Shetani na vipaji kwa wanadamu

Shetani na vipaji kwa wanadamu

monde arabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2017
Posts
8,888
Reaction score
13,645
Habar za leo ndugu wanajukwaa,

Kwenye mada moja kwa moja;sote tunaoamini tunafaham kuwa shetani alikuwa ni malaika wa sifa huko mbinguni (alikuwa muimbaji) baadae alipotaka kuichukua nafasi ya Mungu ndipo Mungu alipokasirika na kuamua kumtupa kuzimu

Shetani alipofika kuzimu akaanza kufanya kazi kijanja na kwaakili nyingi sana kwa kupandkiza vipaji vibaya kwa wanadamu,mfano wa vipaji anavyowapandkizia wanadamu ni pamoja na hivi;

1.Uongo

2.Usinzi

4.Ulevi

5.Ulafi (ikiwa ni pamoja na kutaka kumiliki vitu vingi pekee yako)

6.Usingiziaji

7.Hasira

8.kutokusamehe

9.Kutukana

10.Ugomvi

11.Kutokutaka suluhu

12.Kutokuwapenda watu bila sababu za msingi

13.Kuwashuhudia watu uongo
Nb:kila mwanadamu kuna mahali shetani amempa kitengo,hakuna mwanadamu ambaye shetani hajampa kitengo

Swali la msingi;je,wewe shetani amekupa kitengo gani ili tuanze kuombeana kuanzia hivi sasa?
 
Ndo hivo kwa hiyo daima ukikutana na zuri mshukuru Mungu
Na ukikutana na baya jilaumu mwenyewe.
 
Huenda shetani alifanya mapinduzi mbinguni na kimpindua Mungu !'mbona mafanikio makubwa hapa duniani ni ya shetani ?
 
Dunia ya sasa hivi ilivyo, kila anachopanga shetani kufanya kesho, anajikuta binaadamu washakifanya toka juzi.

Tena kuna dhambi mpya mpya ambazo sisi binaadamu ndio tumemfundisha yeye, alikua hazijui.
 
Je tukiombeana si hiyo kauli yako kila binadamu shetani amempa kitengo itakuwa batili?tumepewa au tumejipa?
 
duuuh shetani alikuwa muimba kwaya ndo kwanza nasikia kwako[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom