Sheria ya kudhibiti maandamano yaja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya kudhibiti maandamano yaja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Jul 30, 2011.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]
  KAULI za kuendelea na maandamamo mpaka kieleweke ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa Chadema zinaonekana kuikera Serikali na sasa inakusudia kuifanyia marekebisho sheria husika ili kuyadhibiti.Maandamano ni miongoni mwa mambo ambayo yalitawala mjadala wa siku mbili bungeni wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, iliyowasilishwa juzi na Waziri Shamsi Vuai Nahodha.

  Akichangia hotuba hiyo jana kabla ya kuahirishwa kwa Bunge kwa ajili ya mapumziko, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema mabadiliko hayo ya sheria yatalenga kuzuia bughudha katika maeneo ambayo watu hawashiriki maandamano husika.

  "Tunadhani kuna haja ya kurekebisha sheria ili kuregulate (kudhibiti) maandamano katika maeneo ambayo watu si washiriki wa maandamano hayo, hili linawezekana maana nchi kama Ujerumani wamefanya hili," alisema Werema na kuongeza:

  "Nimesikia hapa kauli mbalimbali zinazohamasisha maandamano na wengine wanasema tutaandamana mpaka kieleweke na wengine wanasema kutoka Mwanza mpaka Dar es Salaam, tunasema ndiyo ni haki ya kisheria, lakini lazima tuzingatie kwamba wapo wasiopenda maandamano haya."

  Kadhalika, Werema alitumia nafasi hiyo kutoa somo kwa wabunge kuhusu mivutano iliyotokea bungeni siku chache zilizopita: “Peaneni nafasi kwa kila mtu na mwenzake na muwe na ushirikiano kama ambavyo mikono ya kushoto na kulia inakuwa na ushirikiano mzuri.”

  Jaji Werema aliwaambia wabunge kuwa kazi ya kuwakilisha wananchi inahitaji uvumilivu kuliko kazi nyingine na akawataka wabunge wa pande zote kutumia lugha za kistaarabu wanapo kuwa ndani ya ukumbi wa bunge.

  Hata hivyo, alikemea tabia za baadhi ya wabunge kutumia lugha za maneno makali akitolea mfano wa hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi... “Ni kweli Mheshimiwa Lema (Godbless) alitumia lugha kali kidogo.
  Hapa naomba ifahamike hivyo, lakini yote mimi ambaye ni Mwanasheria wa Serikali nasema muendelee kuvumiliana na kuangalia lugha za kutumia. Namshukuru sana Mheshimiwa Lukuvi (William), katika hotuba ile alitaka kusimama amzuie Lema, lakini nikamwabia muache aendelee kwani kuna njia nyingi za kuzungumzia hivyo akimaliza utaomba mwongozo.’’

  Alisema kuwa katika suala lile yeye (Werema) akiwa Mwanasheria Mkuu, ndiye mwenye dhamana ya kulisemea jambo hilo.

  Chanzo: mwananchi

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Lukuvi wakati anaomba mwongozo/anahutubia baada ya Lema kusoma hoja za kambi ya upinzania alisema hivi: 'Tulikata' asome yote ili wananchi wayasikie". Kwangu mimi swali lilikuwa kwenye 'Tulitaka' - nani hao?

  Sasa napata picha kwamba Lukuvi alipopata copy ya speech ya Lema alienda kwa Mwanasheria Mkuu na 'wakapanga' akae kimya, huku Ndugai akipewa jukumu la kuhakikisha paragraph moja haisomwi. Pia wakakubaliana leo mwanasheria atumie kofia yake ili kutishia wawakilishi halali wa wananchi bungeni! kwangu hii ni sawa na State Intimidation. Nimeuliza maswali kuhusiana na hii issue kwenye thread nyingine naomba niulize tena:

  1.Mwanasheria mkuu anapata wapi mamlaka ya kutishia wawakilishi wa wananchi? Inakuwaje mwanasheria mkuu anasimama bungeni na kuhutubia wabunge huku akiwafundisha kazi? Nini maoni ya Werema kuhusu report ya kituo cha haki za binadamu na ile ya East Africa Bribery Index?

