Sheria inasemaje timu kumchezesha mchezaji mwenye kadi za njano 3?

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Wadau naomba kujulishwa iwapo mchezaji ana kadi 3 Na timu ikaendelea kumchezesha Na hakuna timu iliyolalamika Sheria inasemaje?
 
Wajuzi wa mambo ya soka inakuwaje iwapo timu itamchezesha mchezaji wake mwenye kadi 3 za njano huku ikijua?
 
Kwa ilichofanya tff ni sawa na kuzipa kazi klabu pinzani kuweka rekodi ya kadi za wapinzani wao wakati hiyo si kazi yao.

Ligi iliyopita Azam alinyang'anywa pointi kwa kosa hilo ikiwa imepita miezzi mitatu tena bila klabu waliyocheza nayo kulalamika. Je, hii sio double standards!?
 
Mkuu Achana Nalo Hilo Takataka linaloitwa jamal malinzi..
Linaleta mahaba yake ya kuipenda yanga hadi kwenye maslahi ya soka la taifa
 
Ata polisi walipo kata rufaa dhidi ya Simba kuchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano Polisi waliambiwa kadi za FA na ligi haziingiliani, alafu wakaambiwa wamekata rufaa nje ya muda na wamekata rufaa bila ada ya rufaa kwahiyo rufaa yao ilitupiliwa mbali.
Leo imebainika Simba wamekata rufaa dhidi ya Kagera nje ya muda na hawakulipa ada ya rufaa.

Sasa ilikuwaje kamati ya saa 72 isikilize rufaa ya Simba iliyokatwa nje ya muda tena bila ada ya rufaa?

Kwa maana iyo yaliyo wakuta Simba ndio yaliyo wakuta Polisi kwenye FA.
 
Hawa jamaa wapuuzi kweli yaani ,,wao wanavunja sheria halafu wanataka sheria ziwe zinafuatwa...

waache ujinga wacheze soka kiwanjani.
 
Kwa ilichofanya tff ni sawa na kuzipa kazi klabu pinzani kuweka rekodi ya kadi za wapinzani wao wakati hiyo si kazi yao.

Ligi iliyopita Azam alinyang'anywa pointi kwa kosa hilo ikiwa imepita miezzi mitatu tena bila klabu waliyocheza nayo kulalamika. Je, hii sio double standards!?
Lengo la TFF ni simba asiwe bingwa for any means
 
Hivi Simba angekua na point za kutosha kuchukua ubingwa nini kingemzuia? Wacheze mpira point ziko uwanjani, hili la kusubiria points mezani tena baada ya kufungwa ni aibu kwa timu kama Simba. Wajipange kwa msimu ujao, timu iwe bora, watachukua tu.
 
Team ya wahaya, rais wa TFF muhaya, unategemea kuna mpira hapo zaidi ya kuimba nyimbo za ccm
Sasa huko ni kutapatapa mkuu. Mnatakiwa muwaadabishe kiongozi wenu pamoja Na wachezaji wenu, ndiyo kwenye makosa. Ila habari ya kuingia makabila hiyo ni ya kijinga kabisa.
 
Hivi Simba angekua na point za kutosha kuchukua ubingwa nini kingemzuia? Wacheze mpira point ziko uwanjani, hili la kusubiria points mezani tena baada ya kufungwa ni aibu kwa timu kama Simba. Wajipange kwa msimu ujao, timu iwe bora, watachukua tu.
Hakuna kitu kingemzuia,LAKINI haihalalishi haramu kuwa halali!
Kwamba hata timu ikimchezesha mchezaji mwenye kadi nyekundu halafu baadae ikithibitika,basi hakuna shida as long walalamikaji walichelewa! Hii sheria ya wapi hii. Na kama sheria ya TFF inaruhusu mapungufu hayo,ni sheria mbovu kabisa!
 
Wadau naomba kujulishwa iwapo mchezaji ana kadi 3 Na timu ikaendelea kumchezesha Na hakuna timu iliyolalamika Sheria inasemaje?

Kwa mujibu wa TFF ya Malinzi inabidi wajumbe wapige kura na kumuuliza mchezaji kama kweli ana kadi 3 au la! Ushahidi wa mchezaji na kura ndio zitaamua kwa kipindi husika!!!
 
Back
Top Bottom