Shilatu awapongeza Wananchi kuiunga mkono Serikali

Shilatu awapongeza Wananchi kuiunga mkono Serikali

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Na Mwandishi wetu, Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu amewapongeza na kuwashukuru Wananchi kata ya Miuta na maeneo yote ya Tarafa ya Mihambwe kwa kujitolea kwao kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa leo Jumapili Julai 11, 2021 wakati alipotembelea kata ya Miuta na kukuta Wananchi wakijitolea kuchimba msingi na kumwaga zege la msingi ujenzi nyumba ya daktari ambapo Gavana Shilatu alijumuika nao kuwaunga mkono.

"Serikali tunapata faraja sana tunapoona Wananchi mnaungana nasi katika kulijenga Taifa letu. Mimi ni shuhuda mnavyojitoa usiku na mchana kuhakikisha miradi inakamilika. Pongezi kwenu Wananchi na viongozi wote wa hapa Miuta na maeneo yote ndani ya Tarafa ya Mihambwe ambapo nyakati zote mmeonyesha ushirikiano kuijenga Tarafa yetu. Kwa kasi hii niliyoiona hapa natumai nyumba hii ya daktari itakamilika mapema sana, hongereni sana." Alisema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu amehaidi Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuendelea kushirikiana na Wananchi wote kuhakikisha malengo ya ukamilifu wa miradi inayolinga na thamani ya fedha yanatimia.
Screenshot_20210711-143821.jpeg
 
Kuiunga mkono serikali!!!?
Serikali inashobokea wananchi ili iungwe mkono jamani!!!? Ilipatikanaje hii serikali?

Mauzauza government.
 
Hongereni kwa kazi ya kukimbiza shughuli za maendeleo huko Tandahimba.

Usisahau kunijuza bei ya korosho ya Kangomba ikianza, baada ya kupoteza mtaji wangu huko mwaka 2018 baada ya Jeshi kusomba Korosho zetu sasa mwaka huu nataka nirudi kwa Kishindo 💪💪💪💪💪
 
Back
Top Bottom