  2. Mbona mwanasheria hakusimama kusema kama askari polisi wanaruhusiwa kuuwa raia bila idhini ya mahakama? Kwa mfano, mwaka huu wameuliwa watu Nyamongo- North Mara kwa kufyatuliwa rasasi na askari polisi. Mara baada ya mauaji Naibu waziri wa mambo ya ndani alisikika kupitia vyombo vya habari akisema walikuwa wavamizi. Hata hivyo serikali ilitaka kulipa fidia kwa marehemu kabla hata ya uchunguzi! Kwa nini mwanasheria mkuu huyu hakutoa kauli kama kweli sheria inaruhusu serikali kufidia 'wahalifu'? Hadi leo hii Mwanasheria mkuu hajasema chochote kwa watanzania kuhusu utumiaji wa silaha za moto unaofanywa na polisi, mauaji na hata watu kupata vilema vya maisha kutoka kwa polisi. Kati ya maandamano ya amani na mauaji ya raia wasio na hatia nini kikubwa? Kwa Bahati Werema anatoka Mara, kwa nini asiende kuwaona wazazi/ndugu wa marehemu wa Nyamongo na awaambie kuwa walikuwa ni 'wavamizi' hivyo polisi hawakutenda kosa?

  Kule Arusha watu wameuliwa na askari polisi, Werema anasema nini kuhusu hilo?

  Hivi kuna uhalali gani wa kuwa mwanasheria anayesimamia na 'kutoa support' kwa wakiukaji wa haki za binadamu? Mwanasheria mkuu wa zamani Andrew Chenge alitumia utaalam wake na kupindisha mikataba mikubwa na matokeo yake tumeona, madini, rada. Sasa Werema anaonekana kutumia utaalam wake kukandamiza haki za binadamu? Ni mwanasheria gani huyu anayekaa kimya wakati watu wanauliwa bila hatia?
   
 3. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #3
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Ukiona taifa linazidi kuongeza sheria na kuminya haki za watu wake,basi ni dalili na ishara ya anguko la taifa husika,anachosema Werema ni mwendawazimu pekee anayeweza kutoa mawazo kama hayo.Kwa kadri watakavyominya uhuru wwetu ndivyo chuki dhidi yao itakavyoongezeka,na watawala hawataki kuambiwa ukweli eti lugha kali,hakika ukweli na haki vitashinda
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Mkuu! Naunga hoja mkono.
   
 5. A

  Alakara Armamasitai Verified User

  #5
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  bravo chadema upuuzi wanaongeya na kujifanya kukandamiza uhuru na haki za binadamu hakika tutashinda zote kama alivyosema nanyaro ephata hatuwezi kukubali waendeleze ukiritimba huu.
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mkishafunga milango yote ya demokrasia kwa kudhani kuwa nchi hii ni mali yetu kwahiyo mna haki ya kutawala jinsi mtakavyo basi tutakuwa hatuna jinsi isipokuwa ku re create ARAB SPRING ndani ya Tanzania. Hivi kwanini nyie viongozi wa ccm hamjifunzi kutoka kwa wenzenu wa Tunisia na Misri ???. wakati dunia nzima watu wanafikiria namna ya kuboresha demokrasia nyie mnafikiria namna ya ku limit demokrasia sawa fanyeni hayo halafu mutaona.
   
 7. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kutungwa kwa sheria ya kudhibiti maandamano ni kinyume na haki za binadamu, hapo nauhakika wataweka maprocedures mengi yakubana wananchi. then kama serikali itatunga sheria hii ni dhahiri itaonyesha udhaifu wake kiutendaji hususani katika vipaumbele! Haiwezekani washindwe tunga sheria ya kudhibiti mafisadi wakubwa na viongozi wenye kiburi then utunge ya maandamano!
   
