kunena
JF-Expert Member
- Nov 29, 2016
- 506
- 719
Umoja wa waandishi wa habari mkoani Arusha umeipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh John Pombe Magufuli kwa kuupitisha muswada wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 kwani utaleta heshima kwa tasnia ya habari nchini.
"At least sasa sheria hii inamtambua mwandishi ni nani kwani fani hii imevamiwa" alinukuliwa mwenyekiti wa Arusha Press Club Ndg Cloud Gwando wakati wa kongamano la waandishi wa habari na sekretarieti ya mkoa kufanya tathmini ya mafanikio na changamoto kwa kipindi cha nusu mwaka Juni -Desemba 2016.
Pia waandishi hao wamemshukuru mkuu wa mkoa Ndg Mrisho Gambo kwa kutambua mchango wa waandishi kwa maendeleo ya mkoa kiujumla, ambapo Mh Gambo aliwaasa waandishi wafanye kazi zao kwa weledi na kutanguliza uzalendo mbele kwa kuandika habari ambazo zitaonyesha vipaumbele gani serikali ivifanyie kazi kwa maslahi mapana ya taifa.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Ndg Mrisho Gambo
Mwenyekiti wa Arusha Press Club Ndg Cloud Gwando akitoa hotuba ya waandishi wa habari mkoani Arusha
Mmoja wa waandishi akichangia mada katika kongamano hilo
Picha ya pamoja, mkuu wa mkoa wa Arusha,sekreteriet ya mkoa,mkurugenzi wa Jiji la Arusha na wadau wa habari mkoa wa Arusha.