Sheria ya 'Notification' ya Traffic Ikoje?

Truth Matters

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
2,633
Reaction score
5,606
Wakuu,
Naomba kufahamishwa utaratibu wa kisheria juu ya hiki kitu kinachoitwa 'notification' ambacho polisi wa traffic hukuandikia wakikubaini na kosa.
  1. Napaswa kulipa hapo kwa hapo? Je polisi anapaswa kunipa documents zipi? Notification yenyewe na risiti au notification peke yake?
  2. Napaswa kwenda kituo cha polisi kulipa?
  3. Kama jibu ni 2 hapo juu, kama sikuenda, polisi watanipataje tena? wana-active system ya ku-track?
 
Ni notification, na hata ukiisoma hupaswi kulipia pale lakini kwa kuwa hakuna mfumo wa kuweza kuku-track wanalazimika kukudai uwalipe palepale au wanaweza kukudai uache driving license au kadi ya gari.
 
Kwa uelewa wangu mdogo kama hela unayo unalipa hapohapo na ikiwa ni ndani ya muda wa serikali kwa maana ya uwepo wa wahasibu ofisini unatakiwa upewe na risti kama muda wa wahasibu kuwepo ofisini umeisha basi utachukua risti siku nyingne na ww utaondoka na ile karatasi ya notification kama ni gari utaacha kadi na leseni kama ni pkpk utaiacha yenyewe,nawasilisha hoja
 
Malipo yoyoyte halali ya serikali lazima yaambatane na risiti halali ya serikali. Kwa hiyo basi kama amekupa notification na hana risiti na anajua unajua anatakiwa akupe risiti atakwambie mwende kituoni ukalipe. Otherwise kuna traffic police huwa wana risiti ya serikali na wanakukatia palepale. Ukipewa 'notification' ukalipa bila kupewa risiti ni sawa na kumpa hela bure trafick.
 
Wakuu,
Naomba kufahamishwa utaratibu wa kisheria juu ya hiki kitu kinachoitwa 'notification' ambacho polisi wa traffic hukuandikia wakikubaini na kosa.
  1. Napaswa kulipa hapo kwa hapo? Je polisi anapaswa kunipa documents zipi? Notification yenyewe na risiti au notification peke yake?
  2. Napaswa kwenda kituo cha polisi kulipa?
  3. Kama jibu ni 2 hapo juu, kama sikuenda, polisi watanipataje tena? wana-active system ya ku-track?

Polis wakikutana na mimi barabarani wananikimbia 1 nakataa kosa na hawezi kuniandikia mpaka mahakama inikute na kosa 2 polis hana mamlaka ya kukutonza fain barabarani 3 sababu polis wengi kichwani zero na wakijua unajua sheria hawataki tabu watakuwachia tu
 
Malipo yoyoyte halali ya serikali lazima yaambatane na risiti halali ya serikali. Kwa hiyo basi kama amekupa notification na hana risiti na anajua unajua anatakiwa akupe risiti atakwambie mwende kituoni ukalipe. Otherwise kuna traffic police huwa wana risiti ya serikali na wanakukatia palepale. Ukipewa 'notification' ukalipa bila kupewa risiti ni sawa na kumpa hela bure trafick.

Kumbeeee
 
Ni notification, na hata ukiisoma hupaswi kulipia pale lakini kwa kuwa hakuna mfumo wa kuweza kuku-track wanalazimika kukudai uwalipe palepale au wanaweza kukudai uache driving license au kadi ya gari.
Mkuu umechemka sana.... hairuhusiwi kuacha Driving Licence wala kadi ya Gari... hivyo ni mali yako na ya Gari tu... unachotakiwa ni kuongozana na huyo Police hadi kituoni ukalipie fine vingine ni wizi mtupu unaoendelea
 
Back
Top Bottom