 8. w

  woyowoyo Senior Member

  #8
  Jul 30, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 173
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbunge Lusinde wa mtera ameiomba serikali kuachia maandamano akichangia hutuba ya wizara ya mambo ya ndani kuwaacha wanao andamana huenda wanafanya mazoezi kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa kisukari.
   
 9. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,176
  Likes Received: 1,177
  Trophy Points: 280
  Fikra nyepesi.
   
 10. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  mie kila akisimama magamba pale naona ni kilaza tu...Werema kilaza...Lukuvi kilaza...Ndugai kilaza....wooote vilaza ila profesa wao ni Lusinde.
   
 11. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli nilishangaa sana Ndugai alipomwambia Lema kuwa hiyo haitawekwa kwenye hansard. Ni demokrasia gani hiyo ya spika kumpangia mtoa hoja mpinzani wake kitu cha kuongelea!
   
 12. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo marekebisho ya sheria pia tutaandamana kuyapinga mpaka kieleweke hawa sio wa kutuchezea kabisa..huku tukisubiria jamvi jingine la live...al jazeera tutakesha kwenye viwanja mpaka kieleweke..
   
 13. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  serikali ina mpango wa kupeleka sheria mpya ya maandamano ili kukabiliana na wale wenye lengo baya wanaotaka kuleta machafuko kupitia maandamano, habari nilizo zipata kupitia chanzo changu cha habari ni kuwa sheria hiyo itakuwa ikitamka kiwango cha umbali kwa maandamano yoyote kuwa ni lazima yaanzie na 150km na waandamaji watajiorozesha majina yao police, endapo hawatamaliza 150km watakabiliwa na kifungo kisichozidi miezi 6, hii kazi kweli kweli.
   
 14. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Kisu kimegusa mfupa! Maandamano ndo jibu.
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hahahahahaaaaa,,,,,,,,,,UKOLONI IZ BACK,JE YALE MAANDAMNO YA HISAN YA SERIKALI NA VYAMA VYA KIRAIA YATAITWAJEEEEEE,,,,,,,,?????
  <br />
  <br />
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  sheria yoyote lazima ipitie kwa wadau kabla haijapitishwa, na hakuna mdau atakayekubali upumbavu huo
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  si walishasema alinyimwa elimu na ccm? kweli wabunge wa magamba wanashida sana
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  kwahiyo anawatukana hata wapiga kura kuwa wana umwa kisukari? ngoja aone kitakachotokea huko
   
 19. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Chanzo chako cha Habari Gani tena wakati hata Heading ni Ya Gazeti la Mwananchi la Leo!Sema Source Mwananchi
   
 20. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Huyu ndiye mtaalamu na mshauri mkuu wa serikali kuhusu maswala ya kisheria inaelekea naye ameanza kujijenga kisiasa keshokutwa utamkuta anagombea ubunge kwa tiketi ya magamba.

  Badala yakuboresha uhuru na haki ya msingi ya watu kujieleza anapanga kuwawekea gavana nakumbuka Nyerere aliwambia kuwa kila kukicha sheria nzuri mnaona zinawakela na mnataka kuzibadilisha kwa manufaa ya mtu watu au kikundi je mtabadilisha sheria ngapi?.

  Hapa tatizo sio sheria ila jinsi serikali ilivyoona mwitikio na amasa waliyokuwa nayo watanzania wakahofia na yalitokea Misri na Tunisia wakaona eventually nao wanaweza kuondoka hivyohivyo.

  Miaka yote maandamano yalikuwepo na kila yana sababu na maudhui yake kwa hiyo haiwezekani watu wote wakawa wanayapenda, cha msingi ni polisi kuratibu na kuhakikisha yanafanyika kwa amani lakini sio wao kusababisha vurugu katika maandamano ya amani.
   
Loading...