Sheria ya kuwabana manabii na mitume kutungwa

Kutokana na ujanja kuzidi kwenye taasisi hizi za dini na baadhi ya watu kugeuza biashara,sheria ya kuwabana manabii na mitume ipo mbio kutungwa ili kuleta udhibiti kwa wale wote wasio na nia njema.
kwa ujumla hiii sheria itungwe wamekua chanzo cha migogoro mingi sana, yaan bora hats waganga was kienyeji. kuna wengine hata siio mapasta ila ndo wamejipachika upasta ikibid watajwe humu kabisa
 
Mmi nadhani ni wazo zuri maana huo ni wajibu wa serikali. Ila naona wangelipa kodi tu vizuri ili viwe vyanzo vya mapato serikalini viongezeke. Na pia kama Yesu mwenyewe alilipa kodi kwann wao wasilipe? Hii ingewapa hata wao nguvu ya kuibana serikali ktk baadhi ya mambo tofauti na ilivyo sasa. Elimu zao zijulikane na mapato yao pia nni wafanye na nni wasifanye
 
Hivi kumbe Yesu naye alilipa kodi? Tusaidie na kifungu kabisa tuongeze ufahamu.
 
Kutokana na ujanja kuzidi kwenye taasisi hizi za dini na baadhi ya watu kugeuza biashara,sheria ya kuwabana manabii na mitume ipo mbio kutungwa ili kuleta udhibiti kwa wale wote wasio na nia njema.
hiyo sheria ianze kwanza kuthibitisha utume wa kina mo kabla ya wengine wote.
 
kuna jamaa anaitwa ustadh Shabani yupo Bunju B,ni jamaa yangu amejifunza kuhubiri miezi 6 na sasahivi ni mtume anakanisa na anapesa za kutosha.huwa namuuliza kuhusu uwamuzi wake nae anadai imani ya mtu anaijua mungu tu.
 
Watunge tu sheria za kuwabana hapa duniani,lakini mwenye mamlaka ya kuleta Mitume ailikwishamaliza utaratibu wa kuleta mitume duniani tangu karne ya saba.Sasa hawa wanaoibuka baada ya hapo watakua na kesi ya kujibu kwamba nani aliwapa na ni wapi walikoupata huo Utume.Na nani aliyewaagiza kuja kutafuta utajiri badala ya kuwaongoza watu katika njia iliyonyooka.
 
Kutokana na ujanja kuzidi kwenye taasisi hizi za dini na baadhi ya watu kugeuza biashara,sheria ya kuwabana manabii na mitume ipo mbio kutungwa ili kuleta udhibiti kwa wale wote wasio na nia njema.

Nia njema ya masuala ya rohoni unaipima kwa kutumia elimu gani? Na mitume na manabii wamefanya biashara gani haramu kama hoja inavyodai? Nani mlalamikaji na ameathirikaje? Kama kuna mtu anafanya kinyume na Agizo la Imani ile, waaathirika wakimpeleka mahakamani kwa kosa hilo kama liko dhahiri hatahukumiwa?

Ninaoan hii serikali sasa imelewa inataka kuanza kuwafundisha watu MASUALA YA IMANI NA NAMNA YA KUABUDU.

Ninashangaa ni kwa nini srikali inatafuta matatizo na raia wakati tayari inayomengi yaliyo juu ya uwezo wake. Ningefurahi kama ningesikia wanaanza na upatikanaji wa katiba mpya ya wananchi si ya chenge. Ningerurahi wangeanzana wezi wa escrow na waliobebea fedha za lumbesa kutoka stanbic..

Watumiaji wabaya wa madaraka na wenzi wa raslimali za umma.

Bado sijasikia hatua gani srikali iinapanga kuchukua dhidi ya jecha na wahuni wenzake waliovuruga matangazo ya uchaguzi zanzibar na kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
 
Hivi kumbe Yesu naye alilipa kodi? Tusaidie na kifungu kabisa tuongeze ufahamu.
soma mathayo 17:24-27 inasema hivi:

Walipofika Kafarnaumu watu wenye kukusanya fedha ya zaka ya Hekalu walimwendea Petro, wakamwuliza, "Je, mwalimu wenu hulipa fedha ya zaka?" 25 Petro akajibu, "Naam, hulipa." Basi, Petro alipoingia ndani ya nyumba, kabla hata hajasema neno, Yesu akamwuliza, "Simoni, wewe unaonaje? Wafalme wa dunia hukusanya ushuru au kodi kutoka kwa kina nani? Kutoka kwa wananchi ama kutoka kwa wageni?" 26 Petro akajibu, "Kutoka kwa wageni." Yesu akamwambia, "Haya basi, wananchi hawahusiki. 27 Lakini kusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupe ndoana; chukua samaki wa kwanza atakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani utakuta fedha taslimu ya zaka. Ichukue ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako."
 
Hivi zaka sikuhizi ni kodi?
Ndio maana nimejua kwanini watu hawatoi zaka!
 
Kule kny wanatozwa kodi,na no lazima uwe na waumini wasiopungua 500,ndio uanzishe church yako
 
Litakuwa jambo jema sana.Jamaa hawa wanatumia ujinga wa Watanzania kuwaibia.Tatizo sasa litakuwa kujua yupi ni nabii fake na yupi ni genuine,kwa kuwa hii inahitaji spiritual eyes.
Uzi wako umenikumbusha Babu wa Loliondo.That episode proved how stupid and spiritually bankrupt Tanzanians are.Hata viongozi wa juu kabisa wa nchi walichotwa na upumbavu ule.Very shameful.

Back
Top Bottom