibu hoja yako ya kwanza, rejea nilichosema hapo juu na kwa kuongezea ni kwamba hakuna namba au kiasi ambacho ni universal cha kuelezea kushuka kwa thamani ya fedha. Kila nchi ina cha kwake na katika mambo mengi hii pia hutegemea hali halisi ya nchi husika (viwangi vya uwekezaji, uzalishaji, teknolojia, n.k)
Sidhani kama kuna haja ya kujibu hoja yako ya pili wala ya Tatu, nadhani kile kitabu cha Bernake au chochote kile cha Intermediate Macroeconomics kitakusaidia katika hilo na pia kwenye hoja ya Tatu tafadhali rejea terms zinazokubaliwa katika trade rounds mbalimbali kama zile za Uruguay na Doha za WTO na nchi washirika.
Hoja yako ya nne, inagusia exchange rate regimes ambazo kinadharia zipo za aina tatu, free float. partial float/Partial Peg aka Hybrid na Full Peg. Ukiwa katika free float inamaanisha unaliachia soko liamue na zaidi ya kuweka taratibu za jinsi soko litakavyojiendesha, uingiliaji wa wazi (revaluation) unakuwa unakinzana na dhana ya soko huria. Kwenye partially floating regimes mbona nchi bado zinaweza kuingilia kazi ya soko au haujafuatilia migogoro ya Yuan ya China na Marekani?
Mkuu, majibu mazuri na inaonyesha una idea na somo la uchumi. Kitu kimoja ambacho nadhani huna idea nacho ni kwamba kila THEORY YA UCHUMI INALINDWA na CETERIS PARIBUS. Ceteris paribus ndio funguo ya theory za uchumi, sasa huwezi kuipinga theory ya uchumi pasipo kwanza kukubali funguo. Kama unakubali Ceteris paribus majibu yako yote uliyoyatoa hayana maana, kwasababu naadharia niliyoiongelea inatokana na kukubalika kwa ceteris paribus.
Of course unaweza kubisha kila theory ya uchumi kwa kuongelea inputs ambazo hazikuwa considered, au zile ambazo zilikuwa held constant, lakini kufanya hivyo nikutoka nje ya mandhari ya theory. Daktari akikuambia meza dawa hii mara baada ya chakula, manake ceteris paribus, dawa hiyo itakuwa effective ikimezwa baada ya mlo. Sasa wewe husiseme kwamba dawa hiyo sio effective ati tu kwasababu usipomeza baada ya mlo haifanyi kazi; ilitengenezwa iwe effective kwa kumezwa baada ya mlo.
Vile vile naona unalazimisha ubishi kwa kulazimisha maneno ambayo sijayasema. Ni wapi nimesema kwamba SHARTI la kukuwa kwa uchumi ni kupunguza imports? Nisingependa niandike kitabu cha introduction to macroeconomics hapa JF chenye chapter kadhaa za inputs za GDP na kuonyesha effects za devaluations etc, na badala yake nimeandika kwa lugha inayoeleweka na mtu wakawaida. To the contrary mwenzetu umeleta lugha za vitabuni ambazo mtu wakawaida atatakiwa aende shule kwanza kabla ya kupata jibu la uhusiano wa kuteremka kwa shilingi na kukua kwa uchumi. Umeongelea balance of payment, ukaongelea terms of trade, ukaongelea aina za exchange regimes, ukaleta mambo ya productivity capacity, investment nk; haya yote ni kwania ya kuwachanganya kisonmi watu wanaotaka kujuwa uhusiano wa kuteremka kwa shilingi na kukua kwa uchumi katika lugha inayofahamika. Hata hivyo basi, hayo yote uliyoyataja hapo juu tayari yameshaingizwa kwenye "Koba theory" kwa kutumia Ceteris paribus; na ndio maana hakukuwa na haja ya kuyaongelea, kwasababu hayaongezi wala kupunguza validity ya Koba theory"
Tatizo la wasomi ni kuongea kisomi ili kuwapumbaza wasiosoma. We need to end this.