Wanaosema wasanii wanaingia kwenye siasa ili kunufaika ni mtazamo tofauti kanuni na katiba ya Chama cha Mapinduzi CCM ikiwa ni mwanachama ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwahiyo mtu yoyote ana haki hiyo.
"Na sisi tumekuwa kama kundi la wasanii na watu maarufu wengi tumekuwa wanachama na makada watiifu wa CCM lakini pia wengi wetu tumekuwa tukisapoti Chama katika shughuli mbalimbali kwa hiyo tuna haki kama wanachama.
"Ndio maana wengine wameingia na wamepata nafasi kuaminiwa na chama na kuchaguliwa"- Ndugu Nurdin Bilal 'Shetta', Diwani mteule Kata ya Mchikichini kupitia Chama Cha Cha Mapinduzi CCM.