Mr Someone
Member
- Sep 15, 2018
- 39
- 60
Bonjour wanaJF!
Matukio mbalimbali katika maisha huwa yanafikirisha sana. Na humfanya mwanadamu atafakari ni nini hasa kipo nyuma yake. Kwanini yanatokea. Tunaweza tukaishia kusema ni mipango ya Mungu katika matukio kama mafuriko, tsunami au matetemeko ya ardhi kama ya kule Kagera. Lakini yale ambayo unayaona kabisa ni 'kazi ya mikono yetu' hutafakarisha zaidi.
Shida na mazoea ni majina ya watu. Wapo mabinti wengi huitwa majina haya (ingawa binafsi sipendi majina yenye akisi mbaya). Lakini hapa sizungumzii watu bali ninazungumzia hali za kimaisha.
Mwaka jana mwezi mei, nilipanda 'hiace' maeneo ya mwanza. Niliipandia sehemu moja inaitwa njia panda ya mwanangwa (ni takribani km 40 kutoka mwanza mjini katika Dar-Mwz Road). Hiace hii ilikuwa ikitupeleka kijiji kimoja kiitwacho nduha.
Gari hizi kisheria zinatakiwa kubeba watu takribani 16 wakiwa wamekaa. Lakini mule tulikuwa takribani 25. Tukiwa njiani gari ilisimama kwa muda mrefu kidogo. Baadhi tulichoka kukaa ndani ya gari, hivyo tulitoka nje kwani hewa kidogo ilikuwa ni nzito (nadhani tunajua mambo ya vijijini, wanasema ukitaka kujua sehemu fulani ikoje basi watazame abiria wanaoelekea huko). Punde niliona madumu ma5 ya mafuta ya petrol yanapakiwa ndani ya hiace. Binafsi nilistushwa na hili sbb hasa ya usalama wetu. Nilimuuliza konda kwanini wanaruhusu hilo. Karibu gari zima walinishangaa kwa swali langu hilo. Walinishangaa sababu ni MAZOEA yao katika hilo. Nilipata support ya mtu mmoja tu. Finally iliamuliwa asiyetaka abaki. Nifanye nini katika mazingira ambayo hakuna usafiri wa uhakika. Kishingo upande na kwa hofu kubwa nilipanda gari lile kutokana na SHIDA ya usafiri. Mungu mkubwa tulifika salama.
Tuseme bahati mbaya gari ile ipate ajali.. HIACE YATEKETEA YAUWA ABIRIA WOTE 25.. CHANZO CHADAIWA NI PETROL.. Lawama nyingi zitakuwa kwa serikali, na mamlaka mbalimbali. Hamaki na hamasa huondoa fikra makini.
Ukitazama matukio haya, hasa kwa huku mikoani unagundua kuwa SHIDA na MAZOEA ni chanzo kikubwa cha madhila mengi yanayotufika. Wananchi wanathubutu kujazana kwenye vyombo vya usafiri sbb hawana usafiri mbadala. Sbb ya shida ya usafiri. Zipo gari zinabeba mizigo kupeleka mnadani, magunia ya mazao au nguo yanapakiwa kuliko kiasi na watu wanathubutu kukaa juu yake. MAZOEA ya kuwa miaka yote tunafanya hivi na hakuna ttz.
Mungu awarehemu waliofariki katika kivuko cha Nyerere kule ukara. Kule usafiri ni SHIDA ya muda mrefu. Hasa siku za minada hali inakuwa changamoto zaidi. Watu wanahitaji kivukisha mizigo yao, watafanyaje na hakuna njia mbadala. SHIDA ya fedha na usafiri inawafanya watu wathubutu kujaa kwenye meli na mizigo. Lakini kwanini mtu ahofie leo ajali, ikiwa ana MAZOEA ya miaka mingi kuvuka katika hali hiyo hiyo..
Mamlaka zinawajibu mkubwa wa kusimamia sheria mbalimbali za usalama, lakini tukiri waathirika wakuu katika madhila, ni sisi raia. Wananchi ambao ndio tuna SHIDA ya kutafuta fedha na usafiri na kuwa na MAZOEA ya kutumia njia zile zile hatarishi kila siku na kutufanya tujenge umahiri na kuondoa woga wa yanayoweza kujiri, ndio waathirika wakuu. Ni muhimu sisi wananchi tuwe watu wa kwanza kuchukua tahadhari kabla ya mamlaka. Ni kweli waliozidisha watu kwenye MV Nyerere tuseme watachukuliwa hatua, lakini sisi tumeshapoteza maisha tayari.
Mungu atupe busara zaidi za kutumia akili zetu kuyaongoza maisha yetu katika usalama zaidi.