Sheria ya taflisi

TanzaniaLaw

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
1,298
482
[h=3]SHERIA YA TAFLISI[/h][h=3]1.TAFLISI MAANA YAKE NINI?[/h]Tanzania kama nchi nyingine duniani,uwekezaji/ujasilimali na ukopaji wa benki au taasisi za fedha umekuwa ukiongezeka na biashara zimekuwa zikianzishwa na watu binafsi au kwa Ushirika.Asilimia kubwa ya watanzania wamekuwa wakijiajiri wenyewe hasa baada ya ajira za serikali kuwa ngumu.Vile vile ahadi ya serikali kutoa shilingi bilioni mija imehamasisha ufunguaji wa biashara za aina mbali mbali.Lakini hakuna hakika kama biashara hizo zinaweza kudumu kwa zaidi ya miaka mitano mpaka kumi.Mara nyingi biashara hizo huanguka kutokana na ukosefu wa elimu ya biashara na kuzifanya ziangukie madeni makubwa na kukaribisha mlolongo wa kesi mbalimbali zikiwamo za kutaka kuwafilisi.Taflisi ni mashauri ambayo yanafunguliwa pale ambapo mdaiwa hawezi kulipa madenia yake au pale mtu ambaye anamdai hajatimiliziwa deni lake,hivyo basi katika mazingira hayo mali zake huchukuliwa na kugawanywa kwa watu wanaomdai.


Ni tangazo rasmi la kisheria la kutokuwa na uwezo wa kulipa madeni.Hii inatokeapale madeni yanapokuwa makubwa kuliko mtaji.


Kuna sheria mbili zinazoonyesha utaratibu wa kufanya mambo endapo suala la kutokuluoa madeni linajitokeza.Kuna hili suala la makampuni kushindwa kulipa madeni.Hili mahala pake ni kwenya sheria ya makampuni.Hivyo basi kama unaidai kampuni na unataka ilazimishwe kulipa madeni kwa namna inayofanana na kufilisiwa,njia muafaka ni kufuata sheria ya makampuni.Lakini linapokuja suala la watu binafsi,washirika wa biashara[partnership]na vyombo ambavyo si makampuni,basi sheria muafaka ni sheria ya Taflisi

Read more »
 
Back
Top Bottom