Sheria ya manunuzi ya umma ifanyiwe mapitio haraka kunuru fedha za Elimu

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,961
4,245
Moja ya kitu kinachawaumiza vichwa Wakuu wengi wa shule kwa sasa ni namna ya kukidhi mahitaji ya shule.
Bei za baadhi ya bidhaa baina ya soko na mzabuni ni kama ifuatavyo:
1. Mafuta taa lita moja sokoni ni Tsh. 1,600; bei ya mzabuni ni Tsh. 3,000
2. Madumu tupu lita tano bei ya soko ni Tsh. 1,500; bei ya mzabuni ni Tsh. 5,000.
3. Mpira wa miguu bei ya soko Tsh. 9,000; bei ya mzabuni ni Tsh. 120,000.
4. Sare za wasichana za michezo bei ya soko Tsh. 200,000; bei ya mzabuni Tsh. 450,000.
5. Kutoa mjini nakala moja Tsh. 50; bei ya mzabuni Tsh. 200.
Hiyo ni mifano michache inayoonyesha jinsi fedha za umma 'zinavyotumbuliwa' na wajanja kwa kigezo cha sheria ya manunuzi.
Miaka ya nyuma serikali ilikuwa inawakopa hao wazabuni, ila kwa sasa Wakuu wa shule wanatoa fedha taslimu. Je kuna haja gani ya kulipia bei zaidi ya bei ya soko?
Ikishindikana kubadili sheria nzima ni vyema serikali ikatoa waraka elekezi kuwaruhusu Wakuu wa shule kununua bidhaa kadiri ya bei ya soko.
 
Kurekebisha sheria ya manunuzi ni sahihi kabisa ila bei haitabadilika, hiyo bei wazabuni hua wanajumlisha na mabadiliko ya uchumi, kupanda au kushuka thamani ya shilingi namaanisha mfumuko wa bei.

Ukitaka bei ya mzabuni iwe sawa na ya mtaani basi taasisi za umma zinunue mahitaji yao cash, mzabuni analeta analipwa hapo hapo, sio ulete leo mzigo wa 30,000 uje kulipwa mwezi wa 9 30,000,hiyo hela haitaweza kununua tena mzigo ule wa kwanza unaweza kupata robo ya mzigo au hata usipate kabisa maana bei itakua imebadilika sana..

Kusuhu bei hakuna kubadilika ila sheria inabidi ibadilishwe ina ujinga mwingi sana.
 
Mchango wako upo sahihi.
Kwa kipindi hiki ni bora ukatolewa hata waraka, kama inawezekana kadiri ya kanuni, ili serikali iokoe fedha nyingi zinazolipwa moja kwa moja kwa wazabuni. Ikiwa kama mzabuni hayupo tayari kuuza bidhaa husika kadiri ya bei ya soko kwa ofisa wa werikali anayetoa fedha taslimu, basi ofisa huyo awe huru kuchagua dula lingine ili apate bidhaa husika.
Naamini kabisa ikifanyika tathmini ya kina itagundulika kuwa serikali inajipatisha hasara kubwa sana kwa kununua bidhaa hasa za shule toka kwa wazabuni waotoza hata mara tatu ya bei ya soko.
 
Back
Top Bottom