Sherehekea ukijua hili!

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2016
Posts
2,111
Reaction score
1,494
Swala la Yesu kuzaliwa liko wazi Kwa Kila mtu, Yesu alizaliwa (Luka 1:26...) inaitwa incarnation ,hapa Waislamu mtanisamehee! Yohana 1:14.....15, Neno akafanyika mwili, akakaa kwetu nasi tukaona utukufu, Wa Baba!!!
Swali ni kweli birth day ya Yesu ni December 25? Huu mpango umepotoshwa!!!

Katika kitabu cha Mwanzo 10:8 tunakuta habari za mtu mmoja maarufu kwa jina anaitwa Nimrod alikuwa mtu maarufu sana katika zama zake. Tena alikua mfalme wa kwanza wa kibinadamu katika Biblia. Nimrod ananenwa kuwa mtu hodari, katika Mwanzo 10:8-12, mwanzo wa ufalme wake ni babeli; Ereku, Akadi, Kalne, Ashuru, akajenga ninawi na Rehobothiri, Kala na kati ya ninawi na Kalanago ilikuwa ni miji mikubwa. Mke wa Nimrod aliitwa Shemiramis.

Kuzaliwa kwa Tammuz, tarehe 24 kuamkia 25 mwezi wa 12 kuliambatana na sherehe iliyofanyika kwa kuzaliwa kwa mtoto Tammuz, Yeremia 7:17- Leo imegeuzwa kuwa ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa YESU Kristo Mwana wa MUNGU jambo ambalo siyo sahihi. Kilicho badilika hapa ni badala ya kutumia jina la Tammuz wamebandika jina la YESU huku wakiendelea na matendo yao maovu hasa katika siku hiyo.

Katika asubuhi ya tarehe 25/12…ilikuwa ni sherehe kubwa sana ya kuzaliwa kwa mtoto TAMMUZ, pia iliaminika kwamba huyu mtoto ni mtakakatifu, kwakuwa mimba yake imetokana na mionzi ya jua, pia iliaminika kwamba Nimrod aliendelea kuzaa na mke wake huku akiwa katika jua. Yeremia 7:17-18 inaonyesha sherehe aliyofanyiwa katika kuzaliwa kwake (TAMMUZ),Sherehe hiyo iliridhiwa na wana wa Israel. Wakina baba na akina Mama na watoto wote walijumuika katika maandalizi ya sherehe hiyo kubwa. Yeremia 7:18, yeremia 52:31.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…