Tatizo jingine linaloweza kuua kabisa thamani ya sarafu yetu ni ufisadi uliopindukia. Si vigumu kujua kwamba ukimwaga hela yetu ya madafu mitaani kwa mabilioni kadhaa thamani ya fedha itashuka, thamani ya fedha za kigeni zitapanda na maisha kuongezeka ugumu. Hebu tafakari ni mara ngapi kumetokea "kashfa" ya wajanja flani kijichotea mabilioni? Tena chanzo cha ufisadi huo kuhusisha Benki Kuu?