Shida ya maji mtaani kwangu imenipatia utelezi bila kutarajia

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Na hili nalo likatazamwe kwa kina,
Kama ilivyo ada ya shida ya mgawo wa maji na umeme iliyoikumba mkoa wa Dar Es Salaam, wengine tumetumia kama fursa

Kuna mwanamke niliwahi kukutana naye njiani miezi kama mitano iliyopita nikiwa katika harakati za kuwahi kazini. Nilipokutana naye njiani tena nyakati za alfajiri nikaamua kumsemesha, hakutaka kuzungumza nami mbali na kunisonya na kuendelea na safari yake. Siku-mind kiviile, nikaamua kuyaruhusu maisha yaendelee

Mwezi September nilivuta maji hapa kwangu pamoja na kuweka tanki kubwa la maji aina ya jojo, sikuwa na lengo la kuuza, huwa nawapatia majirani ndoo tatu tatu per day ili kudumisha ujirani mwema

Ni wiki ya tatu sasa hapa mtaani kuna huduma ya mgawo wa maji, na si mtaani tu, nahisi ni janga la kimkoa, na sio mkoa tu bali ni janga la kitaifa

Hivyo kiubinadamu zaidi nikaamua kuanza kuuza maji ndoo 150 Tsh. Wakina mama ni wahanga wakubwa wa tatizo hili, hivyo hufunga safari maili kadhaa kuja kwangu kuteka maji, kutokana na foleni, huwa nakaa nao hapa nje mpaka mida ya saa nne wakisubiri maji kutokana na kipenyo kidogo cha bomba nilichonacho

Wakati sina hili wala lile, mida ya saa mbili usiku nilishtushwa na mwanamke mwenye muonekano wa aina yake, kafungasha haswa, kavalia vazi nahisi limetengenezwa kwa khanga, huku mtrako wake uliogawanyika pande mbili zilizosawa na kuacha bonde kubwa kati kati likistiliwa na kivazi kile akiwasili maeneo haya. Moyo ulipiga Pah! Nikatizama kama mke wangu ana dalili za kutoka ndani. Nilishtushwa na sauti, "Za jioni kaka yangu", "Ni nzuri, habari yako", "Safi tu","uko powa',"mh! Naweza kupata maji walau ki ndoo kidogo tu nikawapikie wanangu?". Dah! Nilihisi huruma na hisia za ajabu, ndipo kumfanyia harakati za yeye kupata ndoo 10 za maji kwa kukatiza foleni ile. Baada ya hapo nikamuomba na namba ya simu kwa lengo la kumjulisha maji kama yatakuwepo siku nyingine ili afuate

Siku kadhaa baadae wakati narejea kutoka Boma nilikutana an foleni ya aina yake pale nyumbani huku yeye akiwa nafasi ya nyuma kabisa, ndipo kuingia ndani ili kumset wife, kwa akili ya kuzaliwa nikabahatika kumtoa mwanamke yule na madumu yake 10 yakiwa na maji, kisha kumuongeza nauli ya pick up

Ngoja nitulize ubongo niandike vizuri matukio yaliyofuata...
 
Kapicha kakusindikizia uzi
Sitegemei kuulizwa kapicha
NB: From Library
images%20(3).jpg
 
Chai iliyokosa tangawizi hii
 
Alikuja usiku mwenyewe na kuna folen, ukampa madumu kumi, sasa apo hayo madumu kumi kayabebajeaf ukampa nauliz maana anakaa mbali na mtaa, apoapo amekuja na kanga kweli, au sijaelewa kidogo
 
Back
Top Bottom