Shibuda ambaye alijitoa kuwania kiti cha urais hivi karibuni kumpisha Rais Kikwete, anadaiwa kuwa katika wakati mgumu wa kuamua hatima yake kisiasa kutokana na matokeo ya kura za maoni na shinikizo jipya la kumtaka ajiunge CHADEMA.
"Kweli watu wengi wamenifuata kunishawishi nijiunge CHADEMA, lakini ni mapema mno kwa sasa maana hata matokeo kamili hatujayapata na hivi sasa ndio tunaenda wilayani kupata matokeo, lakini mimi siku zote naamini kugombana na sheikh au askofu, si kugombana na msikiti au kanisa," alisema Shibuda bila kufafanua.